• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Thursday, October 15, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Habari

Makamu wa Rais Ndejembi:Tanzania kuuza umeme nchi za ukanda wa Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika.

Awataka wawekezaji kuchangamkia fursa za kiuchumi mkoani Rukwa

by bajeti
October 15, 2026
in Habari
0
Makamu wa Rais Ndejembi:Tanzania kuuza umeme nchi za ukanda wa Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Deogratius Ndejembi akihutubia (wananchi hawapo pichani) wakati wa Kilele cha Sherehe za kuhitimisha mbio za Mwenge wa Uhuru zilizofanyika Sumbawanga, mkoani Rukwa, tarehe 14 Oktoba 2026. Sherehe hizo zimekwenda sambamba na Kumbukizi ya Miaka 27 ya tangu kufariki kwa Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere

Share on FacebookShare on Twitter

SUMBAWANGA, RUKWA

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Deogratius Ndejembi amesema kukamilika kwa Mradi wa Kituo cha Kupoza na Kusambaza Umeme cha Malangali, mkoani Rukwa, kutafungua ukurasa mpya wa maendeleo ya kiuchumi kwa kuimarisha upatikanaji wa umeme wa uhakika, kuvutia wawekezaji na kuwezesha Tanzania kuuza umeme Mataifa Jirani.

Akizungumza Oktoba 15,2026 mkoani Rukwa wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho, Makamu wa Rais amesema Mkoa wa Rukwa wenye mahitaji ya takribani megawati 30, kwa sasa unapokea megawati 16 pekee, hali iliyokuwa ikikwamisha shughuli za uzalishaji, hususan uchakataji wa mazao ya kilimo na madini.

Amesema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imewekeza katika mradi huo ili kuhakikisha Rukwa inaunganishwa na Gridi ya Taifa na kuwa kitovu cha uzalishaji na biashara ya umeme katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika.

“Leo hii TANESCO inanunua umeme Zambia, lakini kwa laini hii sisi tutaanza kuiuzia Zambia umeme mkubwa na wa uhakika,” amesema Makamu wa Rais, huku akiwataka wawekezaji kuchangamkia fursa za kiuchumi mkoani Rukwa na wananchi kulinda miundombinu hiyo”amesema Makamu wa Rais Ndejembi

Awali, Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Salome Makamba, amesema mradi huo ni sehemu ya uwekezaji wa Serikali unaodhihirisha dhamira ya dhati ya kuhakikisha mikoa yote nchini inaunganishwa na Gridi ya Taifa.

Amesema asilimia 90 ya wafanyakazi wanaotekeleza mradi huo ni Watanzania, huku akieleza kuwa majaribio ya mitambo yanatarajiwa kuanza katikati ya Novemba 2026.

Hassan imewekeza katika mradi huo ili kuhakikisha Rukwa inaunganishwa na Gridi ya Taifa na kuwa kitovu cha uzalishaji na biashara ya umeme katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika.

Awali, Naibu Waziri wa Nishati, Salome Makamba, amesema mradi huo ni sehemu ya uwekezaji wa Serikali unaodhihirisha dhamira ya dhati ya kuhakikisha mikoa yote nchini inaunganishwa na Gridi ya Taifa.

Amesema asilimia 90 ya wafanyakazi wanaotekeleza mradi huo ni Watanzania, huku akieleza kuwa majaribio ya mitambo yanatarajiwa kuanza katikati ya Novemba 2026.

Awali akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa mradi huo, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme nchini (TANESCO), Lazaro Twange, amesema ujenzi wa kituo cha Malangali umefikia asilimia 85.17, huku kazi za kuwasha na kuingiza umeme zikipangwa kukamilika Novemba 2026.

Amesema kituo hicho kinachojengwa na kampuni ya TBEA kutoka China kwa gharama ya shilingi bilioni 161.9, kitakuwa na uwezo wa kupokea umeme wa kilovolti 400 na kuushusha katika misongo ya kilovolti 220, 66 na 33, kikijumuisha transfoma nne na njia nane za kusambaza umeme katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Rukwa.

Kukamilika kwa mradi huo kunatarajiwa kuondoa changamoto ya upungufu wa umeme, kuchochea ujenzi wa viwanda, kuongeza thamani ya mazao na kufungua fursa mpya za ajira na uwekezaji, huku Tanzania ikiimarisha nafasi yake katika biashara ya nishati kikanda.

 

 

 

 

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:40
  • Today's page views 42
  • Total visitors 22,546
  • Total page views 25,124

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In