NA MFAUME PASTORY,NJOMBE
KAMPUNI ya ESAP Mining Services LTD inayojishughulisha na uuzaji wa baruti nchini kwa wachimbaji wa wadogo na wakubwa wameanzisha kiwanda cha kutengeneza vilipuzi ili kurahisisha uchimbaji wa madini.
Sekta ya Madini ambayo inatajwa kuwa mchango mkubwa kwa Taifa imeendelee kukua siku hadi huku makampuni ya wazawa yakipewa nafasi na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan
Kampuni hiyo ambayo ni ya wazawa inasaidia kulinda usalama wa makazi ya watu na mali zao tofauti na miaka ya nyuma ambapo bidhaa kama hizo zilikuwa zikitolewa nje ya nchi na wakati mwingine kuwafikia watu wenye nia mbaya kwa matumizi tofauti.
Hata hivyo uwepo wa Kampuni ya wazawa inayoweza kutengeneza bidhaa hizo utasaidia kuwatambua wahusika wote ambao wamepatiwa huduma hizo pindi yanapotokea majanga makubwa yanayohusishwa na binadamu.
Akizungumza na Bajeti Communication Aprili 27,2026 katika maonesho yaliyoandaliwa na Wakala wa Usalama wa Mahali na Afya Mahala pa Kazi (OSHA) yanayoendelea mkoani Njombe,Afisa Usalama Mahali pa Kazi wa ESAP Charles Chigabilo amesema shughuli yao kubwa ni uuzaji wa baruti kwa wachimbaji wadogo wadogo,kati na wakubwa ambao hujishughulisha na uchimbaji wa madini.
Amesema licha ya kujishughulisha na uuzaji huo wa baruti lakini pia wameanzisha kiwanda cha kutengeneza vilipuzi ikiwa la lengo la kuwarahisishia wachimaji wadogo wanapofika kwenye mwamba mgumu na kusaidia ulipuaji wake.

Chigabilo ameongeza kuwa hata wale waliona na viwanja vilivyopo katika mawe makubwa basi wao huweza kutumia utaalamu wao na nyenzo hizo kukiweka sawa na mhusika kuendelea na ujenzi wake kwa kuzingatia usalama wa mazingira ya watu na mali zao.
“Kwa sasa tunafanya kazi na Kampuni mbalimbali ikiwemo ule mradi wa Bomba la Mafuta Mkoa wa Singida na Manyara ,lakini pia tunaendelea kujitanua na maeneo mengine kwani tunachimba mashimo na kulipua”amesema Chigabilo
Chigabilo amebainisha kuwa hiyo ni Kampuni ya wazawa chini ya Mkurugenzi Mtendaji wake Mhandisi Yahaya Kiyaga ambapo wanafanya kazi katika Mkoa wa Mbeya,Singida,Manyara,Mara,Geita,Shinyanga,Kagera,Kigoma lakini pia wanasambaza bidhaa zao nje ya nchi kama Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo(DRC),na Burundi.
“Sisi pia tunazingatia sana usalama mahala pa kazi kwa wafanyakazi wetu na wengine kwani kabla ya kuanza utekelezaji,tunatoa mafunzo ili wafanyakazi wetu watambue vihatarishi na namna gani wanazuia vihatarishi hivyo ikiwemo kuvaa vifaa maalum vya kuzuia vumbi,kelele na kuumia kwa kudondokewa na vitu kichwani.
“Mafunzo na vifaa bora tunavyotoa kwa wafanyakazi wetu vinawafanya waendelee kuwa na afya zao za kila siku na sio kwamba akitoka kazini na kurejea nyumbani awe katika hali yake ya kawaida na sio kulalamika kuwa amechoka”ameeleza Chibagilo


Discussion about this post