• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Monday, June 1, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Sayansi na Teknolojia

Udhibiti vidukari katika zao la mpunga utakavyoimarisha usalama wa chakula.

Atajwa kupatikana pia katika bamia.

by bajeti
June 1, 2026
in Sayansi na Teknolojia
0
Udhibiti vidukari katika zao la mpunga utakavyoimarisha usalama wa chakula.

Mtafiti (Mtaalam wa Maaara) katika Idara ya Kilimo Sayansi za Ufugaji wa Nyuki Katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM-CoAF) Wilson Masele

Share on FacebookShare on Twitter

 

NA GOODLUCK HONGO

MPUNGA ni moja ya zao muhimu zaidi la chakula nchini Tanzania linaloshika  nafasi  ya pili baada ya mahindi huku mtama ukishika nafasi ya tatu.

Zao hili la chakula na biashara hulimwa kwa wingi katika mikoa karibu yote ya Tanzania ikiwemo Mtwara,Dodoma,Lindi, Shinyanga, Mbeya, Morogoro, Kilimanjaro, Mwanza, Tanga na Pwani,

Kwa mujibu wa wa Sensa ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi ya Mwaka wa Kilimo 2019/20 iliyotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu(NBS) imeonesha kuwa eneo lililopandwa mpunga lilikuwa na jumla ya hekta 1,700,701 sawa na asilimia 23.7 ya eneo lililopandwa nafaka  ambapo (wakulima wadogo walipanda hekta 1,688,241 na mashamba makubwa walipanda hekta 12,460)

Hata hivyo uzalishaji wa zao la mpunga ulifikia tani 3,443,605 ambapo (wakulima wadogo walizalisha tani 3,380,715 na mashamba makubwa tani 62,890.

Pamoja na umuhimu mkubwa wa zao hilo linaloshika nafasi ya pili baada ya mahindi kwa uzalishaji,linatumika pia kama zao la chakula na hapo hapo ni zao la biashara ambapo inadaiwa  kuwa asilimia kubwa hupotea wakati wa kuvunwa,kuhifadhi na usafarishaji.

Ni mara chache sana kusikia habari kuhusu wadudu wanaoshambulia zao hilo kutoka kwa wakulima ingawa wengi hutumia dawa ya kuuwa magugu ili kulinusuru katika ukuaji wake.

Kutokana na umuhimu wa zao hilo kwa chakula na biashara, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kimefanya utafiti na kugundua kuwa zao hilo pia linashambuliwa na mdudu anayejukana kama Kidukari, hivyo kuwatia hasara wakulima wa zao hilo.

Akizungumzia kuhusu utafiti huo,Mtafiti (Mtaalam wa Maaara) katika Idara ya Kilimo Sayansi za Ufugaji wa Nyuki Katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM-CoAF)  Wilson Masele anasema Vidukari wanaathiri zaidi miwa lakini wao wamejikita katika kufanyia utafiti zao la mpunga.

Anasema mwanzo mdudu huyo alikuwa akishambulia zaidi miwa na aligundulika  mwaka 2006 nchini Morocco ambapo mwaka 2013 aligundulika nchini Afrika Kusini na Kenya alionekana mwaka 2016 na kwa mara ya kwanza Tanzania aligundulika   mwaka 2020.

Anasema Miwa kwa mara ya kwanza ndio ilionesha dalili za kushambuliwa lakini baada ya hapo hakukuwa na taarifa nje ya zao la Miwa kwamba  kuna zao gani lingine ambalo mdudu huyo anaathiri hivyo kukawa na changamoto juu ya zao lingine ambalo anaathiri.

Anasema waliona lazima ufanyike utafiti japokuwa baadhi ya maandiko yalionesha kuwa miwa ilikuwa ikishambuliwa na huyo mdudu na  hapo ndio utafiti ulipoanzia.

Anasema Miwa ni zao la biashara lakini Mpunga pamoja na ni kwamba ni zao la biashara lakini ni zao pia la chakula,sasa namna anavyoathiri Muwa akienda kuathiri Mpunga,Nchi itakuwa imeathirika na usalama wa chakula kwa kiasi kikubwa.

“Anachokifanya huyu mdudu,yeye anakwenda kufyonza utomvu,anaenda kuzuia mmea kutengeneza chakula chake (Photosythesis),anazuia mwanga wa jua  usiweze kusaidia mmea katika kutengeneza chakula chake.

“Wakulima wengi wametoa taarifa za athari kubwa kwa maeneo hayo kwa sababu Mpunga ambao umeathiriwa unatengeneza mapepe zaidi na inapunguza uzalishaji kwa kiasi kikubwa sana.

“Kwa bahati mbaya anazaliana sana,mvua ikinyesha anadondoka hivyo anaweza kusababisha hasara ya asilimia 90 hadi 100”anaeleza Masele

Masele anasema hapo ndio wakaamua kuingia katika utafiti wa kumchunguza huyo mdudu ili kujua anapatikana wapi na mazingira gani,wadudu wanaoweza kumuathiri au kumuua,na kujua mazingira anayopendelea zaidi  na  ndipo wanapotafuta mbinu ya kumdhibiti asiweze kuathiri zaidi mazao mbalimbali hasa Mpunga.

Masele anaongeza kuwa utafiti juu ya Miwa unaendelea chini TARI   na wao kwa kushirikiana  na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kupitia Idara ya Kilimo ndio wakaunda timu ya kuendesha utafiti kwenye zao la Mpunga.

Masele anabainisha kuwa kupitia Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) wakawa wamefanikisha andiko lao kupita na ikabidi waanze kazi na wakachagua mikoa ambayo inazalisha sana Mpunga japo kwa Tanzania sasa hivi karibu mikoa yote wanalima Mpunga.

“Lakini tulitafuta mikoa kama 17 ambayo wanazalisha Mpunga kwa kiasi kikubwa ili tujue kwenye Mpunga huyu Kidukari ameshafika?Tulifanya Surveyor mwaka jana.

“Kwenye mikoa hiyo 17 na Wilaya kama 34 ambapo timu ziligawanyika katika makundi matatu ili kuendana na muda lakini pia mazingira.

“Mdudu huyu anatabia moja,kipindi cha mvua ni rahisi kutoonekana na kwa sababu anakuwa anajificha zaidi chini,haonekani juu kwa hiyo mvua ikinyesha anaondoka”anasema Masele

Aidha anafafanuwa kuwa hatua anayoonekana zaidi  ni kipindi kile ambacho Mpunga umechanua na haujaanza kukomaa.

“Maeneo ambayo tulitembelea Bukoba tulimuona huyu mdudu,Morogoro alionekana,Kilimanjaro,lakini na Manyara,mikoa hiyo huyu mdudu alionekana”anaongeza Masele

Masele anaeleza kuwa yeye anazuia mmea kujitengenezea chakula chake na shamba ambalo limeathiriwa na mdudu huyo linakuwa  na mapepe mengi na anakuwa na nguvu zaidi kipindi cha kuchanua hivyo mpunga hauwezi kujaza ambapo ikiwa mkulima ana hekari moja basi anaweza kuvuna gunia moja na ukienda kupeta unakuta hakuna kitu.

Anasema hata maeneo ambayo hawakufika lakini wakulima waliwaambia kuwa walishawahi kumuona mdudu huyo hata hivyo wadudu hao wako wa aina mbalimbali lakini huyo wamemuita Aphitis.

“Tulikusanya taarifa na wadudu wengine wanaopatikana katika mashamba yale ili kujua hao wadudu wanamahusiano gani na huyo mdudu kitaalam zaidi na walichukua mfano wa Mpungapori ili kujua kama ni kinzani juu ya mdudu huyu.

“Kama nilivyosema lengo ni kumdhibiti hivyo tulichukua aina ya Mpungapori,wadudu wanaopatikana kwenye mazingira ambayo mpunga umelimwa  na kisha kuandika taarifa rasmi.

“Pia tulikuwa na wanafunzi ngazi ya Uzamili kwa maana ya Masters na Uzamivu kwa maana ya PHD hivyo tunawanafunzi watatu,wawili Uzamili(Masters) na mmoja Uzamivu(PHD)  na kila mmoja ana kitu anachokifanya ambapo mmoja anatafiti mbinu za kiasili za kumdhibiti huyu mdudu”anasema Masele

Akizungumzia kuhusu kumdhibiti mdudu huyo kwa mbinu za asili,Masele anaeleza kuwa kuna mbinu za asili wamekuwa wakisikia kama kutumia mwarobaini na nyingine hivyo kuna mmoja ambaye anaangalia hilo lakini kuna mwingine anaangalia mpunga ambao utakuwa ni kinzani juu ya hao wadudu na mwingine anaangalia jinsi ya kutumia kuchanganya kemikali katika kumdhibiti.

“Wanafunzi wawili wameshapita katika ngazi za kitaaluma na dodoso zao zimeshapitishwa kwa maana ya kwenda kukusanya taarifa  na mwingine anamalizi kazi zake na mwezi wa saba atakuwa amekamilisha andiko lake na ataenda sasa kufanyia kazi.

“Lengo la mwisho wa haya yote ni kupata bidhaa(product) ambayo tunategemea tupate mpunga ambao ni kinzani kwa huyu mdudu lakini pia tupate dawa ambayo itaweza kutumika kumdhibiti huyo mdudu,na hayo ndio malengo makubwa ya huu mradi wetu ”anasema Masele

Mtafiti (Mtaalam wa Maaara) katika Idara ya Kilimo Sayansi za Ufugaji wa Nyuki Katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM-CoAF) Wilson Masele (wa sita kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya waandishi wa habari pamoja na maofisa waandamizi kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi naTeknolojia (COSTECH) mara baada ya kutembelea Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) hivi karibuni

Utafiti na Dira na Maendeleo 2050

Akizungumza malengo ya nchi kupitia Dira ya Maendeleo ya 2050,Masele anasema mradi wao unaingia moja kwa moja kwenye sera ya nchi kwa maana ya usalama wa chakula ni sehemu sahihi kwa maana ya viwanda lakini pia wanaweza kupata dawa ambayo wawekezaji wakawa watanzania na wakazalisha zaidi lakini pia kuongeza maarifa kwa watanzania.

“Huu utafiti timu yote ni wataalam wa ndani kwa maana hiyo,tunao uwezo na maabara ambazo zinaweza zikafanya mambo makubwa na kupata suluhisho bila kutegemea kutoka nje”anasema Masele

Masele anabainisha kuwa madhara ya moja kwa moja kwa binadamu wanayapima kwa kuathiri usalama wa chakula.

Hata hivyo Masele anaongeza kuwa wao hawajaangalia zao la Mpunga pekee lakini waliangalia na wapi pengine anaweza kujificha mdudu huyo na waligundua pia katika Mkoa wa Morogoro ameonekana katika zao la bamia lakini pia katika majani mengine ambayo hayatumiki kama chakula hivyo ni mazingira mengine ambayo anaweza kujificha.

“Sisi tulienda zaidi na tukaangalia athari kwenye mpunga lakini mazingira sasa anaweza kupatikana katika mazingira tofauti tofauti  na tukishajua kwamba anapatikana katika mazingira tofautitofauti ina maana hata namna ya kukabiliana naye ni rahisi kwa sababu tutakuwa tumeshajua kwamba huyu anafuatilia zaidi jamii ya nyasi kwa mfano,tunaangalia njia ya kudhibiti kwenye eneo hili.

“Au huyu mdudu anapenda jamii ya mikunde kwa mfano basi twendeni na njia hii,kwa hiyo tunafanya kitu ambacho sio kwenye mpunga bali pia na mazingira mengine ambayo anaweza kupatikana ili tuweze kumdhibiti vizuri “anasema Masele

Sera ya Elimu ya Amali

Akizungumzia kuhusu Sera ya Elimu ya Amali,Masele anasema hilo ndio eneo wanalofanya vizuri zaidi ikiwemo kuwawezesha hao wanafunzi kwa kuwa wengi wao hawana uwezo kulipia tafiti.

“Wanafunzi tumewashirikisha kuanzia mwanzo tunapokea mradi  na tulipokea maombi ya wanafunzi 17 waliokuwa na maandiko na tuliyashindanisha na tukapa wanafunzi watatu  na wote 17 walikuwa na uwezo lakini kwa sababu ya bajeti tuliweza kuwachukua wanafunzi watatu.

“Bajeti ya mwanafunzi wa PHD hapa haipungui Sh.Milioni 20  na ni miaka mitatu na  kwa mwanafunzi wa Masters bajeti yake haipungui Sh.Milioni 10 na ni miezi 18  na hawawezi kumaliza hadi wakamilishe tafiti zao ndio watatunukiwa.

“Lakini pamoja na hayo hao watatu walikuwa wanaenda moja kwa moja kwenye malengo ya mradi na tukaona hapo tunaweza tukapata bidhaa(product)”anabainisha Masele

Hata hivyo Masele anaeleza kuwa wakiendelea kupata uwezeshaji wa kifedha basi na hao wengine wanaweza kuongezea pengine hata yale mazao mengine badala ya mpunga.

“Tunaamini Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika kutekeleza Sera ya Elimu tunaweza kuendeleza pale ambapo tutakuwa tumeishia,hivyo tunawakaribisha zaidi wawekezaji”anaongeza Masele

Watumia wa juisi ya miwa

Akizungumzia kuhusu wadudu hao katika miwa na athari zake kwa watumiaji wa juisi ya miwa,Masele anabainisha kuwa bado hawajafanya utafiti juu ya eneo hilo lakini wanalipokea.

Uwezeshwaji kutoka COSTECH

Akizungumzia fedha walizopata kutoka Tume Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) Masele anaongeza kuwa wao walipokea kiasi cha Sh.Milioni 301.9 kutoka COSTECH ambapo pia ilikuwa pungufu na bajeti waliyoiomba na kulazimika kupunguza baadhi ya vitu ili kuendana na hiyo bajeti waliyopokea.

“Tunaishukuru Serikali kupitia COSTECH kwa kutupatia kiasi cha Sh.Milioni 309 .9  na kama fedha zaidi zitapatikana sasa zile bidhaa zetu zinaweza kufanyiwa kitu kinaitwa commercialization bidhaa zetu zikaingia sokoni.

“Sasa kutoka hapa kwenda mbele zaidi kunahitajika uwezekaji zaidi hivyo nashauri kwamba hizi tafiti zilizowezeshwa na COSTECH zisiishie tu kwenye ile fedha ya awali na kuwe na mkakati wa kuziendeleza na wawekezaji wakiingia waoneshwe kuwa hapa kuna kitu kinatakiwa”anasema Masele

–

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:40
  • Today's page views 45
  • Total visitors 16,706
  • Total page views 18,963

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In