• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Tuesday, June 2, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Habari

Mashine Kiwanda cha Urafiki zaikosesha NHC mapato ya Sh.Bilioni 3.36

by bajeti
June 2, 2026
in Habari
0
NHC kubadili eneo la Urafiki kuwa kitovu cha maendeleo ya kiuchumi

Ofisi za kilichokuwa Kiwanda cha Urafiki mkoani Dar es Salaam

Share on FacebookShare on Twitter

NA GOODLUCK HONGO

MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Charles Kichere amesema ucheleweshaji wa kuhamisha mashine na vifaa vya Kiwanda cha Urafiki kilichopo mkoani Dar es Salaam yamesababisha Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) upotevu wa mapato ya Sh.Bilioni 3.36 kwa mwaka wa fedha 2024/25.

Amesema  mnamo tarehe 03 Novemba 2023, Shirika la Nyumba la Taifa lilishiriki na kushinda mnada wa kununua mali zilizokuwa zinamilikiwa na Kiwanda cha Urafiki (Lot 1, Kitalu Na. 409, Kiwanja Na. 1 pamoja na viwanja mbalimbali vya nyumba za wafanyakazi) kwa bei ya Sh.Bilioni 3.60 katika mnada ulioendeshwa kwa amri ya mahakama kupitia Kampuni ya Santana iliyoteuliwa na mahakama.

Meneja wa NHC Urafiki, Jackson Maagi (wa pili kutoka kulia) akimpa taarifa ya maendeleo ya utekelezaji ya eneo la Urafiki Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Hamad Abdallah (wa tatu kutoka kulia) wakati alipotembelea eneo la hilo

CAG Kichere ameyabainisha hayo katika Ripoti Kuu ya Mwaka ya Ukaguzi wa Mashirika ya Umma kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025 iliyotolewa tarehe 30/3/2026 .

“Mapitio yangu ya uwekezaji wa Shirika la Nyumba la Taifa katika eneo la Urafiki kwa mwaka ulioishia tarehe 30 Juni 2025, ambayo yalijumuisha ziara yangu katika eneo la uwekezaji uliofanyika tarehe 14 Novemba 2025, yalibaini kuwa mojawapo ya mali zilizonunuliwa na Shirika ni jengo ambalo kwa sasa linahifadhi mashine za Kiwanda cha Urafiki ambazo hazikua sehemu ya mali zilizonunuliwa na zinatakiwa kuondolewa na wamiliki wa Kiwanda cha Urafiki.

“Jengo hili lenye mita za mraba 35,019.69 linaweza kukodishwa kwa bei ya soko ya Sh. 8,000 kwa mita ya mraba, hivyo kuzalishia Shirika mapato ya Sh.Milioni 280.15 yatokanayo na kodi kwa mwezi.

 “Ucheleweshaji wa kuhamisha mashine na vifaa vya Kiwanda cha Urafiki yamesababisha Shirika la Nyumba la Taifa kushindwa kukodisha eneo hilo; hivyo kusababisha upotevu wa mapato ya Sh.Bilioni 3.36 kwa mwaka wa fedha 2024/25″amesema CAG Kichere.

Majengo ya kilichokuwa Kiwanda cha Urafiki mkoani Dar es Salaam

Hata hivyo CAG Kichere amependekeza kuwa Shirika la Nyumba la Taifa lifuatilie kwa ukaribu pande zinazohusika kukamilisha mazungumzo ili kuharakisha uhamisho wa mashine na vifaa vya kiwanda cha Urafiki.

Aidha ameongeza kuwa hiyo itawezesha kukodishwa kwa maeneo ambayo kwa sasa yapo chini ya kizuizi na kuliongezea Shirika mapato.

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:35
  • Today's page views 45
  • Total visitors 16,749
  • Total page views 19,018

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In