NA MFAUME PASTORY,NJOMBE
HALMASHAURI ya Mji Njombe na Makambako mkoani Njombe zimetajwa kuwa halmashauri zilizofanikiwa kukopa na kurejesha mkopo wote wa fedha iilizopatiwa kwa ajili ya Utekelezaji wa Miradi ya Kupanga, Kupima na Kumilikisha Ardhi (KKK) Mwaka 2021/22.
Taarifa hiyo imeelezwa na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Leonard Akwilapo Mei 28,2026 katika hotuba yake bungeni Jijini Dodoma alipokuwa akiwasilisha Makadirio na Mapato na Matumizi ya Wizara kwa Mwaka wa Fedha 2026/2027.

Dkt.Akwilapo ameeleza kuwa Halmashauri ya Mji Njombe ilikopeshwa kiasi cha Sh. Milioni 700 na imefanikiwa kurejesha kiasi chote cha fedha wakati Halmashauri ya Mji Makambako ilikopeshwa kiasi cha Sh. Milioni 683.3 na imefanikikiwa kurejesha kiasi chote cha mkopo huo.

Katika kuwezesha utekelezaji wa vipaumbele na Mpango wa Bajeti wa Wizara kwa mwaka 2026/27, Waziri Dkt Akwilapo ameliomba Bunge kuidhinisha bajeti ya jumla ya Shilingi Bilioni 210.2 kwa ajili ya matumizi ya mafungu yote mawili (Fungu 48 – Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi) na (Fungu 03 – Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi).

Kwa upande wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa imetajwa kuwa miongoni mwa Halmashauri ambazo zimerejesha sehemu ya fedha katika deni la kiasi cha Sh. Milioni 405.0 fedha iliyokopeshwa kwa ajili ya Utekelezaji wa Miradi ya Kupanga, Kupima na Kumilikisha Ardhi (KKK) Mwaka 2021/22.

Kwa mujibu wa Waziri Akwilapo katika hotuba yake bungeni ameeleza kuwa Halmashauri ya Ludewa ilikopeshwa kiasi cha Sh. Milioni 405.0 na imefanikiwa kurejesha kiasi cha Sh.Milioni 147.64 na kiasi ambacho bado inadaiwa ni Sh.Milioni 257.35 sawa na asilimia 36
“Wizara imeendelea kuziwezesha halmashauri ili kuongeza kasi ya kupanga, kupima na kumilikisha ardhi kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Ardhi (Plot Development Revolving Fund – PDRF) ambao moja ya vyanzo vyake ni marejesho ya fedha shilingi bilioni 50.00 zilizokopeshwa mwaka 2021/22 kwenye halmashauri 57, Vyuo vya Ardhi vya Tabora na Morogoro, Chuo Kikuu Ardhi na Ofisi ya Ardhi Mkoa wa Iringa.
“Hadi tarehe 15 Mei 2026, Shilingi bilioni 33.18 zimerejeshwa sawa na asilimia 66.41 ya fedha zilizokopeshwa. Wizara inaendelea kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu- TAMISEMI na Wizara ya Fedha kuchukua hatua madhubuti kwa halmashauri zote ambazo hazijakamilisha kurejesha fedha hizo.
Nitumie fursa hii kuzipongeza halmashauri ambazo zimekamilisha marejesho ya fedha zilizokopeshwa na kuzitaka halmashauri ambazo hazijakamilisha kurejesha mikopo hiyo zifanye hivyo mara moja ili kuziwezesha halmashauri nyingine nchini kunufaika na fursa hiyo.”amesema Dkt.Akwilapo
Kwa mujibu wa hotuba ya Waziri Dkt.Akwilapo ni kuwa jumla Halmahauri zilizorejesha kiasi chote cha fedha ni pamoja na Moshi DC,Jiji la Mwanza, Meru,Morogoro,Kilosa, Geita,Halmashauri ya Mji Bariadi, Mbozi, Ilemela,Ileje,Halmashauri ya Mji Tunduma, Songwe,Kaliua, Ofisi ya Ardhi Mkoa wa Iringa,Kigamboni,Halmashauri ya Mji Kibaha,Sumbawanga,Mbulu,Halmashauri ya Jiji la Tanga,Hanang’,Rhombo ,Halmashauri ya Mji Njombe,Ushetu,Halmshauri ya Mji Makambako,Halmashauri ya Jiji la Dodoma ,Kikuu Ardhi naHalmashauri ya Jiji la Mbeya.
Halmashauri zilizorejesha Sehemu ya Fedha ilizokopeshwa ni pamoja na Halmashauri ya Mji Bunda,Halmashauri ya Mbeya, Buchosa,Uyui,Mtwara,Babati,Musoma,Chalinze,Halmashauri ya Mji Mbinga,Butiama,Meatu,Tabora,Halmshauri ya Mji Babati,Musoma,Halmshauri ya Mji Tarime,Morogoro, Ludewa, Ikungi,Kishapu,Msalala,Roryam,Shinyanga,Maswa,Lushoto,Lindi,Chamwino,Halmashauri ya Mji Mbulu ,Shinyanga,Manyoni,Halmashauri ya Mji Korogwe na Halmshauri ya Korogwe .


Discussion about this post