• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Friday, January 9, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Habari

Msigwa: Vita vya sasa duniani ni taarifa na si vifaru wala mabomu

Asema waandishi wa habari Tanzania sio dhaifu

by bajeti
December 19, 2025
in Habari
0
Msigwa: Vita vya sasa duniani ni taarifa na si vifaru wala mabomu

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Sanaa,Utamaduni na Michezo ambaye pia ni Msemaji wa Serikali ya Tanzania Gerson Msigwa

Share on FacebookShare on Twitter

NA GOODLUCK HONGO
WAANDISHI wa habari za mtandaoni wametakiwa kutumia kalamu zao kujenga nchi na sio kuzitumia kubomoa kwa kuwa vita vya sasa duniani havipiganwi kwa mabomu wala vifaru bali ni taarifa kupitia vyombo vya habari.

Mbali na hilo lakini pia waandishi wa habari wa Tanzania sio dhaifu kama inavyoelezwa bali hufanya kazi zao kwa kufuata sheria za nchi na vinginevyo.

Kauli hiyo imetolewa mkoani Dar es Salaam Desemba 18,2025 na Msemaji wa Serikali Gerson Msigwa wakati akifunga kikao kazi baina ya Mtandao wa Bloggers Tanzania (TBN) pamoja na Jumuiya ya Mitandao ya Kijamii Tanzania (JUMIKITA) yaliyoandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

Msigwa amebainisha kuwa taarifa zinazochapishwa ni muhimu zaidi kwa nchi kuliko hata kuwa na leseni kwani siku za nyuma mamlaka iliweka mbele katika kushughulikia wadau kuliko kuwasaidia lakini mwelekeo wa Serikali ya Awamu ya Sita sio kuwashughulikia bali ni kuwashirikisha na kuwaunga mkono ili waweze kutekeleza majukumu yao kama inavyotakiwa.

Msigwa ambaye ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,Sanaa,Utamaduni na Michezo ameongeza kuwa TBN na JUMIKITA wamefanya kazi nzuri na Serikali inatambua mchango huo.

“Kuna kasiasa kanapita kwamba waandishi wa habari wa Tanzania ni dhaifu,ninyi sio dhaifu wala mitandao ya kihabari ya Tanzania sio dhaifu kwa sababu nyinyi ni watanzania,mnaishi Tanzania na nchi yenu inapaswa iwe mahali salama na sio sehemu yenye hatari kwenu.

“Sisi tunafanya tathmini kwenye maudhui mnafanya kazi sahihi kwa sababu ninyi ni watanzania ,mnaishi Tanzania,tunawaomba mtumie kalamu zetu kujenga nchi na tusitumie kalamu zetu kubomoa nchi.

“Mheshimiwa Rais anawapongeza sana na sisi tuna maelekezo kutoka kwa Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwamba waandishi wa habari za mtandaoni wapewe fursa ili waweze kufanya kazi zao vizuri.

Msigwa amefafanuwa kuwa hali ikiharibika hakuna anayekuwa salama hivyo ni muhimu kuhakikisha kuwa taarifa zinazotolewa mitandao ni za kujenga na kuleta maendeleo kwa kuwa fedha zinazopatikana huwanufaisha kila mtu wakiwemo wao waandishi wa habari kwani nao ni sehemu ya jamii.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt.Jabir Shaban akizungumza na waandishi wa habari wa mtandaoni (hawapo pichani) kutoka TBN na JUMIKITA Desemba 18,2025 mkoani Dar es Salaam.Kushoto ni Mwenyekiti wa TBN Beda Msimbe

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt. Jabir Shaban amesema kwa sasa dunia iko katika zama za kidigiti na uchumi wake pia ni wa kidigiti.
Ameeleza kuwa waandishi wa habari wa mitandaoni wanawajibu mkubwa sana katika uchumi huo wa kidigiti ambao utasaidia pia kizazi kijacho na nchi kwa ujumla.

“TCRA tunaendelea kufanya maboresho ya kanuni kwa kuwa eneo hili la utangazaji linabadilika sana,utaratibu tuliokuwa nao sasa hivi ni wa kulea na utaambiwa umekiuka kanuni kwa kuelekezwa ili usirudie kosa na ufanye vizuri zaidi”ameongeza Dkt.Jabir

Katika Mkutano huo waandishi wa habari za mtandaoni wamependekeza masuala mbalimbali kwa Serikali ili kuboresha utendaji kazi wao ikiwemo gharama za leseni na upatikanaji wa mikopo ili kukuza taasisi zao.

Kauli ya Msigwa inaendana na baadhi ya mataifa yanayojinasibu duniani kwa kufuata sheria na kuwalinda waandishi wa habari wakichukua hatua kali dhidi ya waandishi na vyombo vya habari ambavyo vinaonekana kuharibu na kutishia amani na usalama wa nchi.

Siku kadhaa zilizopita Ikulu ya Marekani ilizindua ukurasa mpya kwenye tovuti yake rasmi ikiorodhesha kile inachokiita ‘Vyombo vya Habari Vihalifu’ ikishutumu baadhi ya taarifa kuwa ni za kupotosha na zenye upendeleo ambapo moja ya vyombo vilivyotajwa humo ni pamoja na CNN,CBS NEWS,msnbc na baadhi ya waandishi wa habari.

Wakati Marekani ikizindua ukurusa huo iliouita “Offender Hall of Shame,Urusi imelipiga marufuku Shirika la Utangazaji la Ujerumani (DW) kutokana na kile ilichoeleza taarifa zisizo sahihi kwa upande wa nchi hiyo.

Hayo yote yanafanyika ili kulinda usalama wa nchi hizo lakini yangetajwa na za kiafrika wangeshutumiwa kuwa wanakiuka haki za waandishi wa habari

 

Next Post
Balozi wa Palestina Tanzania ahimiza wanahabari  kushikamana na nchi yake dhidi ya madhila wanayofanyiwa na majeshi ya Israel

Balozi wa Palestina Tanzania ahimiza wanahabari kushikamana na nchi yake dhidi ya madhila wanayofanyiwa na majeshi ya Israel

TCRA,TBN na JUMIKITA wakutana kujadili changamoto zinazowakabili  

TCRA,TBN na JUMIKITA wakutana kujadili changamoto zinazowakabili  

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:0
  • Today's page views 0
  • Total visitors 12,989
  • Total page views 14,727

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In