• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Friday, May 29, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Habari

Waziri Mkuu Mwigulu awahimiza watanzania kujiunga na Bima ya Afya kwa Wote

by bajeti
January 29, 2026
in Habari
0
Waziri Mkuu Mwigulu awahimiza watanzania kujiunga na Bima ya Afya kwa Wote

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Mwigulu Nchemba

Share on FacebookShare on Twitter

NA GOODLUCK HONGO

WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Mwigulu Nchemba amesema Bima ya Afya kwa wote limekuwa hitaji la wananchi wa Tanzania kwa muda mrefu na kujiunga kutawawezesha kumudu masuala ya matibabu.

Amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan katika uongozi wake wa awamu ya kwanza alielekeza taratibu zote za masuala ya kisheria  ziweze kukamilika.

Katika ahadi na Maelekezo ya Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) 2025-2030   imeeleza kuwa Chama kinatambua kuwa huduma bora za afya ni haki ya msingi ya kila Mtanzania kama mtaji wake wa kwanza wa kujiendeleza.

Aidha Ilani hiyo imeongeza kuwa huduma bora za afya ni muhimu katika kuhakikisha wananchi wanakuwa na afya bora ili kuwawezesha kushiriki katika shughuli za maendeleo na kuboresha maisha yao.

“Katika kuendelea kuimarisha huduma za afya nchini, katika kipindi cha utekelezaji wa Ilani hii, Chama kitaielekeza Serikali  kutekeleza programu na Sheria ya Bima ya Afya kwa Wote (Universal Health Insurance)”imebainisha Ilani hiyo

Hata hivyo Sheria ya Bima ya Afya kwa Wote ilipitishwa rasmi na Bunge Novemba Mosi,2023 na kuchapishwa katika gazeti la Serikali la Desemba Mosi ,2023 ambapo Bima ya afya itakuwa ni ya lazima kwa watu wote.

“Kwa kuzingatia masharti ya Sheria hii, kila mtu anapaswa kujiunga na skimu ya bima ya afya ili kuhakikisha anapata huduma za afya,Kila mwajiri atatakiwa kumchangia mwajiriwa wake katika skimu ya bima ya afya kiwango cha uchangiaji

“Kwa kuzingatia masharti ya Sheria hii,Wageni wote wenye umri wa miaka kumi na nane au zaidi wanaoingia nchini na kukaa zaidi ya siku thelathini ambao hawana bima ya afya inayotambulika nchini watapaswa kujiunga na bima ya afya kwa mujibu wa Sheria hii”Imefafanua Sheria hiyo

Akizungumza bungeni jijini Dodoma Januari 29,2026 wakati wa maswali ya papo kwa hapo na Waziri Mkuu katika Bunge la 13 Mkutano wa pili kikao cha tatu,Dkt Mwigulu amebainisha kwamba hatua iliyosalia sasa ni ya kutoa elimu na  kujiunga na Bima ya Afya kwa Wote ni jambo la msingi ambalo litawawezesha watanzania wote kuweza kumudu masuala ya matibabu.

“Jambo kubwa ambalo tunatakiwa kufanya ni kujiunga kwenye vitita hivyo ambavyo vimeelekezwa na Wizara ya Afya na baada ya kujiunga upande wa Serikali tunafanya kila jitihada kuhakikisha huduma hizo za afya zinapatikana kwa ukaribu  na uhakika ili kuweza kuhakikisha kwamba kwa yeyote ambaye amejiunga na Bima ya Afya anapata matibabu ya chochote kile kinachomsumbua tena kwa uhakika bila usumbufu”amesema Dkt Mwigulu 

Dkt.Nchemba ameeleza kuwa katika maandalizi hayo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliahidi ndani ya siku 100 ataongeza wahudumu wa afya na wataajiriwa wahuduma wa afya 5000

“Hivi tunavyoongea tayari wataalamu hao 5000 walishaajiriwa na wamepelekwa kwenye Zahanati zetu ,vituo vyetu vya afya ,hospitali zetu ili kuweza kuhakikisha kwamba mbali na majengo mazuri aliyoyajenga Daktari Samia Suluhu Hassan pia tunakuwa na wahudumu na wataalamu wa afya wa kutosheleza katika maeneo ya hospitali zetu na hili linaenda sambamba na upatikanaji wa vifaa vya kisasa ambavyo kwa sasa vinapatikana kwenye hospitali zetu zote.

“Zamani baadhi ya vifaa vilikuwa vinapatikana tu kwenye Hospitali zilizopo Dar es Salaam,ukitaka MRI Dar es Salaam,ukitaka Cit Scan Dar es Salaam,hivi tunavyoongea kila Hospitali ya Mkoa ina vifaa hivyo vya Cit Scan,masuala ya Ultra Sound na imeenda hadi katika hospitali zetu za Halmashari na Wilaya na  masuala ya MRI sasa yanapatikana hata kwenye hospitali zetu za Kanda na Rufaa”amefafanuwa Dkt.Mwigulu

Aidha ameongeza kuwa ni hatua kubwa ambayo Serikali imefanya ambayo inawahakikishia watanzania watakaojiunga na Bima ya Afya watakuwa wameweka utaratibu wao  wa undugu wa kuweza kujihakikishia kwamba wanapata matibabu.

“Nitoe rai kwa waheshimiwa wabunge,madiwani na viongozi wengine wote tuendelee kuelimishana,tuendelee kuelimisha makundi mbalimbali,tuendelee kuwaelimisha watanzania juu ya jambo hili kubwa ambalo lina manufaa makubwa na mapana kwa jamii nzima ya Tanzania.

“Nianzie hapa hapa kutoa rai kwa kwa watanzania wote kwamba kujiunga na Bima ya Afya kwa Wote ni jambo la msingi ambalo litatuwezesha watanzania wote kuweza kumudu masuala ya matibabu,kuweza kuchangia matibabu ya wale ambao wanauhitaji mkubwa wa matibabu na pengine wanaweza wasimudu kulipia matibabu hayo”amebainisha Dkt.Mwigulu

Awali akimuuliza swali Waziri Mkuu Mwigulu,Mbunge wa Viti Maalum wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Ritha Kabati ambaye awali aliiponge za Serikali juu ya mfumo huo wa Bima ya Afya kwa Wote lakini alitaka kujua jinsi Serikali ilivyojipanga kutoa elimu ya Bima ya Afya kwa Wote hadi vijijini.

Next Post
Kasi ya Air Tanzania  ‘kupasua anga la dunia yatisha’

Kasi ya Air Tanzania  'kupasua anga la dunia yatisha'

Tanzania nchi ya tano duniani kwa kujenga Reli ndefu ya kisasa (SGR)

Tanzania nchi ya tano duniani kwa kujenga Reli ndefu ya kisasa (SGR)

Wilaya 75 hazina vituo vya Polisi ikiwemo Maswa

Wilaya 75 hazina vituo vya Polisi ikiwemo Maswa

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:10
  • Today's page views 10
  • Total visitors 16,603
  • Total page views 18,841

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In