• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Friday, January 9, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Habari

TCRA,TBN na JUMIKITA wakutana kujadili changamoto zinazowakabili  

by bajeti
January 2, 2026
in Habari
0
TCRA,TBN na JUMIKITA wakutana kujadili changamoto zinazowakabili  

Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Dkt.Jabir Shaban (kulia) akipokea nyaraka kutoka kwa Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanablog Tanzania (TBN) Beda Msimbe wakati wa kikao kazi kilichofanyika Desemba 18,2025 mkoani Dar es Salaam

Share on FacebookShare on Twitter

 

NA MWANDISHI WETU

MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imepokea maoni na ushauri uliotolewa na waandishi wa habari za mtandaoni ili kuboresha utendaji kazi na ushirikiano baina ya pande hizo mbili.

Mbali na hilo lakini pia TCRA haifurahishwi na mazingira ya kuvifungia vyombo vya habari vinavyotoa maudhui yake mtandaoni kwani dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita ni kuvikuza zaidi na sio kuvididimiza.

Kauli hiyo imetolewa mkoani Dar es Salaam  Desemba 18,2025 na Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Dkt.Jabir Shaban baada ya kupokea maoni mbalimbali yaliyowasilishwa na Mtandao wa Bloggers Tanzania (TBN) wakati wa kikao kazi kilichowajumuisha pia Jumuiya ya Mitandao ya Kijamii Tanzania (JUMIKITA) na TCRA.

Dkt.Jabir amesema TCRA imepokea maoni na ushauri wao na kwamba watayafanyia kazi kwa yale yaliyo ndani ya uwezo wao na yaliyo nje ya uwezo wao watayafikisha kwa wahusika.

Amesema Tanzania kama nchi ina sheria na desturi zake hivyo baadhi ya maudhui yanayowekwa katika mitandao sio sahihi kwa nchi lakini kwa nchi zingine kwao ni sawa.

“ Kwanza faini sio chanzo cha bajeti yetu sisi TCRA na inatusumbua sana kufika mahali kuwalipisha watu faini na tungependa kuona mnafanyakazi zenu vizuri.

“ Kuhusu suala la ada ya leseni kulitoa hapa lilipo mimi sina shaka nalo kabisa lakini mimi ningependa unapoingia katika mafunzo(trainning) uingie ukiwa fulani na utoke ukiwa tofauti”amesema Dkt Jabir

Kwa upande wake Mwenyekiti wa TBN Beda Msimbe amesema waandishi wa habari za mtandaoni wanamchango mkubwa kwa Taifa kwa kuhakikisha kuwa taswira ya Tanzania inang’ara kimataifa.

Amesema TBN wamefanikiwa Kutangaza Utalii na Utamaduni na kuonyesha vivutio vya nchi kwa hadhira ya ndani na nje ya nchi,Habari Chanya (Positive Narrative): Kujaza nafasi ya mtandaoni na taarifa zinazojenga taswira nzuri ya nchi, maendeleo ya kiuchumi, na fursa za uwekezaji. na kuwa diplomasia ya kidijitali kwa kuwa daraja kati ya serikali, sekta binafsi, na wananchi katika kusambaza taarifa muhimu kwa haraka.

Akizungumzia kuhusu mfanikio Msimbe amebainisha kuwa Tuzo na
Ufanisi wa TBN unajidhihirisha kupitia ubora wa kazi za wanachama wake ambapo wanajivunia wadau ambao wameshinda tuzo mbalimbali za uandishi wa habari na ubunifu wa kidijitali (ndani na nje ya nchi).

“Tuzo hizi ni ushahidi kuwa blogu za Kitanzania si vyanzo vya habari tu, bali ni taasisi za kitaaluma zinazozingatia ubunifu na weledi.

Msimbe amebainisha kuwa pamoja na kazi kubwa inayofanywa, wanachama wa TBN wanakabiliwa na vikwazo vya kisheria na kifedha ambavyo vinahatarisha uendelevu wa kazi zao ikiwemo gharama kubwa za leseni kwani ada za sasa za usajili wa maudhui mtandaoni (Online Content License) ni mzigo mkubwa kwa wanablogu wadogo na wa kati.

“Hali hii inasababisha baadhi ya wabunifu kushindwa kurasimisha kazi zao au kuacha kabisa taaluma hii.

“Tanzania sio kisiwa na tunapoeleza changamoto zetu ni muhimu pia kujilinganisha na watu wengine kwani katika nchi zingine blog hutambuliwa kama biashara ndogo”amesema Msimbe

Waandishi wa habari za mtandaoni wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt.Jabir Shaban wakati wa kikao kazi kilichofanyika Desemba 18,2025 mkoani Dar es Salaam

Naye Mwenyekiti wa JUMIKITA Shabani Matwebe ameongeza kuwa mitandao ya kijamii haitambuliki katika mifumo ya uombaji wa tenda yakiwemo matangazo licha ya kuwa na mamilioni ya watu wanaowafuatilia katika mitandao yao.

“Tunaomba basi mifumo itutambue rasmi digital platform iwepo kwenye mifumo ya watu wanaoomba tenda za utangazaji.

“Tunalipa ada ya mwaka 500,000 na youtube  wanakata asilimia 30 na sasa wakati huo facebook ,instagram ,tiktok wanalipa katika nchi zingine kama Kenya na Afrika Kusini na Tanzania tumeona facebook wanaanza kulipa  basi kuwepo na nguvu ya kuhakikisha kuwa instagram na social media zingine walipe lakini Instagram hawalipi kabisa wakati kuna watu wanawafuasi 1,000,000 5,000,000 hadi 10,000,000 lakini wapo tu pale na kama hakuna mtu wa kutangaza chochote ipo tu pale.

“Lakini wenzetu Kenya mtu akiwa na wafuasi 100,000 anapata fedha nyingi kuliko hata mfanyakazi wa CRDB benki lakini sasa mmeanza tena kukata kodi kwenye facebook,sasa Instagram ikianza kulipa nayo mtakata kodi na 500,000 tena tutoe sasa hii ni kama double tax”amebainisha Matwebe

Kama tunasajili kwa 500,000 na kila mwaka tunalipa 500,000 sasa hayo makato ya facebook,youtube na hayo mengine mnayotarajia kukata.

Waandishi wa habari za mtandaoni wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt.Jabir Shaban wakati wa kikao kazi kilichofanyika Desemba 18,2025 mkoani Dar es Salaam

Hata hivyo Matwebe ameongeza kuwa ni muhimu kuwa na mfuko wa waandishi wa habari  ili waweze kupata mikopo itakayowawezesha waandishi wa habari za mtandaoni ikiwemo kubadilisha kanuni za kulipishwa adhabu ya 5,000,000

 

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:0
  • Today's page views 0
  • Total visitors 12,989
  • Total page views 14,727

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In