• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Saturday, July 18, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Habari

Waingereza,Wachina na Mjerumani wakamatwa wakijihusisha na dawa za kulevya

by bajeti
July 18, 2026
in Habari
0
DCEA yazuia tani 159.3 za Kemikali Bashirifu kuingizwa nchini

Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibi na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Aretas Lyimo akitoa ufafanuzi kuhusu zoezi la uteketezaji wa dawa za kulevya zikiwemo kemikali bashirifu nchini kwa mujibu wa sheria wakati wa uteketezaji wa kilo 614.12 katika Kiwanda cha Saruji cha Twiga kilichopo Wazo mkoani Dar es Dalaam Desemba 19,2024

Share on FacebookShare on Twitter

NA GOODLUCK HONGO

RAIA 14 kutoka mataifa ya kigeni wakiwemo Waingereza,Wachina na Mmarekani wamekamatwa nchini wakijihusisha na dawa za kulevya

Raia wengine waliokamatwa ni pamoja na raia kutoka Marekani na Sri lanka ambapo kwa pamoja wanajumuisha watuhumiwa ambao ni raia wa kigeni kufikia 14.

Kwa mujibu wa Taarifa ya Hali ya Dawa za Kulevya ya Mwaka 2025 iliyotolewa Mei,2025 na kuwekwa saini na Waziri wa Nchi ,Ofisi ya Waziri Mkuu(Sera,Bunge,Uratibu na Wenye Ulemavu) Prof.Palamagamba Kabudi pamoja na Kamishna Jenerali  wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) kuwa  raia wa kigeni 14 walikamatwa nchini kwa kujihusisha na dawa za kulevya.

“Mwaka 2025,raia wa kigeni 14 walikamatwa kwa tuhuma za kujihusisha na dawa za kulevya,kutoka nchi za China wawili,Lebanoni mmoja,Congo mmoja,Sri Lanka wawili,Uingereza wawili,Marekani mmoja,Naigeria mmoja,Ujerumani mmoja,Kenya mmoja,Msumbiji mmoja, na Uganda mmoja”imeeleza taarifa hiyo

Kwa upande wa watanzania waliokamatwa nje ya nchi kwa kujihusisha na dawa za kulevya,taarifa hiyo imefafanuwa kuwa takwimu za mwaka 2025 zinaonesha kuwa juma la watanzania 28 walikamatwa.

Taarifa hiyo imebainisha kuwa 20 kati yao walikamatwa nchini Zambia,wawili nchini Botwana,wawili nchini Msumbiji,Mauritania mmoja,Japan mmoja,Ufaransa mmoja na Shelisheli mmoja.

Hata hivyo idadi ya watanzania imeendelea kushuka katika kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya ambapo kwa mujibu wa Taarifa ya Hali ya Dawa za Kulevya ya Mwaka 2022 imeonesha kuwa watanzania waliokamatwa nje ya nchi kwa kujihusisha na dawa za kulevya  walikuwa 147 ambapo wanaume  walikuwa 136 na wanawake 11.

 

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:10
  • Today's page views 10
  • Total visitors 21,069
  • Total page views 23,455

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In