• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Wednesday, April 15, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Habari

Kasi ya Air Tanzania  ‘kupasua anga la dunia yatisha’

Kutua Accra nchini Ghana mara tatu kwa wiki

by bajeti
January 29, 2026
in Habari
0
Kasi ya Air Tanzania  ‘kupasua anga la dunia yatisha’

Ndege ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) zinazojulikana kama Air Tanzania

Share on FacebookShare on Twitter

 

NA GOODLUCK HONGO

SHIRIKA la Ndege Tanzania (ATCL) limeendelea kuongeza safari za ndege  katika nchi mbalimbali duniani ikiwemo barani Afrika ambapo kwa sasa limeingia rasmi nchini Ghana.

ATCL ikiwa na ndege zake za Air Tanzania ambayo kwa sasa inatua katika majiji makubwa duniani ikiwemo Mumbai nchini India imeendelea kuongeza wigo wa safari zake ambapo mbali na kusafirisha abiria lakini pia linasafirisha na mizigo.

ATCL ambalo ndio Shirika lenye ndege mpya barani Afrika litaanza rasmi safari za moja kwa moja kutoka Tanzania hadi jiji kuu la Accra nchini Ghana mara tatu kwa wiki.

Hayo yanakuja wakati Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) 2025-2030 imeeleza kuwa Serikali yake itaendelea  kuimarisha usafiri wa anga  ambapo katika miaka mitano iliyopita, kuanza kuimarika kwa usafiri wa anga umechochea sana shughuli za utalii na huduma ya usafiri kwa wananchi kwa ujumla.

“Ni lengo la CCM kuona kuwa usafiri wa anga nchini unaendelea kuimarika kwa kuimarisha Shirika la Ndege Tanzania kwa kuongeza idadi ya ndege za abiria na mizigo, na kuboresha uendeshaji wake.

“Kukamilisha ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Msalato Dodoma na kukamilisha ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Mwanza na kukipandisha hadhi kuwa cha Kimataifa pamoja na  kukamilisha ukarabati na upanuzi wa viwanja vya ndege vya Tanga, Lake Manyara, Lindi na Iringa”Imeeleza Ilani hiyo

Akizungumza katika kipindi cha maswali na majibu bungeni jijini Dodoma Januari 29,2026 katika Bunge la 13 Mkutano wa pili, Kikao cha tatu,Naibu Waziri wa Uchukuzi  David Kihenzile amebainisha kwamba tayari Waziri wa Uchukuzi Prof.Makame Mbarawa ameongozana na timu maalum nchini Ghana juu ya uzinduzi wa safari za ndege za Air Tanzania.

Amebainisha kuwa hicho kitakuwa kituo cha 17 kikiwa kimeanzishwa  ndani ya siku 100 za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan  ambapo ndege kubwa wa kubeba abiria 180 ambayo ni Boing B 737- MAX 9 mbapo itasafiri moja kwa moja hadi Accra Ghana

“Watanzania wanaweza kwenda moja kwa moja mpaka Accra nchini Ghana   siku za Jumatatu,Jumatano na Ijumaa,hii ni habari kubwa na nzuri.

“Tumpongeze Rais wetu Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa maono makubwa na yanayotekelezeka   na yanayoonekana”amesema Kihenzile

Awali akijibu swali na Mbunge wa Ilemela Kafiti Kafiti aliyetaka kujua kuhusu mgogoro wa wananchi na kiwanja cha ndege cha Mwanza,Naibu Waziri Kihenzile amebainisha kuwa Serikali inaendelea kulishughulikia suala hilo kupitia timu ya wataalam iliyoundwa na Ofisi ya Waziri Mkuu itakayofanya uchambuzi wa kina juu ya suala hilo.

“Timu hiyo pamoja na mambo mengine itatoa mapendekezo kwa ajili ya maamuzi ya Serikali  na Waziri wetu Mkuu kwa kutambua uzito na umuhimu ameamua kuunda Tume au timu ishughulikie  na hatimaye tufikie mahali pazuri ili wananchi wetu wa Shibula  na mitaa mitano  na wananchi wa Ilemela na Mwanza kwa ujumla  tufikie hatima ya mgogoro huu

“Dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita ni kuhakikisha kwamba Uwanja wa ndege wa Mwanza unaboreshwa na tunajenga jengo la abiria kubwa  na mwisho na muhimu kuliko yote tunataka tuufanye uwanja wa ndege wa Mwanza kuwa wa kimataifa,ili ufanikishe hilo lazima uhakikishe kwamba usalama unazingatiwa na huwezi kuwa na usalama kama wananchi watakuwa wamevamia kwenye maeneo ya uwanja”amefafanuwa Kihenzile

Awali akiuliza swali la nyongeza, Kafiti amefafanuwa kuwa mgogoro huo wa wakazi hao na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege umechukua muda mrefu wa zaidi ya miaka 10 sasa

“Kwa kuwa Serikali imekiri uwepo wa mgogoro huu wa muda mrefu na ni shukuru Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kuweza kuteua Tume hii ya kitaalamu kuweza kushughulikia mgogoro huo,mgogoro huu ni wa muda mrefu na unahusisha wakazi katika Kata ya Sibula na  mitaa mitano  ikiwemo Simba A,Bulyanhulu,Nyaminyolelwa pamoja na Kihili .

“Mitaa hii mitano imekuwa katika mgogoro mkubwaambapo wakazi hao sasa wanashindwa kueendeleza makazi yao.

“Ni nini kauli ya Serikali kuhakikisha kwamba Kamati hii iliyoundwa lini itakwenda kukamilisha suala hili ili wananchi wa Kata hizi waweze kupata muafaka wa suala hili”ameuliza Kafiti

Next Post
Tanzania nchi ya tano duniani kwa kujenga Reli ndefu ya kisasa (SGR)

Tanzania nchi ya tano duniani kwa kujenga Reli ndefu ya kisasa (SGR)

Wilaya 75 hazina vituo vya Polisi ikiwemo Maswa

Wilaya 75 hazina vituo vya Polisi ikiwemo Maswa

Ugonjwa Homa ya Ini tishio mikoa tisa, ‘ngono’yatajwa kusababisha

Ugonjwa Homa ya Ini tishio mikoa tisa, ‘ngono’yatajwa kusababisha

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:18
  • Today's page views 18
  • Total visitors 15,722
  • Total page views 17,815

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In