• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Tuesday, April 28, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Habari

MSD yaanza kuzalisha bidhaa za afya kupunguza gharama za uagiza nje

Yamshukuru Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuifanyia mengi Sekta ya Afya

by bajeti
April 28, 2026
in Habari
0
MSD yaanza kuzalisha bidhaa za afya kupunguza gharama za uagiza nje

Mteknolojia wa Bohari ya Dawa Tanzania (MSD) Said Omary

Share on FacebookShare on Twitter

MFAUME PASTORY,NJOMBE

BOHARI ya Dawa Tanzania (MSD)  imeanza kuzalisha bidhaa za afya hapa nchini ili kupunguza gharama za uagizaji wa dawa kutoka nje ya nchi.

MSD ambayo ilianzishwa mwaka 1993 kwa Sheria ya Idara ya Bohari ya Dawa,Sura ya 70. ina majukumu ya Ununuzi,Uhifadhi na Usambazaji wa bidhaa za Afya  ambapo mwaka 2020 iliongozewa jukumu la nne la Uzalisha  baada ya kutokea kwa janga la ugonjwa wa Corona mwaka 2020.

Hata hivyo mwaka 2021 Sheria hiyo ilifanyiwa marekebisho ili kupanua mamlaka yake kwa kuongeza Uzalishaji wa ndani  wa bidhaa za afya katika kazi zake.

Taasisi hiyo nyeti kwa mhimili wa bidhaa bora za afya kwa watumiaji wake inaongozwa na Mkurugenzi Mkuu Mavere Tukai na imekuwa ikihakikisha kuwa Vituo vya Umma vinapata dawa kwa wakati licha ya Tanzania kuwa na ongezeko kubwa la idadi ya watu katika miji mbalimbali jambo linaloweza kuleta changamoto kutokana na ongezeko la wagonjwa katika vituo husika.

Moja ya bidhaa za afya zinazosambazwa na Bohari ya Dawa Tanzania (MSD)

Akizungumza na Bajeti Communication Aprili 27,2026 katika maonesho  yaliyoandaliwa na Wakala wa Usalama wa Mahali na Afya Mahala pa Kazi (OSHA) yanayoendelea mkoani Njombe,Mteknolojia wa MSD Said Omary amesema MSD ilikuwa na majukumu matatu tangu kuanzishwa kwake lakini  mwaka 2020 ilipewa jukumu lingine la Uzalishaji ambapo ilihitajika baada ya kutokea changamoto ya ugonjwa wa Korona ambao uliathiri dunia na mnyonyoro  mzima wa ugavi,

Amesema wao kama Bohari ya Dawa walikuwa wakiagiza na kununua bidhaa za afya kutoka sehemu mbalimbali lakini mahitaji ya bidhaa hizo hasa za kujikinga zikiwemo barakoa,gloves na nyingine yaliongezeka sana baada ya kutokea changamoto ya ugonjwa wa Korona na ikawa kuna changamoto pia ya usambazaji lakini pia matumizi yaliongezeka.

“Hivyo Bohari ya Dawa ikapewa jukumu la kuweza kuanzisha uzalishaji wa bidhaa hizo kuanzia mwaka 2021 Bohari ya Dawa ilianza kuzalisha bidhaa za barakoa ambayo inapatikana katika Kiwanda kilichopo Keko Dar es Salaam lakini sambamba na hilo,Bohari Kuu ya Dawa kuanzia mwaka 2023 imeanza kuzalisha bidhaa ya pili ambayo ni gloves ambayo inapatikana katika kiwanda chake kilichopo katika eneo la Makambako Mkoa wa Njombe.

“Kwa sasa hivi Bohari ya Dawa inaweza kuzalisha na kusambaza bidhaa hizo kutoka ndani ya nchi hapa hapa na kukidhi soko kwa zaidi ya asilimia 80 ya mahitaji ya Tanzania nzima.

“Kwa sasa hivi ukienda katika hospitali zote nchini  Tanzania utaona tayari bidhaa hiyo imeshafika sokoni,utaona barakoa za kawaida,barakoa kubwa kwa ajili ya kujikinga zaidi(Respilatory musk),kuna gloves kwa ajili ya kufanyia uchunguzi ,zipo katika vituo vyote vya afya nchini zinapatikana na zinafanya vizuri sokoni na tunapata mrejesho kutoka kwa wateja wetu zikiwemo hizo hospitali tunazozihudumia”amesema Omary

Banda la MSD katika Maonesho yaliyoandaliwa na Wakala wa Usalama na Afya Mahala pa Kazi (OSHA) mkoani Njombe Aprili 27,20206

Aidha Omary amebainisha kuwa utaratibu wao katika Viwanda vinavyozalisha hizo bidhaa huzichukua na kuzisambaza katika vituo mbalimbali vya afya kupitia mfumo wa kuwauzia kutoka katika Bohari ya Dawa yenyewe kama ambavyo walivyokuwa wanapata bidhaa nyingine hivyo hivyo pia bidhaa hizo huingia katika mfumo ule ule wa ugavi  na wataziomba kutoka Makao Makuu ya Bohari ya Dawa kupitia Kanda zote 10 zilizopo na zitawafikia katika vituo vyao kama ambavyo zinavyowafikia bidhaa zingine.

Amesema Mtanzania wa kawaida  lazima awe na imani na Bohari ya Dawa kwani ipo na inajitahidi sana kuhakikisha kuwa huduma zote za bidhaa za afya inasambaza hadi kwa mtumiaji wa mwisho.

Amebainisha kuwa  Bohari Kuu ya Dawa imejidhatiti katika kuhakikisha kuwa jukumu la nne la Uzalishaji linakwenda vizuri na linasambaza bidhaa hizo ambazo wanazalisha wenyewe kwa ajili ya kupunguza gharama ya uagizaji kutoka nje lakini pia gharama kwa mtumiaji wa mwisho.

“Kwa hiyo Watanzania wawe na imani na Bohari Kuu ya Dawa lakini pia Serikali ya Awamu ya Sita kupitia kwa Rais wetu Dkt.Samia Suluhu Hassan ambaye anafanya mengi sana hasa katika Sekta ya Afya ikiwemo usambazaji wa vifaa tiba pamoja na bidhaa zote za afya zinakwenda hadi kwa Mtanzania wa mwisho kwa hali ya juu sana.

“Bohari Kuu ya Dawa katika majukumu yake manne pia inajukumu la usambazaji wa bidhaa za Afya ambapo bidhaa hizi kwa mujibu wa utaratibu wa Bohari Kuu ya Dawa ni kumsambazia au kumpelekea mtumiaji wa mwisho mpaka kwenye kituo ambacho atapatiwa huduma ya afya kwa maana kuanzia kwenye ngazi ya chini ya Zahanati mpaka kufika katika Hospitali za Taifa na zile teule zilizopo katika Kanda tofauti tofauti ambapo utaratibu wake Bohari ya Dawa watachukua maombi kutoka katika vituo hivyo vya afya na baada ya hapo maombi hayo yatachakatwa  na mzigo utaandaliwa.

“Bohari ya Dawa ndiyo yenye jukumu la kupeleka bidhaa hizo za Afya mpaka kwenye kituo au zahanati yeyote zilizopo nchi nzima,ambapo kwa sasa hivi MSD inahudumia zaidi ya Vituo 8000 katika kusambaza hizo bidhaa za Afya na mapaka sasa hivi hakuna kituo hata kimoja ambacho hakifikiwi ndani ya mwaka”ameeleza Omary

Kutokana na mfumo huo MSD hadi sasa inakidhi mahitaji ya dawa nchini kwa zaidi ya asilimia 80 kwa kuwa walikuwa wakiagiza dawa kutoka sehemu mbalimbali za dunia ili kukidhi mahitaji hayo.

Ameeleza kuwa kila kituo kitafikiwa mara sita kwa mwaka  kwa maana kwamba kila miezi miwili kituo cha afya kitapelekewa bidhaa zake ambazo zitakuwa imeziagiza.

Katika hatua nyingine,Omary amefafanuwa kuwa mfumo huo unafanya kazi kama jukumu linavyoainisha kwa vituo vyote vya afya vya Serikali vilivyopo nchini Tanzania kuanzia Zahanati hadi Hospitali Kuu ya Taifa lakini pia vituo binafsi ambavyo vitakuwa vimepewa kibali na Serikali kwa ajili ya kununua hizo bidhaa katika Bohari ya Dawa ya Serikali yaani MSD.

Next Post
ESAP yaanza utengenezaji vilipuzi kwa ajili ya uchimbaji madini

ESAP yaanza utengenezaji vilipuzi kwa ajili ya uchimbaji madini

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:28
  • Today's page views 37
  • Total visitors 15,961
  • Total page views 18,111

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In