• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Monday, May 4, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Habari

Dkt.Mpango:Waziri Mkuu Mstaafu Hayati Edward Lowassa alikuwa mwanamazingira

Awasihi watanzania kutumia msiba huo kudumisha na kuimarisha upendo, amani na mshikamano wa Taifa.

by bajeti
February 13, 2024
in Habari
0
Dkt.Mpango:Waziri Mkuu Mstaafu Hayati Edward Lowassa alikuwa mwanamazingira

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akitoa heshima za mwisho kwa Waziri Mkuu Mstaafu Hayati Edward Ngoyai Lowassa katika Viwanja vya Karimjee Jijini Dar es salaam Februari13, Februari 2024.(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Share on FacebookShare on Twitter

NA MWANDISHI WETU

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango amewaongoza viongozi na wananchi katika kutoa heshima za mwisho kwa Waziri Mkuu Mstaafu hayati Edward Ngoyai Lowassa katika viwanja vya Karimjee Jijini Dar es salaam.

Makamu wa Rais amesema  Lowassa alikuwa mwanamazingira hodari ambapo katika wadhifa wake wa  Waziri wa Nchi – Ofisi ya Makamu wa Rais na alipokuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alihimiza sana uhifadhi na Utunzaji wa mazingira na aliongoza kampeni nyingi za upandaji miti na usafi wa mazingira.

Akitoa salamu za pole kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan Februari 13,2024, Makamu wa Rais ametoa pole kwa familia, ndugu, marafiki pamoja na watanzania wote kwa ujumla kufuatia msiba huo mkubwa kwa Taifa.

Amesema mchango wake huo uwakumbushe watanzania wote wajibu wa msingi wa kulinda na kutunza mazingira na hususan vyanzo vya maji ili kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi ambazo zinaendelea kuleta madhara mengi katika Taifa na dunia kwa ujumla.

”Serikali inathamini uzalendo na mchango mkubwa aliyoutoa Hayati Edward Lowassa katika maendeleo ya nchi kwa kuwa alijitolea kwa dhati kulitumikia Taifa pamoja na kutumia vema karama alizojaliwa na Mwenyezi Mungu kuwatumikia Watanzania katika nyadhifa mbalimbali alizowahi kushika.

”Ni muhimu kila mmoja mtanzania kujikumbusha wajibu aliyonao kwa taifa na kuyaishi kwa vitendo mambo yote mazuri yanayotokana na maisha ya hayati Lowassa.

”Ni vema Watanzania kumuenzi hayati Lowassa kwa kuendelea kuchapa kazi ili kuboresha maisha na hivyo kuchangia katika ujenzi wa Taifa kwa kuwa alikuwa mchapa kazi hodari katika utumishi wa umma na katika shughuli zake binafsi ikiwemo ufugaji”ameongeza Dkt.Mpango

Viongozi wastaafu wa serikali wakimsiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango (hayupo pichani) wakati wa akitoa salamu za pole kwa familia, viongozi na wananchi kwa ujumla wakati wa kuaga mwili wa Waziri Mkuu Mstaafu Hayati Edward Ngoyai Lowassa katika Viwanja vya Karimjee Jijini Dar es salaam Februari 13, 2024.(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Aidha Makamu wa Rais ametoa wito kwa watanzania wote na hususan vijana kumuenzi  hayati Lowassa kwa kutumia fursa mbalimbali kujipatia elimu kwa manufaa ya Taifa kwa kuwa alikua kinara katika elimu na kusimamia kwa uhodari  utekelezaji wa sera, mikakati na mipango mbalimbali ya elimu hususan ujenzi wa shule za Sekondari kila Kata..

Makamu wa Rais amewasihi watanzania kutumia msiba huo kudumisha na kuimarisha upendo, amani na mshikamano wa Taifa.

 

Next Post
Utunzaji wa mazingira Mkinga-Tanga

Utunzaji wa mazingira Mkinga-Tanga

Jeshi la Polisi Songwe

Jeshi la Polisi Songwe

Rais Vladimir Putin wa Urusi ‘si binadamu wa kawaida’

Rais Vladimir Putin wa Urusi 'si binadamu wa kawaida'

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:1
  • Today's page views 1
  • Total visitors 16,050
  • Total page views 18,209

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In