• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Sunday, January 18, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Habari

Kanisa Katoliki laanza mchakato wa kumtangaza Hayati Mwalimu Julius Nyerere kuwa Mtakatifu

Launda Mahakama ya Kijimbo kushughulikia mchakato huo

by bajeti
February 26, 2024
in Habari
0
Kanisa Katoliki laanza mchakato wa kumtangaza Hayati Mwalimu Julius Nyerere kuwa Mtakatifu

Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam Mhashamu Jude Thadaeus Ruwa'ichi

Share on FacebookShare on Twitter

 

NA MWANDISHI WETU

bajetinews@gmail.com

KANISA Katoliki nchini Tanzania limeanza mchakato wa kumtangaza Mtakatifu Baba wa Taifa hilo Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliyefariki dunia mnamo Oktoba 14,2019 nchini Uingereza.

Nyerere ambaye ndiye Rais wa kwanza wa Taifa hilo lenye historia ya ukarimu na amani,alitawala tangu Desemba 9, 1961 baada ya kupata uhuru wake kutoka kwa waingereza na kisha kuachia madaraka kwa hiyari.

Hata hivyo Nyerere ndiye mwasisi wa ukombozi wa mataifa mengi ya Kusini mwa Afrika.

Uamuzi wa Kanisa hilo umekuja wakati ambapo taarifa kutoka nchini Uganda zikieleza kuwa tayari mchakato huo ulishaanza miaka kadhaa nyuma juu ya kutangazwa kwa Baba wa Taifa  Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kuwa mwenye Heri na Mtakafu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Februari 25,2024  na Kanisa hilo Jimbo Kuu la Dar es Salaam na kusainiwa na Askofu Mkuu Juda Thadaeus Ruwa’ichi ameeleza kuwa ameunda Mahakama ya  Jimbo Kuu la Dar es Salaam inayoshughulikia mchakato wa kutangazwa Mwenye Heri na Mtakatifu ,Mtumishi wa Mungu Julius Kambarage Nyerere.

Ameeleza kuwa Mahakama hiyo ya kijimbo itashughulikia ufuatiliaji wa maisha ,fadhila kubwa na sifa za utakatifu na nguvu ya maombezi ya Mtumishi wa Mungu.

”Mhashamu Askofu Mkuu JudeThadeus Ruwaichi ameunda Mahakama hiyo baada ya ombi lililowasilishwa kwake Julai 23,2023 na Bruda Reginald D.Cruz  wa Shirika la Wamisionari wa Afrika ,aliyeteuliwa kisheria kuwa Mratibu wa Mchakato huo na Mshashamu Askofu Mkuu Gervas John Nyaisonga ,Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania  na mwombaji wa kufanyika kwa mchakato huo.

”Hivyo Askofu Mkuu Ruwaichi anamualika yeyote mwenye taarifa yoyote ,iwe ya kufaa au isiyofaa kuhusu maisha na fadhila kubwa sana za Mtumishi wa Mungu kama Mwamini Mlei Mkatoliki na Baba wa familia.

”Pia taarifa kuhusu sifa zake za Utakatifu na nguvu ya maombezi yake,kuziwasilisha kwenye Mahakama hiyo ya Jimbo Kuu la Dar es Salaam inayoshughulikia mchakato huo’’amesema Ruwaichi”amesema Askofu Ruwa’ichi

Askofu Ruwaichi amebainisha kuwa kwa kuwa kuna taratibu za ushahidi wa kisheria ,maandiko yote yanayodhaniwa kuwa yake yanapaswa kukusanywa.

”Kwa tangazo hilo inaelekezwa kwamba yeyote ambaye ana maandiko hayo ,pamoja na nyaraka zozote zilizoandikwa na Mtumishi wa Mungu ambazo bado hazijakabidhiwa kwa Mratibu wa Mchakato ayatume kwa umakini kwa Mahakama hiyo.

”Inakumbushwa kwamba neno ‘’maandiko’’isielewe kama machapisho tu ambayo yameshakusanywa bali pia miswada,shajara,barua na maandishi binafsi ambavyo vinaweza kudhihirisha maisha ya kiroho ya Mtumishi wa Mungu Julius Kambarage Nyerere na wale wanaohitaji kubaki na maandiko halisi wanaweza kuwasilisha nakala iliyothibitishwa ipasavyo”ameongeza Askofu Ruwa’ichi

Hata hivyo tangazo hilo litabaki kwa muda wa miezi sita katika milango yote ya Kanisa Kuu la Mtakatifu Yosefu na makanisa yote ya maparokia ya Metropolitani ya Dar es salaam

 

Next Post
CCM-Zanzibar:Wananchi wanahitaji siasa za kuvumiliana na ustaarabu

CCM-Zanzibar:Wananchi wanahitaji siasa za kuvumiliana na ustaarabu

Jeshi la Polisi Songwe na mikakati ya ulinzi na usalama

Jeshi la Polisi Songwe na mikakati ya ulinzi na usalama

Donge -Zanzibar

Donge -Zanzibar

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:23
  • Today's page views 23
  • Total visitors 13,180
  • Total page views 14,926

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In