• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Saturday, October 10, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Habari

Spika Zungu:Tanzania kuchangia uzoefu huduma za mama na mtoto

by bajeti
October 9, 2026
in Habari
0
Spika Zungu:Tanzania kuchangia uzoefu huduma za mama na mtoto

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mussa Zungu akisalimiana na mmoja wa washiriki wa mkutano kuhusu masuala ya afya ya mama na mtoto Oktoba 8,2026 ulioandaliwa na Serikali ya Tanzania na wajumbe wa Mkutano wa 153 Umoja wa Mabunge Duniani unaoendelea jijini Arusha.Kulia ni Mshauri wa Rais anayeshughulikia masuala ya Afya, Ustawi wa Jamii, Wanawake na Watoto, Ummy Mwalimu.

Share on FacebookShare on Twitter

NA TBN, ARUSHA.

SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mussa Zungu amesema Tanzania ipo tayari kuchangia uzoefu wake katika kuimarisha upatikanaji wa huduma za mama na mtoto mchanga, afya ya uzazi, lishe na ustawi wa vijana.

Zungu ameeleza hayo Oktoba 8, 2026, wakati akitoa hotuba ya ufunguzi katika mdahalo kuhusu masuala ya afya ya mama na mtoto ulioandaliwa na Serikali ya Tanzania na wajumbe wa Mkutano wa 153 Umoja wa Mabunge Duniani.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mussa Zungu

Zungu amebainisha kuwa afya na ustawi wa wanawake, watoto na vijana ni msingi wa maendeleo ya Taifa na kwamba Tanzania inatarajia kuchangia uzoefu wake na kufanya kazi na washirika kugeuza dhamira ya kisiasa kuwa matokeo ya kudumu.

“Kila kifo kinachozuilika, kila hitaji la kiafya lisilotimizwa na kila kikwazo cha kupata huduma,kinahitaji umakini na hatua endelevu za kisiasa.

“Ndio maana Rais Samia Suluhu Hassan ameweka kipaumbele cha kupunguza vifo vya wajawazito, kupunguza vifo vya watoto na idadi ya watoto wasiochanjwa hadi sifuri, si tu nchini Tanzania bali pia kuchochea hatua hizi kote barani Afrika kupitia wadhifa wake kama Kinara wa Afya ya Mama na Mtoto barani Afrika,” ameongeza Zungu.

Aidha amebainisha kuwa Bunge lina jukumu la kuendeleza sheria, kuhakikisha fedha za kutosha  zinatengwa na kusimamia utekelezaji kuhakikisha rasilimali zinafika kwenye huduma za mstari wa mbele na kwa jamii.

“Kipaumbele chetu kiwe kwenye upatikanaji sawa wa huduma, ikiwemo huduma za mama na mtoto mchanga, afya ya uzazi, lishe, na afya na ustawi wa vijana.

“Kupitia Mtandao huu, tunaweza kujifunza kutoka kwa kila mmoja, kuimarisha uwajibikaji wa kibunge na kuendeleza hatua za vitendo katika nchi zetu”amebainisha Zungu

Washiriki wa mdahalo kuhusu masuala ya Afya ya Mama na Mtoto ulioandaliwa na Serikali ya Tanzania na wajumbe wa Mkutano wa 153 Umoja wa Mabunge Duniani,wakimsikiliza Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mussa Zungu hayupo (pichani) wakati akihutubia mkutano huo uliofanyika jijini Arusha Oktoba 8,2026.

Kwa upande wake Mshauri wa Rais anayeshughulikia masuala ya afya, ustawi wa jamii, wanawake na watoto, Ummy Mwalimu aliyemuwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, amefafanuwa kuwa Afrika imepiga hatua katika kupunguza vifo vya kina mama japo bado haijatosha.

“Vifo vya kina mama katika nchi wanachama wa Umoja wa Afrika vilipungua kwa asilimia 42 kati ya mwaka 2000 na 2023, lakini Afrika bado inachangia takribani asilimia 70 ya vifo vya kina mama duniani.

“Kwa kasi iliyopo sasa Afrika haitaweza kufikia lengo la Maendeleo Endelevu la kuwa na vifo vya kina mama 70 kwa kila vizazi hai 100,000 hadi karibu mwaka 2050,” amesema Mwalimu.

Washiriki wa mdahalo kuhusu masuala ya Afya ya Mama na Mtoto ulioandaliwa na Serikali ya Tanzania na wajumbe wa Mkutano wa 153 wa Umoja wa Mabunge Duniani,(IPU) wakimsikiliza Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mussa Zungu (hayupo pichani) wakati akihutubia mkutano huo uliofanyika jijini Arusha Oktoba 8,2026.

Mwenyekiti wa Kundi la Kijiografia la Afrika la IPU,  Ali Kolotou Tchaïmi amesema Wabunge wana wajibu wa kuhakikisha ahadi za afya zinawafikia wananchi wa kawaida.

Amesema watunga sheria wana jukumu la kutunga sheria, kuidhinisha bajeti na kusimamia serikali, hususan katika kulinda makundi yaliyo katika mazingira hatarishi.

Spika wa Bunge la Afrika Kusini, Angela Thokozile Didiza, ametoa wito wa kuimarishwa kwa uongozi wa kisiasa, akibainisha kuwa vifo vya kina mama na chanjo za watoto bado ni changamoto kubwa za afya ya umma.

Next Post
IPU:Dira ya Maendeleo 2050,Tanzania ina fursa kuimarisha ushiriki wa wanawake na vijana kutekeleza ajenda za maendeleo ya muda mrefu

IPU:Dira ya Maendeleo 2050,Tanzania ina fursa kuimarisha ushiriki wa wanawake na vijana kutekeleza ajenda za maendeleo ya muda mrefu

Spika Zungu akutana na Spika wa Bunge la Uingereza

Spika Zungu akutana na Spika wa Bunge la Uingereza

Dunia ilivyohamia Tanzania kupitia Umoja wa Mabunge Duniani (IPU)

Dunia ilivyohamia Tanzania kupitia Umoja wa Mabunge Duniani (IPU)

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:1
  • Today's page views 1
  • Total visitors 22,443
  • Total page views 25,011

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In