• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Friday, December 5, 2025
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Siasa

Wamiliki wa  nyumba kuzuiwa kujenga frame za maduka katika maeneo ya makazi

Kutenga sehemu na barabara maalumu kwa biashara

by bajeti
November 8, 2025
in Siasa
0
Share on FacebookShare on Twitter

NA MWANDISHI WETU

CHAMA Cha Sauti ya Umma (SAU) kimesema Serikali yake haitaruhusu wenye nyumba kujaza frame za maduka  ya biashara katika maeneo ya makazi

Hata hivyo Serikali ya SAU itatenga sehemu maalum na kujenga barabara zitakazotumika kwa ajili ya biashara.

Kwa mujibu wa Ilani ya Chama hicho  yenya kauli mbinu Amani,Uadilifu na Maendeleo iliyopitishwa April 28,2025  yenye nguzo muhimu za Kilimo, Viwanda na Teknolojia inaeleza kuwa ni Ilani ya ukombozi kwa mtanzania ambapo juu ya nguzo hizo SAU  inakwenda kuboresha maisha ya watanzania na maendeleo ya taifa.

“Ilani hii ni mtiririko wa ahadi za chama kwa wapiga kura na watanzania wote, inaonyesha dira, maadili, sera na mipango ya chama katika kipindi cha miaka mitano ya utawala na kwa jinsi gani tutaweza”imefafanuwa Ilani hiyo

Kwa upande wa masuala ya ardhi,SAU imebainisha kuwa upimajiwa  ardhi umesuasua na kupelekea kutokea dhuluma na kesi nyingi ambazo hazikupaswa kutokea ambapo wakati mwingine watendaji wa wizara husika wanakuwa chanzo cha gomvi hizo.

“Chama cha SAU kupitia Serikali yake kitahakikisha kila ardhi ya Tanzania inapimwa, inamilikishwa na kulipiwa kodi. Hii itaondoa ugomvi na kuongeza pato kwa taifa na wale ambao hawana matumizi ya ardhi hawatakubali kukaanayo pasipo izalisha.

“Kurekebisha wizara  ya ardhi na kuweka wafanyakazi waadilifu ili kuondoa malalamiko na dhuluma za ardhi kwa wananchi mbalimbali”imeongeza Ilani hiyo

Ilani hiyo imeeleza kuwa Serikali ya SAU itatumia vyema ardhi kubwa iliyopo kwa kuhusisha wawekezaji wakubwa wa ndani na nje ya nchi, katika kilimo na viwanda ili ajira nyingi zaidi zipatikane na uuzaji mkubwa wa bidhaa nje ya nchi.

“Kodi ya majengo kwa nyumba za makazi itafutwa kabisa na kutokuruhusu ujenzi wa  maduka ya biashara katika maeneo ya makazi.

“Sehemu na barabara maalumu zitatengwa badala ya kila mwenye nyumba kujaza frame za maduka mbele ya nyumba yake.

“Vikundi vya kina mama vicoba vitapewa ardhi bure ili wawekeze katika kilimo, ufugaji, uvuvi, majengo kama hostel n.k na kupunguza gharama za vifaa vya ujenzi”imebainisha Ilani hiyo

Ilani hiyo imeonesha kuwa Serikali ya SAU itajenga nyumba bora za gharama nafuu 200,000  za makazi vijijini ambazo zitajengwa katika kipindi cha miaka mitano, kwa kushirikiana na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Sekta binafsi, taasisi za fedha na viwanda vya vifaa vya ujenzi.

“Tutaanzishwa kampeni maalum vijijini ya nipe mazao au mfugo nikupe nyumba bora katika eneo lako. Lengo ni kuhakikisha watanzania wanaishi maisha bora”imeeleza Ilani hiyo

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho Betha Mpata amesema Ilani imefafanua ni jinsi gani Chama cha Sauti ya Umma  kitakavyo mhudumia mtanzania endapo atakipa mamlaka ya kushika dola kwa kuwapa wagombea wake kura nyingi za ndio  katika uchaguzi  mkuu wa mwaka 2025.

“Kama Mwenyekiti wa Chama cha Sauti ya Umma (SAU), pamoja na viongozi wenzangu wa chama chetu, tunayo dhamira ya dhati ya kuleta mabadiliko na maendeleo na kujenga mustakabali mzuri kwa wote.

“Sambamba na kulinda muungano wetu na kukuza umoja na mshikamano  miongoni mwa watanzania na waafrika.

“Ilani hii ni zaidi ya hati ni ahadi, ahadi ya kupigania haki zako na kufanya kazi bila kuchoka ili kuunda jamii yenye haki, jamii yenye maendeleo na jumuishi.”amesema Mpata

Hata hivyo Mpata amebanisha kuwa Ilani yao  ni ramani ya mabadiliko wanayoyahitaji kwa pamoja na kupitia SAU wanaweza kushinda changamoto za leo na kujenga kesho iliyobora ambayo wote wanaweza kujivunia.

“Rai yangu, ninawaomba sana muungane nasi na mchukue maamuzi sahihi ya kuiamini na kuichagua kwa kura nyingi Chama cha Sauti ya Umma (SAU)  ili kupata mustakabali bora kwa ajili yetu na kwa vizazi vijavyo”ameongeza Mpata

Katibu Mkuu wa SAU na Mgombea wa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Majalio Kyara amesema amekuja kwa watanzania  si tu kama mgombea Urais wa Jamhuri  ya Muungano wa Tanzania, lakini pia kama mtanzania anayeelewa changamoto zinazowakabili na kesho wanayoitamani.

“Nchi yetu imebarikiwa kuwa na ardhi yenye rutuba, rasilimali nyingi na idadi nzuri ya vijana wanaotaka kuchangia maendeleo yetu ya pamoja.

“Hata hivyo, hatuwezi kupuuza hali halisi ya umaskini, ukosefu wa ajira na miundombinu duni ambayo inazuia ukuaji wetu.

“Nguzo zetu kuu za Kilimo, Viwanda na Teknolojia katika Ilani hii ya 2025 – 2030, zitawezesha kusukuma maendeleo, kudumisha jamii zetu, upatikanaji wa  ajira na maendeleo kwa vijana wetu”amebainisha Kyra

Kayra ameongeza  kuwa wanatazamia Taifa ambalo hakuna aliyesalia nyuma ambapo ndoto za vijana, hekima za wazee, na bidii za wakulima, wafanyakazi na wajasiriamali zinauungwa mkono.

Watanzania wanatarajiwa kupiga kura katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29,2025 na kuwachagua wagombea wa nafasi ya Urais,Ubunge na Udiwani  watakaodumu kwa muda wa miaka mitano hadi 2030 utakapoitishwa uchaguzi mwingine.

Next Post
Mradi wa Maji wa Miji 28 mkoani Niombe utakavyoondoa changamoto ya maji safi na salama

Mradi wa Maji wa Miji 28 mkoani Niombe utakavyoondoa changamoto ya maji safi na salama

Kaburi la ajabu la Hayati Rais Laurent-Désiré Kabila wa DRC

Kaburi la ajabu la Hayati Rais Laurent-Désiré Kabila wa DRC

Miradi ya Rais Samia kupitia TASAF kunufaisha kaya zaidi ya 364 mkoani Njombe

Miradi ya Rais Samia kupitia TASAF kunufaisha kaya zaidi ya 364 mkoani Njombe

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:16
  • Today's page views 16
  • Total visitors 12,057
  • Total page views 13,710

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In