MOSCOW-Urusi
RAIS wa Urusi Vladimir Putin Alhamisi aliishangaza dunia baada ya kupaa angani akiwa kama rubani msaidizi wa ndege ya kijeshi ya kubebea mabomu ya nyuklia.
Ndege hiyo ya kimkakati ya nyuklia aina ya TU-160M iliruka kutoka eneo la Kazan nchini humo kwa muda wa dakika 30 baada ya kufanyiwa maboresho makubwa ya kimkakati.
Rais Putin anaweza kuwa ndiye rais pekee duniani kutoka moja ya mataifa makubwa yenye kumiliki silaha za nyuklia kuruka na ndege za kijeshi akiwa kama rubani msaidizi bila kuogopa huku nchi yake ikiwa vitani na Ukraine.
Hata hivyo safari ya ndege ya Putin ya dakika 30 pia ilionekana kutuma ujumbe kwa nchi za Magharibi wakiongozwa na Marekani kuwa nchi hiyo bado ina nguvu kubwa za kijeshi na haiogopi vikwazo ilivyowekewa wala haitaisitisha oparesheni zake za kijeshi.
Kuruka kwa ndege hiyo pia kunaashiria kuwa vita vya nchi hiyo na jirani yake Ukraine vinavyoingia mwaka wa tatu vinaweza kusababisha matumizi ya nyuklia ikiwa misaada wanayopewa Ukraine itafanikisha kuishinda Urusi
Putin, 71, ambaye jeshi lake limepata mafanikio makubwa katika vita vyake nchini Ukraine hivi karibuni baada ya kuliteka jiji la Adviika lililokuwa ngome kuu ya Jeshi la Ukraine.
Nchi za Magharibi ambazo zimetuma maelfu ya tani za makombora,mabomu,vifaru,risasi,magari na misaada mingine ili kulisaidia Jeshi la Ukraine kujilinda dhidi ya Urusi lakini misaada hiyo haijasaidia katika kulifanya Jeshi la Ukraine kurudisha maeneo yaliyotekwa na Urusi.
Siku ya Alhamisi, vyombo vya habari vya Urusi vilimuonesha Rais Putin, akiwa amevalia mavazi ya rubani, alipanda ndege ya kivita katika uwanja wa ndege uliofunikwa na theluji wa kiwanda cha kutengeneza ndege katika mji wa Mto Volga wa Kazan.
Kiwanda hicho kilipokea maagizo ya serikali kutoa toleo la kisasa la Tu-160 ambalo liliruka kwa mara ya kwanza miaka ya 1980 na lilipewa jina la Blackjack na NATO.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya safari ya kuruka,Rais Putin aliisifu ndege hiyo mpya kama “bora,” akibainisha kuwa ina maboresho makubwa ikilinganishwa na toleo la awali.
Safari ya ndege ya Alhamisi ilikuwa angalau mara ya tatu alipoingia kwenye chumba cha marubani cha ndege za kivita.
Mnamo 2000,Rais Putin alichukua kiti cha rubani msaidizi katika ndege ya kijeshi aina ya Su-27 na kuruka hadi Chechnya wakati wa mapigano ya kujitenga na mnamo 2005 aliongoza ndege ya Tu-160 wakati wa mazoezi ya kijeshi. lakini pia Rais Putin alikuwa rubani msaidizi katika ndege ya amphibious,
Rais Putin ambaye hazungumzi mara kwa mara zaidi ya kuonesha vitendo,aliwahi pia kuonekana akiendesha gari juu ya daraja kubwa linalounganisha Rasi ya Crimea na nchi hiyo baada ya kufanyiwa maboresha miezi kadhaa tangu liliposhambuliwa na vikosi vya Ukraine
Katika hatua nyingine,Rais huyo wa Urusi hajawahi kuonekana akiwa na mkewe katika hala zote wala safari za nje ya nchi yake tofauti na marais wengine duniani.




Discussion about this post