NEW YORK,MAREKANI
KAMPUNI ya Boeing ya Marekani inayotengeneza ndege imesitisha zoezi la kuzipeleka kwa wateja wake kutoka sehemu mbalimbali duniani ndege aina ya 787 Dreamliner kutokana na ukaguzi unaoendelea kufanywa na Mamlaka ya Anga ya Marekani(FAA)
Kwa mujibu wa taarifa iliyotangazwa na Sauti ya Amerika (VOA) kutoka nchini Marekani Februari 24,2023 ikinukuu taarifa ya FAA imeeleza kuwa sababu za kusitishwa huko kunatoka na FAA kufanya ukaguzi juu ya bodi za ndege hizo.
Ndege hizo hazipelekwa kwa wateja tena hadi FAA itakapojiridhisha kuwa kasoro hiyo imeshughulikiwa,
Hata hivyo FAA imesema inashirikiana na Boeing kubaini hatua zote zinazohitajika kuchukuliwa kwa ndege zilizopelekwa kwa wateja hivi karibuni.
Awali Jarida la Wall Street liliripoti awali kwamba Boeing haijakabidhi kwa wateja ndege aina ya Dreamliner tangu Januari 26,2023 kutoka kwa viwanda vya utengenezaji au maghala yake ambapo ndege nyingi zimehifadhiwa zikizubiri kupelekwa kwa wateja kwa sababu ya suala hilo la ukaguzi




Discussion about this post