NA MWANDISHI WETU,
WAZIRI Mkuu Mstaafu wa Tanzania Edward Lowasa amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 70 leo jijini Dar es Salaam baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Lowassa alikuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kati ya mwaka 2005 na 2008, akihudumu chini ya Rais Jakaya Kiwete kabla ya kuamua kujiuzulu wadhifa huo .
Lowasa alizaliwa,jijini Arusha na kupata watoto wane ambao ni Bernad,Pamela,Adda na Fredrick Lowasa.
Kifo cha Lowasa kimetangazwa leo Februari 10,2024 na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzanzania Dkt.Philip Mpango.




Discussion about this post