• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Monday, May 25, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Mazingira

Kilometa 92,770 za ardhi Mradi wa Dege Eco Village Kigamboni zavamiwa,

Wavamizi watakiwa kulipia gharama.

by bajeti
May 25, 2026
in Mazingira
0
Kilometa 92,770 za ardhi Mradi wa Dege Eco Village Kigamboni zavamiwa,
Share on FacebookShare on Twitter

NA GOODLUCK  HONGO

MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Charles Kichere amebainisha kuwa katika mradi wa Dege Eco Village ardhi yenye ukubwa wa kilometa za mraba 92,770.39 ilikuwa imevamiwa kinyume cha sheria ikiwa na thamani ya Sh. Bilioni 1.41.

Dege Eco Village ni mradi uliotekelezwa kupitia mkataba wa ubia kati ya Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii kwa Sekta Binafsi na Kampuni ya Nyumba ya Azimio.

Mkataba huu uliositishwa Machi 2016 kufuatia masuala ya udhibiti yaliyotolewa na Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii na Benki Kuu ya Tanzania.

CAG Kichere ameyasema hayo katika Ripoti Kuu ya Mwaka ya Ukaguzi wa Mashirika ya Umma wa Mwaka wa Fedha 2024/2025 iliyotolewa tarahe30/3/2026.

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Charles Kichere

Aidha, amebaini kuwa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii kwa Sekta Binafsi, kupitia Mthamini wa Serikali, umebaini thamani ya ardhi iliyovamiwa kuwa ni dola za Marekani 547,044.50 (sawa na shilingi bilioni 1.41).

Amesema udhaifu huo ulisababishwa zaidi na usimamizi duni na ufuatiliaji usioridhisha wa sehemu hiyo ya ardhi ambapo Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii kwa Sekta Binafsi ulieleza kuwa unashirikiana na Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni kurejesha mpaka wa sehemu ya ardhi iliyovamiwa.

“Majadiliano pia yanaendelea kwa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii kwa Sekta Binafsi kukutana na viongozi wa serikali za mitaa, huku ajenda ikiwa sehemu ya ardhi iliyovamiwa.

“Kwa maoni yangu, ikiwa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii kwa Sekta Binafsi haitatumia haki yake ya umiliki wa ardhi hiyo, kuna uwezekano mkubwa wa kupoteza sehemu ya ardhi iliyovamiwa, ambayo hatimaye itasababisha hasara kwa Mfuko.

 “Ninapendekeza kuwa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii kwa Sekta Binafsi uharakishe mchakato wa uwekaji mipaka halisi ya ardhi iliyovamiwa na kuirejesha ardhi yote iliyovamiwa kwa gharama ya wavamizi”ameeleza CAG Kichere

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:26
  • Today's page views 30
  • Total visitors 16,480
  • Total page views 18,695

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In