• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Tuesday, January 13, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Habari

Makamu wa Rais Dkt.Mpango ataka wanawake kujitokeza katika kugombea nafasi za uongozi

awasihi watanzania kushiriki mazoezi yote ya uchaguzi

by bajeti
October 12, 2024
in Habari
0
Makamu wa Rais Dkt.Mpango ataka wanawake kujitokeza katika kugombea nafasi za uongozi

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akishiriki zoezi la Uandikishaji kwenye Daftari la Wapiga kura kwaajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika Kitongoji cha Kihanga Kijiji cha Kasumo Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma Oktoba 12,2024.

Share on FacebookShare on Twitter

NA MWANDISHI WETU,KIGOMA

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango na Mwenza wake Mama Mbonimpaye Mpango wameshiriki zoezi la Uandikishaji kwenye Daftari la Wapiga kura kwaajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika Kitongoji cha Kihanga Kijiji cha Kasumo Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma.

Akizungumza na wanakijiji wa Kasumo Oktoba 12, 2024 mara baada ya kujiandikisha, Makamu wa Rais Dkt.Mpango amesema zoezi la kujiandikisha katika daftari la kupiga kura ni muhimu kwa kuwa ni wajibu kushiriki katika kuchagua viongozi watakaoweza kuwasaidia wananchi.

Amesema viongozi wa Serikali za Mitaa ndiyo wanaoishi jirani zaidi na wananchi hivyo ni muhimu kushiriki katika kuwachagua wale watakaolinda maslahi ya jamii husika.

Makamu wa Rais ameongeza kwamba upatikanaji wa viongozi wazuri unaanza kwa kujiandikisha na baadae kujitokeza kupiga kura hivyo amewasihi kushiriki kikamilifu katika mazoezi yote ya uchaguzi yanayotarajiwa hivi karibuni.

Halikadhalika Makamu wa Rais ametoa wito wa kipekee kwa wanawake kujitokeza katika kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kwa kuwa wanazifahamu vema changamoto za jamii na pia wanao uwezo wa kuongoza vizuri.

Amesisitiza wananchi kushiriki vema chaguzi zote kwa amani na utulivu kwa kujiepusha na lugha zisizo na staha pamoja na vurugu wakati wa kampeni.

Next Post
Rais Dkt Samia awasili Mwanza kushiriki kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru 2024

Rais Dkt Samia awasili Mwanza kushiriki kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru 2024

Rais Dkt. Samia ateta na mkwe wa Hayati Rais Dkt.John Magufuli

Rais Dkt. Samia ateta na mkwe wa Hayati Rais Dkt.John Magufuli

Dkt. Diallo awataka wakulima kuzingatia matumizi sahihi ya mbolea

Dkt. Diallo awataka wakulima kuzingatia matumizi sahihi ya mbolea

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:9
  • Today's page views 9
  • Total visitors 13,065
  • Total page views 14,810

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In