• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Monday, June 1, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Habari

Halmashauri Mji Njombe,Makambako vinara ulipaji madeni,Ludewa yajikongoja

Waziri Dkt.Akwilapo azishukuru halmashauri zilizomaliza madeni yao

by bajeti
June 1, 2026
in Habari
0
Halmashauri Mji Njombe,Makambako vinara ulipaji madeni,Ludewa yajikongoja

Wakurugenzi wa Halmashauri Mji Njombe,Makambako pamoja na Ludewa

Share on FacebookShare on Twitter

 

NA MFAUME PASTORY,NJOMBE

HALMASHAURI  ya Mji Njombe na Makambako mkoani Njombe zimetajwa kuwa halmashauri  zilizofanikiwa kukopa na kurejesha mkopo wote wa fedha  iilizopatiwa kwa ajili ya  Utekelezaji wa Miradi ya Kupanga, Kupima na Kumilikisha Ardhi (KKK) Mwaka 2021/22.

Taarifa hiyo imeelezwa na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Leonard Akwilapo Mei 28,2026 katika hotuba yake bungeni Jijini Dodoma alipokuwa akiwasilisha Makadirio na Mapato na Matumizi ya Wizara kwa Mwaka wa Fedha 2026/2027.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Njombe mkoani Njombe Kuruthum Sadick

Dkt.Akwilapo ameeleza kuwa Halmashauri ya Mji Njombe ilikopeshwa kiasi cha Sh. Milioni 700 na imefanikiwa kurejesha kiasi chote cha fedha wakati Halmashauri ya Mji Makambako ilikopeshwa kiasi cha Sh. Milioni 683.3 na imefanikikiwa kurejesha kiasi chote cha mkopo huo.

 

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Makambako mkoani Njombe Keneth Haule

Katika kuwezesha utekelezaji wa vipaumbele na Mpango wa Bajeti wa Wizara kwa mwaka 2026/27, Waziri Dkt Akwilapo ameliomba Bunge kuidhinisha bajeti ya jumla ya Shilingi Bilioni 210.2 kwa ajili ya matumizi ya mafungu yote mawili (Fungu 48 – Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi) na (Fungu 03 – Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi).

 Mkurugenzi Mtendaji wa Halmshauri ya Wlaya ya Ludewa mkoani Njombe Sunday Deogratias

Kwa upande wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa imetajwa kuwa miongoni mwa Halmashauri ambazo zimerejesha sehemu ya fedha katika deni la kiasi cha Sh. Milioni  405.0 fedha iliyokopeshwa kwa ajili ya Utekelezaji wa Miradi ya Kupanga, Kupima na Kumilikisha Ardhi (KKK) Mwaka 2021/22.

Mratibu wa kodi ya ardhi Mkoa wa Njombe Godfrey Masunga akiwa katika moja ya majukumu yake ya kutoa elimu juu ya umuhimu wa kulipa kodi ya ardhi

Kwa mujibu wa Waziri Akwilapo katika hotuba yake bungeni ameeleza kuwa Halmashauri ya Ludewa ilikopeshwa kiasi cha Sh. Milioni 405.0 na imefanikiwa kurejesha kiasi cha Sh.Milioni 147.64 na kiasi ambacho bado inadaiwa ni Sh.Milioni  257.35 sawa na asilimia 36

“Wizara imeendelea kuziwezesha halmashauri ili kuongeza kasi ya kupanga, kupima na kumilikisha ardhi kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Ardhi (Plot Development Revolving Fund – PDRF) ambao moja ya vyanzo vyake ni marejesho ya fedha shilingi bilioni 50.00 zilizokopeshwa mwaka 2021/22 kwenye halmashauri 57, Vyuo vya Ardhi vya Tabora na Morogoro, Chuo Kikuu Ardhi na Ofisi ya Ardhi Mkoa wa Iringa.

“Hadi tarehe 15 Mei 2026, Shilingi bilioni 33.18 zimerejeshwa sawa na asilimia 66.41 ya fedha zilizokopeshwa. Wizara inaendelea kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu- TAMISEMI na Wizara ya Fedha kuchukua hatua madhubuti kwa halmashauri zote ambazo hazijakamilisha kurejesha fedha hizo.

Nitumie fursa hii kuzipongeza halmashauri ambazo zimekamilisha marejesho ya fedha zilizokopeshwa na kuzitaka halmashauri ambazo hazijakamilisha kurejesha mikopo hiyo zifanye hivyo mara moja ili kuziwezesha halmashauri nyingine nchini kunufaika na fursa hiyo.”amesema Dkt.Akwilapo

Kwa mujibu wa hotuba ya Waziri Dkt.Akwilapo ni kuwa jumla  Halmahauri zilizorejesha kiasi chote cha fedha ni pamoja na  Moshi DC,Jiji la Mwanza, Meru,Morogoro,Kilosa, Geita,Halmashauri ya Mji Bariadi, Mbozi, Ilemela,Ileje,Halmashauri ya Mji Tunduma, Songwe,Kaliua, Ofisi ya Ardhi Mkoa wa Iringa,Kigamboni,Halmashauri ya Mji Kibaha,Sumbawanga,Mbulu,Halmashauri ya Jiji la Tanga,Hanang’,Rhombo ,Halmashauri ya Mji Njombe,Ushetu,Halmshauri ya Mji Makambako,Halmashauri ya Jiji la Dodoma ,Kikuu Ardhi naHalmashauri ya  Jiji la Mbeya.

Halmashauri zilizorejesha Sehemu ya Fedha ilizokopeshwa ni pamoja na Halmashauri ya Mji Bunda,Halmashauri ya Mbeya, Buchosa,Uyui,Mtwara,Babati,Musoma,Chalinze,Halmashauri ya Mji Mbinga,Butiama,Meatu,Tabora,Halmshauri ya Mji Babati,Musoma,Halmshauri ya Mji Tarime,Morogoro, Ludewa, Ikungi,Kishapu,Msalala,Roryam,Shinyanga,Maswa,Lushoto,Lindi,Chamwino,Halmashauri ya Mji  Mbulu ,Shinyanga,Manyoni,Halmashauri ya Mji Korogwe na Halmshauri ya Korogwe .

Next Post
Udhibiti vidukari katika zao la mpunga utakavyoimarisha usalama wa chakula.

Udhibiti vidukari katika zao la mpunga utakavyoimarisha usalama wa chakula.

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:40
  • Today's page views 45
  • Total visitors 16,706
  • Total page views 18,963

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In