• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Monday, May 18, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Habari

Ugonjwa Homa ya Ini tishio mikoa tisa, ‘ngono’yatajwa kusababisha

Serikali yawataka wananchi kwenda hospitali  kupata chanjo na matibabu

by bajeti
February 1, 2026
in Habari
0
Ugonjwa Homa ya Ini tishio mikoa tisa, ‘ngono’yatajwa kusababisha

Naibu Waziri wa Afya Dkt.Frolence Samiz (Picha na Wizara ya Afya )

Share on FacebookShare on Twitter

 

NA MWANDISHI WETU,DODOMA

SERIKALI imetaja Mikoa tisa ya Tanzania Bara kuwa inaongoza kwa maambukizi ya Ugonjwa wa Homa ya Ini kwa kuvuka viwango vya kitaifa  ambao pia huambukizwa kwa njia za kujamiiana kama ulivvyo UKIMWI.

Hata hivyo Serikali imewatoa hofu wananchi kuwa chanjo na matibabu ya ugonjwa huo zinapatikana katika hospitali zote nchini zikiwemo za Kanda na Rufaa.

Mikoa hiyo imetajwa na Naibu Waziri wa Wizara ya Afya Dkt. Frolence Samiz Januari 29,2026 Bungeni jijini Dodoma wakati wa kipindi cha maswali na majibu  katika Bunge la 13 Mkutano wa pili.

Naibu Waziri Dkt Samiz ametoa maelezo hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kigoma kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Naomi Mwaipopo ambaye alitaka kujua kuhusu jitihada za Serikali katika kuutokomeza ugonjwa huo.

Akiuliza swali la nyongeza,Mbunge Mwaipopo amesema,“Pamoja na majibu mazuri ya Serikali kuhusu ugonjwa wa Ini katika Mkoa wa Kigoma,Mheshimiwa Mwenyekiti Kigoma imepakana na nchi tatu za jirani Burundi,Congo na Rwanda  hivyo maambukizi kwenye mkoa  ni makubwa ukilinganisha na mikoa mingine

Mwaipopoi ameishukuru Serikali kwa jitihada kubwa inayoifanya kwenye mkoa huo hasa kwenye Wizara ya Afya,ambapo sasa hivi wana hospitali ya mkoa ambayo imekamilika.

“Sasa hivi unapima kila kitu Kigoma,hatuendi tena Muhimbili wala Bugando,pongezi kwa Serikali lakini pia Wizara ya Afya,majibu ya Serikali kwenye ugonjwa huu Mwenyekiti niombe waongeze juhudi kwa sababu.

“Ugonjwa huu unaambukizwa sawa kabisa na maambukizi ya VVU,kwa maana ya kwamba unaambukizwa kwa kutumia vitu vyenye ncha kali,unaambukizwa kupitia ngono,zile sababu zinazosababisha kupata ugonjwa wa UKIMWI ndio sababu zinazosababisha kupatikana kwa ugonjwa wa Homa ya Ini

“Pamoja na Elimu wanayoitoa lakini maambukizi kwa Mkoa wetu wa Kigoma bado yako juu,”Je Serikali inampango gani mkakati wa kuhakikisha ugonjwa huu unatokomezwa kabisa kwenye Mkoa wa Kigoma”amesema Mwaipopo.

Akijibu swali hilo,Naibu Waziri Dkt.Samizi amesema anampongeza Mbunge Naomi kutoka Mkoa wa Kigoma kwa kujali maisha ya wananchi wa Mkoa wa Kigoma ili wasiendelee kuathirika na ugonjwa huo wa Homa ya Ini.

“Kipekee kabisa nimpongeze Daktari Samia Suluhu Hassan,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye kwa juhudi za makusudi kabisa amewekeza sana kupambana na ugonjwa huu wa Ini.

“Kwa sasa hivi ugonjwa huu wa Ini unao chanjo kwa watoto wadogo ambayo inatolewa bure,ambapo mtoto tu anapozaliwa wanapewa chanjo hii wiki nne,10 na 12 bure,mama akijifungua tu anaingizwa kwenye mpango wa kupata chanjo.

“Lakini sio hiyo tu ipo chanjo kwa ajili ya watu wazima hivyo tupo sisi ambao hatukupata chanjo ya utotoni ,tunayo chansi ya kuchanja tukiwa watu wazima ambao tunapata chanjo kwa ajili ya kujikinga na ugonjwa huu wa Homa ya Ini”amefafanuwa Dkt Samiz

Amesema kwa jitihada za makusudi za kutokomeza ugonjwa huo wa Ini,Serikali imeanzisha tiba ya ugonjwa huo ambapo mpaka sasa inatolewa kwenye hospitali zote za Rufaa za Mkoa nchi nzima lakini pia inatolewa kwenye Hospitali zote sita za Kanda na kwenye Hospitali ya Taifa .

“Niwahimize watanzania wote kwamba sasa chanjo kwa ajili ya ugonjwa wa Ini ipo,tiba kwa ajili ya ugonjwa Ini ipo,waende hospitalini watapata matibabu”amesema Dkt.Samiz

Hata hivyo Naibu Waziri Dkt.Samizi amekiri kuwa ugonjwa huo wa Ini unaambukizwa sawasawa na Ugonjwa unavyoambukizwa wa UKIMWI,

Amebainisha kuwa wao kama Wizara wataongeza juhudi kwa kufanya usimamizi shirikishi  wa miongozo yote ya kusimamia magonjwa hayo na hasa kwa mikoa ambayo imeathirika zaidi na iko juu ya kiasi cha kitaifa.

“Hepatitis kitaifa ni asilimia 3.5 lakini iko mikoa ambayo iko juu ya asilimia 3.5 ikiwemo Rukwa ,Katavi,Geita,Kigoma,Morogoro,Mara,Songwe ,Tanga na Simiyu

“Tutafanya juhudi ili kutokomeza ugonjwa huu wa Ini kwenye mikoa hii iliyoathirika zaidi.

“Nitoe rai kwa watanzania wote tujitokeze kupimwa kwa sababu wengi wetu hatujui hali zetu za Hepatitis na imekuwa desturi kwamba mtu akijipima UKIMWI basi anajua yuko salama na kuendelea na ngono nzembe ,naomba niwahakikishe kwamba Hepatitis ipo na tuchukue tahadhari tuweze kujikinga na ugonjwa huu.”ameeleza Dkt.Samiz

Aidha amewaomba wabunge katika ,maeneo yao husika kushirikiana na Serikali katika kuendelea kutoa elimu kwa ajili ya wananchi ikiwemo kwenda kupima ili waendelee kupata chanjo  na matibabu

“Serikali pia imejumuisha huduma hizi za Ugonjwa wa Ini pamoja na UKIMWI ili kuweka huduma hizi jumuishi,na kama ambavyo suala hili ni mtambuka,Wizara zote zimeshapata muongozo wa kuendelea kuwaelimisha watumishi wao na kuwahudumia.

“Nitoe rai kwa Taasisi zote kama ambavyo tulikuwa tukiwahudumia wagonjwa wa UKIMWI lakini kuendelea kuwapima watumishi wetu basi tuendelee kutumia mpango huu jumuishi ili pia watumishi wote katika Taasisi zote wanufaike na huduma hii ya kupimwa,kuchanjwa na kupata matibabu kwa ajili ya ugonjwa huu wa Ini”amebainisha Dkt Samiz

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa (UN) Homa ya Ini ni kuvimba kwa Ini, kitendo cha Ini kuvimba ghafla ndio huitwa Homa kali ya Ini  na sababu zinazofahamika zaidi za Ini kuvimba ghafla ni maambukizi ya virusi vya Homa ya Ini aina A na E ikiwemo aina za dawa za matibabu ambazo zina sumu inayoweza pia kusababisha Homa Kali ya Ini.

Baadhi ya dalili za ugonjwa huo ni pamoja na kutapika, kuhara au maumivu ya tumbo,rangi ya manjano kwenye macho na ngozi na choo kilicho na rangi mpauko.

Next Post
Kahawa ya Tanzania yaongoza kwa ubora duniani,husaidia kuongeza uwezo wa kufikiri ,kuishi miaka mingi.

Kahawa ya Tanzania yaongoza kwa ubora duniani,husaidia kuongeza uwezo wa kufikiri ,kuishi miaka mingi.

‘Moto wa Waziri Mkuu Dkt.Nchemba waanza kuchoma’,Katibu Mkuu adaiwa kudhulumu Kampuni

‘Moto wa Waziri Mkuu Dkt.Nchemba waanza kuchoma’,Katibu Mkuu adaiwa kudhulumu Kampuni

TFS na mikakati ya kulinda Mazao ya Misitu Kiteto

TFS na mikakati ya kulinda Mazao ya Misitu Kiteto

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:3
  • Today's page views 3
  • Total visitors 16,270
  • Total page views 18,443

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In