NA MWANDISHI WETU
TAMASHA la Uimbaji linaloandaliwa na Kwaya ya Flying Family (FFC) na kuwatanisha watu wa aina mbalimbali wakiwemo,maaskofu, mabalozi na viongozi wa Serikali linatarajiwa kufanyika Desemba 6,2026 mkoani Dar es Salaam.

Tamasha hilo linalohusisha pia watu wazima na familia zao wakiwemo watoto,ni tamasha la tisa kufanyika nchini likijumuisha waimbaji kutoka madhehebu mbalimbali ya makanisa ya kikristo wenye vipaji vya uimbaji.
Mbali na hilo lakini pia tamasha hilo linakwenda sambamba na kusheherekea sikukuu ya Krismasi ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo zaidi ya miaka 1000 iliyopita ambayo huadhimishwa kila ifikapo Desemba 25 ya kila mwaka na kuwahusisha mamilioni ya wakristo duniani kote.

Akizungumzia tamasha hilo Novemba 19,2026 jijini Dar es Salaam,Mwenyekiti wa Kwaya ya Flying Family (FFC) ambayo ndio waandaji wa tamasha hilo Innocent Fundisha amesema FFC ni kwaya iliyoanzishwa mwaka 2018 ikijumuisha waimbaji kutoka makanisa mbalimbali ya kikristo ikiwa la lengo la kutengeneza umoja wa wakristo kupitia uimbaji.

Amesema tangu wakati huo walianza kufanya matamasha mbalimbali ambapo tamasha la kwanza walianza kulifanya mwaka 2018.
“Hili ni tamasha la 11 tangu tulipoanza kufanya tamasha hili na kwaya yetu inajumisha wanakwaya kutoka madhehebu mbalimbali ya kikristo ambao wanatokea katika maeneo ya Mkoa wa Dar es Salaam,mikoani na baadhi kutoka nje ya nchi ikiwemo Uganda.
“Mwanzo tulikuwa tukifanya mara moja kwa mwaka lakini sasa hivi tunafanya kwa mwaka mara mbili na tumeshafanya katika kumbi za Kardinal Rugambwa,Mlimani City,Mwalimu Nyerere Posta ambapo mwaka huu tutafanyia katika ukumbi wa Skywave hall Msasani Beach.
“Tamasha hili litafanyika Desemba 6,2026 katika ukumbi wa Skywell Msasani Beach kuanzia saa 11.00 jioni na tutakuwa na uimbaji mzuri sana wa classical music tukichanganya nyimbo nzuri za Krismasi,nyimbo ambazo zimeandikwa kwa umahiri mkubwa sana wakiwemo watunzi nguli kama kina George Handel,W.Morzat,J.S.Bach,Mendelssohn na wengine wengi“amesema Fundisha

Fundisha ameongeza kuwa hilo ni tamasha kubwa la watu waliojaa vipaji vingi vya mziki ambapo pamoja na muziki,kutakuwepo na chakula cha jioni pamoja na vinywaji.

“Tiketi za tamasha ni Sh.50,000 kwa watu wazima,30,000 kwa watoto na V.I.P itakuwa ni Sh.100,000 ambapo ndani ya bei hiyo kutakuwepo na chakula na vinywaji.
“Tunawaalika watu wote kuanzia watoto wadogo,familia na wengine kuja kusheherekea sikukuu ya Krismass kwani tamasha hili linajumisha watu wote ikiwemo viongozi wa kidini ,viongozi wa Serikali ,mabalozi pamoja na watu wa kada mbalimbali wanakaribishwa kufika na kufurahia kwa kuwa linalofanyika kulingana na utamaduni wa sikukuu ya Krismasi.
“Tamasha hilo pia litakuwa na watumbuizaji wa Saxophone na wengine hivyo tunawakaribisha sana ndugu zetu watanzania tuje tufurahie umoja wetu na kusheherekea Krismass kwa kushiriki na familia zetu”amebainisha Fundisha


Discussion about this post