• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Friday, July 10, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Habari

Rais Samia anavyoiheshimisha NHC,yaendelea kutimiza maono ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere

Yakamilisha majengo nane ya Wizara mbalimbali Mji wa Serikali Mtumba

by bajeti
July 4, 2026
in Habari
0
Rais Samia anavyoiheshimisha NHC,yaendelea kutimiza maono ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere

Mradi wa Kawe 711 ukiwa katika hatua za mwisho za kukamilika kwake ikiwa na nyumba zaidi ya 700 ambazo zote zimeshauzwa

Share on FacebookShare on Twitter

 

 

Mradi wa Kawe 711 wa NHC ukiwa katika hatua za mwisho kukamilika

NA GOODLUCK HONGO

SHIRIKA  la Nyumba la Taifa (NHC) limekuwa chachu ya mageuzi makubwa katika Sekta ya Nyumba nchini Tanzania, likitimiza jukumu lake la kipekee la kuhakikisha Watanzania wanapata makazi bora.

Tangu kuanzishwa kwake mwaka 1962 kwa Sheria ya Bunge Na. 45, Shirika limeendelea kusimamia maono ya waasisi wa Taifa, likiongozwa na Dira ya Maendeleo Endelevu ya makazi.

Shirika hili liliundwa kama sehemu ya maono ya Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Nyerere ya kuhakikisha mahitaji ya msingi ya mwanadamu yanapatikana kwa urahisi.

Katika miaka ya mwanzo, NHC lilitekeleza miradi mbalimbali ya ujenzi wa nyumba za makazi na majengo ya umma, lakini changamoto za kiuchumi na kisheria zilianza kuathiri utendaji wake.

Mageuzi ya kihistoria yalifanyika katika miaka ya 1990 hadi 2008, ambapo sheria zisizokuwa rafiki katika Maendeleo ya Sekta ya Nyumba zilibadilishwa, na NHC likapewa Mamlaka mpya ya kujiendesha kibiashara bila kusahau jukumu lake la msingi.

Hatua hizi ziliweka msingi wa kuboresha huduma za makazi kwa Watanzania, lakini ni katika kipindi cha uongozi wa Rais Dkt. Samia ambapo kasi ya utekelezaji wa miradi ya nyumba imeongezeka kwa kiwango cha kipekee.

Mwaka 2015, NHC lilianzisha Mpango Mkakati wa Miaka 10 (2015/16 – 2024/25), uliolenga kujenga nyumba 10,000 na kuimarisha ushirikiano kati ya sekta ya umma na binafsi. Lakini ni katika kipindi cha Uongozi wa Rais Dkt. Samia ambapo utekelezaji wa mpango huu umechukua sura mpya, ikiwemo uanzishaji wa miradi mikubwa kama “Samia Housing Scheme” ambayo zinaendelea na ujenzi wa nyumba 5,000 katika maeneo mbalimbali nchini.

Mhandisi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Mkoa wa Dodoma Omary Chitawala akiwaonesha waandishi wa habari (hawapo pichani) Jengo la Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo ambalo analisimamia wanalojenga katika Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma Desemba 12,2024. ambalo sasa limeshakamilika

NHC ina pia jukumu la kujenga nyumba za makazi na majengo mengine kwa ajili ya kuuza na kupangisha.

Mbali na hilo lakini pia NHC ina jukumu la kujenga majengo kulingana na mipango iliyoidhinishwa na Serikali; kuzalisha na kuwezesha uzalishaji wa vifaa vya ujenzi.

Hata hivyo NHC ina jukumu la kusimamia milki za majengo; kufanya ukarabati wa nyumba; kukusanya kodi ya pango la nyumba za Shirika; kutoa huduma ya ushauri elekezi; upangaji wa maeneo ya ujenzi wa nyumba; na kutekeleza kazi za ukandarasi wa majengo.

Majukumu hayo yanatekelezwa kwa kuzingatia Mpango Mkakati wa Shirika wa miaka 11 (2015/16 – 2025/26).

Hata hivyo NHC imeendelea kuwa mfano wa Shirika bora la Umma lenye kuleta matokea yanayoonekana mbele ya macho ya watanzania kwa ujenzi wa majengo bora yenye kupendezesha mandhari ya majiji na miji mbali mbali nchini.

Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kipindi chake ameruhusu fedha kwenda  NHC ili  ikamilisha miradi mbalimbali ambayo awali ilisimama na kuanzisha mingine mipya ili kukabiliana na uhaba wa nyumba.

Nyumba za Shirika la Nyumba la Taifa (NHC ) zikiwa katika hatua za mwisho kukamilika katika Mradi wa Samia Housing Scheme zilizopo Kawe Manispaaa ya Kinondoni mkoani Dar es Salaam ambazo kwa sasa zimeshakamilika na watu wameshahamia 

Akizungumzia NHC bungeni jijini Dodoma, Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Leonard Akwilapo anasema NHC limeendelea kutekeleza mradi wa ujenzi wa nyumba 5,000 wa Samia Housing Scheme unaotarajiwa kugharimu jumla ya Sh.Bilioni 466.

Anasema katika mwaka 2025/26, Shirika lilipanga kuendelea na awamu ya pili ya utekelezaji wa Mradi wa Samia Housing Scheme kwa kujenga nyumba 908 katika maeneo mbalimbali nchini.

Dkt.Akwilapo ameyasema hayo  Mei 28,2026 wakati akitoa hotuba yake bungeni Jijini Dodoma alipokuwa akiwasilisha Makadirio na Mapato na Matumizi ya Wizara kwa Mwaka wa Fedha 2026/2027.

“Napenda kuliarifu Bunge lako Tukufu kuwa hadi tarehe 15 Mei 2026, ujenzi wa nyumba 68 za makazi eneo la Iyumbu (Dodoma) umekamilika hivyo kufanya jumla ya nyumba zilizokamilika kufikia 628.

“Aidha, ujenzi wa nyumba 260 katika eneo la Mtoni Kijichi umefikia asilimia 30, ujenzi wa nyumba 160 eneo la Medeli (Dodoma) umefikia asilimia 25 na nyumba 100 Iyumbu awamu ya pili imefikia asilimia tano.

“Kadhalika, maandalizi ya ujenzi wa nyumba katika maeneo ya Njedengwa (Dodoma), Kawe na 105 Boulevard Residence (Dar es Salaam) yanaendelea”anasema Dkt.Akwilapo

Jengo la Wizara ya Madini lililopo katika Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma lililojengwa na Mkandarasi Shirika la Nyumba la Taifa (NHC)

MIRADI ILIYOSIMAMA

Akizungumzia miradi iliyosimama,Dkt.Akwilapo anasema katika mwaka 2025/26, Wizara kupitia Shirika la Nyumba la Taifa ilipanga kukamilisha ujenzi wa miradi iliyokuwa imesimama katika Mkoa wa Dar es Salaam ikiwemo nyumba 422 katika Mradi wa Kawe 711 wenye thamani ya shilingi bilioni 169.

“Napenda kuliarifu Bunge lako Tukufu kuwa, ujenzi wa mradi huu umefikia asilimia 85 ya utekelezaji na unatarajiwa kukamilika ifikapo tarehe 30 Juni 2026.

“ Aidha, ujenzi wa nyumba 196 katika Mradi wa Golden Premier Residence (GPR) wenye thamani ya shilingi bilioni 127 umefikia asilimia 50 na unatarajiwa kukamilika mwaka 2027.

“Vilevile, ujenzi wa mradi wa Kiwanja Na. 300 Regent Estate upo katika hatua ya zabuni”anaongeza Dkt.Akwilapo

Anaeleza kuwa katika mwaka 2025/26, Wizara kupitia Shirika la Nyumba la Taifa ilipanga kuendelea na usimamizi wa ujenzi wa miradi 21 ya ubia yenye thamani ya Sh.Bilioni 351 na kukaribisha wawekezaji wengine kutoka sekta binafsi ili kufanya uendelezaji wa majengo ya biashara na makazi kupitia Sera ya Ubia.

 “Napenda kuliarifu Bunge lako Tukufu kuwa usimamizi wa miradi hii unaendelea ambapo miradi mitatu imekamilika na miradi mingine iliyobaki imefikia wastani wa asilimia 56 ya utekelezaji na inatarajiwa kukamilika mwaka 2027.

“Aidha, maombi mapya ya miradi  yenye thamani ya shilingi bilioni 607 yapo katika hatua mbalimbali ambapo miradi 38 inatarajiwa kuanza mwezi Juni 2026 na miradi 30 ipo katika hatua mbalimbali za uchambuzi”anabainisha Dkt.Akwilapo

Nyumba za Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) mkoani Lindi baada ya kufanyiwa ukarabati

MIRADI YA UBIA

Akizungumzia kuhusu miradi ya ubia,Dkt.Akwilapo anaongeza kuwa katika mwaka 2025/26, Wizara kupitia Shirika la Nyumba la Taifa ilipanga kuendelea na usimamizi wa ujenzi wa miradi 21 ya ubia yenye thamani ya shilingi bilioni 351 na kukaribisha wawekezaji wengine kutoka sekta binafsi ili kufanya uendelezaji wa majengo ya biashara na makazi kupitia Sera ya Ubia.

“Napenda kuliarifu Bunge lako Tukufu kuwa usimamizi wa miradi hii unaendelea ambapo miradi mitatu imekamilika na miradi mingine iliyobaki imefikia wastani wa asilimia 56 ya utekelezaji na inatarajiwa kukamilika mwaka 2027.

“Aidha, maombi mapya ya miradi yenye thamani ya shilingi bilioni 607 yapo katika hatua mbalimbali ambapo miradi 38 inatarajiwa kuanza mwezi Juni 2026 na miradi 30 ipo katika hatua mbalimbali za uchambuzi.”anasema Dkt.Akwilapo

Aidha anafafanuwa kuwa katika mwaka 2025/26, Wizara kupitia Shirika la Nyumba la Taifa ilipanga kuendelea na utwaaji wa miradi ya ubia iliyosimama kwa muda mrefu ili iweze kutekelezwa na Shirika lenyewe kwa mujibu wa mikataba.

“Napenda kuliarifu Bunge lako Tukufu kuwa kati ya miradi ya ubia 24 iliyokuwa imesimama, miradi 13 imekamilika na miradi minne (4) inaendelea kusimamiwa na Shirika ili wabia waikamilishe, miradi mitatu (3) imetwaliwa na utekelezaji wake utaendelea kuanzia Julai, 2026.

“Vilevile, miradi mingine minne  inatarajiwa kutwaliwa ifikapo Juni 2026 katika mikoa ya Mwanza miwili, Dar es Salaam mmoja na Iringa mmoja”anabainisha Dkt.Akwilapo

Dkt Akwilapo anaongeza kuwa katika mwaka 2025/26, Wizara kupitia Shirika lilipanga kuendelea na ujenzi wa miradi ya majengo ya biashara katika mikoa mbalimbali nchini ikiwamo Meru View shops (Arusha), Tabora Commercial Complex (Tabora), Singida 2F Plaza (Singida), Mkwakwani Commercial Complex (Tanga), Kashozi Commercial Complex (Kagera), Uluguru Plaza (Morogoro), Iringa Commecial Complex (Iringa) na Uhuru shopping centre- Ilala (Dar es Salaam).

“Napenda kuliarifu Bunge lako Tukufu kuwa, ujenzi wa mradi wa Meru View Shops (Arusha) umefikia asilimia 52; Tabora Commercial Complex (Tabora) umefikia asilimia 46; Singida 2F Plaza (Singida) umefikia asilimia 85;

“Mkwakwani Commercial Complex (Tanga) umefikia asilimia 40; Kashozi Commercial Complex (Kagera) umefikia asilimia 65; Uluguru Plaza (Morogoro) umefikia asilimia 42; na Iringa Commercial Complex (Iringa) umefikia asilimia 40”anaeleza Dkt.Akwilapo

Afisa Miliki wa Shirika la Nyumba la Taifa(NHC) Mkoa wa Dodoma Pauline Kamaghe akiwaonesha waandishi wa habari kutoka Bajeti Communication (hawapo pichani) nyumba za Shirika hilo zilizokarabatiwa katika eneo la Iringa road Desemba 12,2024 jijini Dodoma

WADAIWA WATAKIWA KULIPA MADENI

Akizungumzia kuhusu madeni,Dkt.Akwilapo anabainisha kuwa katika mwaka 2025/26, Wizara kupitia Shirika la Nyumba la Taifa ilipanga kuanza ujenzi wa miradi mipya 79 katika miji na halmashauri mbalimbali ikiwemo jengo la matumizi mchanganyiko mkoani Ruvuma, majengo ya biashara na ofisi – Masasi, Lindi, Usa River na Ngarenaro.

“Napenda kuliarifu Bunge lako Tukufu kuwa ujenzi wa jengo la matumizi mchanganyiko mkoani Ruvuma uko katika hatua ya ujenzi wa msingi, miradi ya Usa River na Ngarenaro maandalizi ya ujenzi yako hatua za mwisho”anaeleza Dkt.Akwilapo

Nyumba za Shirika la Nyumba la Taifa (NHC)zilizojengwa kupitia mradi wa Iyumbu Nyumba 1000 katika eneo la Iyumbu jijini Dodoma ambazo tayari zimeshauzwa

Aidha ameongeza kuwa Shirika limekamilisha ujenzi wa majengo ya biashara na ofisi ya Mtanda (Lindi), Zongomela (Kahama) na Masasi Commercial Complex (Masasi- Mtwara). Vilevile, ujenzi wa maghala tisa kwa ajili ya kupangisha katika Manispaa ya Mtwara umeanza ambapo awamu ya kwanza ya ujenzi wa maghala matatu unaendelea na umefikia asilimia 78.

Dkt Akwilapo anasema katika mwaka 2025/26, Wizara kupitia Shirika la Nyumba la Taifa ilipanga kuendelea na kuanza upembuzi yakinifu wa ujenzi wa miradi ya vitovu vya miji vikiwemo Mwashiwawala (Songwe), Kwala (Pwani), Urafiki na Salama Creek (Dar es Salaam) ifikapo Juni, 2026.

“Nalitaarifu Bunge lako Tukufu kuwa, upembuzi yakinifu katika miradi ya Mwashiwawala na Usa River, Salama Creek umekamilika.

“ Aidha, upembuzi yakinifu katika eneo la Kwala na Urafiki unaendelea na utakamilika mwezi Juni, 2026.. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2025/26 Wizara kupitia Shirika la Nyumba la Taifa ilipanga kuendelea kukusanya madeni ya kodi ya nyumba, miradi ya ukandarasi, uuzaji wa nyumba, viwanja na madeni mengineyo.

 “Napenda kuliarifu Bunge lako Tukufu kuwa hadi tarehe 15 Mei 2026, Shirika limepunguza madeni hayo kutoka shilingi bilioni 27.98 mwaka 2024/25 hadi shilingi bilioni 19 mwaka 2025/26,nitumie fursa hii kuwataka wadaiwa wote kutekeleza wajibu wao wa kulipa madeni yao kabla Shirika halijachukua hatua kali za kisheria.”anasema Dkt Akwilapo

UKARABATI WA NYUMBA NA KUKABIDHI MAJENGO YA WIZARA NANE

Nyumba za NHC eneo la Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam zikiwa katika muonekano wa kupendendeza baada ya kufanyiwa ukarabati

Akizungumzia ukarabati wa nyumba na kukamilika kwa majengo ya Wizara nane iliyojengwa na NHC kama Mkandarasi Daraja A ,Dkt.Akwilapo anasema katika mwaka 2025/26, Wizara kupitia Shirika la Nyumba la Taifa ilipanga kukarabati nyumba za Shirika 1,600 ambapo hadi tarehe 15 Mei 2026, Shirika lilikuwa limekarabati nyumba 1,283 sawa na asilimia 80 ya lengo ambapo ukarabati wa nyumba 317 uko katika hatua za mwisho za utekelezaji.

“Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2025/26, Wizara kupitia Shirika la Nyumba la Taifa ilipanga kuendelea na ujenzi wa miradi ya ukandarasi na ushauri elekezi,napenda kuliarifu Bunge lako Tukufu kuwa ujenzi wa majengo nane  ya Ofisi za Serikali katika Mji wa Serikali Mtumba umekamilika na kukabidhiwa kwa washitiri.

“Aidha, usanifu na ujenzi wa jengo la soko la madini (Tanzanite) eneo la Mirerani Manyara umekamilika. Vilevile, ujenzi wa miradi ya ukandarasi na utaalamu elekezi wa majengo ya Ofisi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA) jijini Dodoma umefika asilimia 73 na Zanzibar umefikia asilimia 50.

“Kadhalika, Shirika limeanza kutoa ushauri elekezi katika miradi mipya ya ujenzi wa Makao Makuu ya Wakala wa Barabara Vijijini (TARURA) na Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) jijini Dodoma”anafafanuwa Dkt.Akwilapo

Nyumba za NHC Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam zikiwa zimefanyiwa ukarabati na kupakwa rangi

Hata hivyo Dkt.Akwilapo anabainisha kuwa  ili kuwezesha upatikanaji wa nyumba za gharama nafuu, Shirika linaendelea kukamilisha maandalizi ya ujenzi wa nyumba za gharama nafuu kwa awamu ambapo utekelezaji utaanza mwaka 2026/27 katika mradi wa Salama Creek (Kigamboni, Dar es Salaam), Sabasaba (Morogoro), Iyumbu (Dodoma) na Buswelu (Mwanza).

Jengo la Wizara ya Kilimo lililopo katika Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma lililojengwa na Mkandarasi Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) (Picha na Goodluck Hongo)

 KAZI ZITAKAZOTEKELEZWA NA NHC  MWAKA  2026/2027 

Akizungumzia kuhusu kazi zitakazotekelezwa na NHC katika mwaka 2026/ 27,Dkt.Akwilapo anafafanuwa kuwa Shirika hilo limejipanga  kuendelea na ujenzi wa nyumba katika Mradi wa nyumba 5,000 wa Samia Housing Scheme katika maeneo ya Mtoni  Kijichi na Kawe (Dar es Salaam) na Medeli na Iyumbu (Dodoma).

Aidha ameongeza kuwa  Shirika litaanza ujenzi wa nyumba katika maeneo ya Njedengwa (Dodoma), Urafiki (Dar es Salaam), Sokoine complex (Mtaa wa Azimio- Arusha) na Makongoro (Mwanza);

“Kuanza ujenzi wa nyumba 800 za gharama nafuu kwa awamu katika mradi wa Salama Creek (Kigamboni, Dar es Salaam), Sabasaba (Morogoro), Iyumbu (Dodoma) na Buswelu (Mwanza);

“Kuendelea na ujenzi wa nyumba 196 katika mradi wa Golden Premier Residence (GPR) na Kiwanja Na.300 Regent Estate;

“Kuendelea na usimamizi wa ujenzi wa miradi ya ubia na kukaribisha wawekezaji wengine kutoka sekta binafsi na zile za Umma ili kufanya uendelezaji wa majengo ya biashara na makazi kupitia Sera ya Ubia; Kuendelea kukamilisha ujenzi wa miradi ya majengo ya biashara katika mikoa mbalimbali nchini ikiwemo Meru view shops, Ngarenaro na Usa River (Arusha)”anasema Dkt.Akwilapo

Miradi mingine  ni katika mikoa ya Tabora Commercial Complex (Tabora), Mkwakwani Commercial Complex (Tanga), Uluguru Plaza (Morogoro), Iringa Commercial Complex (Iringa), Songea Commercial Complex (Ruvuma); Bukoba Complex (Kagera), 17A mwenge na 1K 83 Market Street (Singida), Uganda Avenues na RAS Kilomoni (Dar es Salaam).

Jengo la Hospitali ya Rufaa Kanda ya Kusini Mtwara ambalo limejengwa na Mkandarasi Shirika la Nyumba la Taifa (NHC)(Picha na Goodluck Hongo)

Mbali na hili lakini pia kuendelea na upembuzi yakinifu wa ujenzi wa miradi ya vitovu vya miji ikiwemo Kwala (Pwani) na Salama Creek (Dar es Salaam); na kuendelea kutekeleza mpango wa ukarabati wa nyumba za Shirika 2,200; na kutekeleza miradi ya ukandarasi na ushauri elekezi inayoendelea na mingine itakayojitokeza.

AJIRA

NHC imekuwa ikitoa maelfu ya ajira kwa mafundi,mama lishe,makampuni ya vifaa vya ujenzi hasa pale wanapotekeleza miradi ya ujenzi wa majengo katika mikoa mbalimbali nchini hali inayoinua kipato cha wananchi.

Gari la NHC jijini Dodoma

 

 

 

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:383
  • Today's page views 385
  • Total visitors 20,694
  • Total page views 23,068

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In