NA GOODLUCK HONGO
RAIA 14 kutoka mataifa ya kigeni wakiwemo Waingereza,Wachina na Mmarekani wamekamatwa nchini wakijihusisha na dawa za kulevya
Raia wengine waliokamatwa ni pamoja na raia kutoka Marekani na Sri lanka ambapo kwa pamoja wanajumuisha watuhumiwa ambao ni raia wa kigeni kufikia 14.
Kwa mujibu wa Taarifa ya Hali ya Dawa za Kulevya ya Mwaka 2025 iliyotolewa Mei,2025 na kuwekwa saini na Waziri wa Nchi ,Ofisi ya Waziri Mkuu(Sera,Bunge,Uratibu na Wenye Ulemavu) Prof.Palamagamba Kabudi pamoja na Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) kuwa raia wa kigeni 14 walikamatwa nchini kwa kujihusisha na dawa za kulevya.
“Mwaka 2025,raia wa kigeni 14 walikamatwa kwa tuhuma za kujihusisha na dawa za kulevya,kutoka nchi za China wawili,Lebanoni mmoja,Congo mmoja,Sri Lanka wawili,Uingereza wawili,Marekani mmoja,Naigeria mmoja,Ujerumani mmoja,Kenya mmoja,Msumbiji mmoja, na Uganda mmoja”imeeleza taarifa hiyo
Kwa upande wa watanzania waliokamatwa nje ya nchi kwa kujihusisha na dawa za kulevya,taarifa hiyo imefafanuwa kuwa takwimu za mwaka 2025 zinaonesha kuwa juma la watanzania 28 walikamatwa.
Taarifa hiyo imebainisha kuwa 20 kati yao walikamatwa nchini Zambia,wawili nchini Botwana,wawili nchini Msumbiji,Mauritania mmoja,Japan mmoja,Ufaransa mmoja na Shelisheli mmoja.
Hata hivyo idadi ya watanzania imeendelea kushuka katika kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya ambapo kwa mujibu wa Taarifa ya Hali ya Dawa za Kulevya ya Mwaka 2022 imeonesha kuwa watanzania waliokamatwa nje ya nchi kwa kujihusisha na dawa za kulevya walikuwa 147 ambapo wanaume walikuwa 136 na wanawake 11.

Discussion about this post