• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Sunday, October 18, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Mazingira

Kakonko ‘wamkuna’Waziri Masauni matumizi ya nishati safi ya kupikia, ujenzi kiwanda cha kuzalisha tani 730 za mkaa mbadala

by bajeti
October 17, 2026
in Mazingira
0
Kakonko ‘wamkuna’Waziri Masauni matumizi ya nishati safi ya kupikia, ujenzi kiwanda cha kuzalisha tani 730 za mkaa mbadala

3. WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhandisi Hamad Yussuf Masauni akiangalia mmoja wa mkaa unaotengenezwa Kiwanda cha Mkaa Mbadala kilichopo Wilaya ya Kakonko, Oktoba 16, 2026.

Share on FacebookShare on Twitter

NA MWANDISHI WETU,KIGOMA

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhandisi Hamad Yussuf Masauni, amesema ameupongeza uongozi wa Wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma kwa namna ambavyo wamekuwa wakihamasisha jamii juu ya matumizi ya nishati safi ya kupikia.

Mhandisi Masauni ameyasema hayo Oktoba 16,2026  wakati wa ziara yake ya siku nne mkoani Kigoma baada ya kutembelea na kukagua Kiwanda cha Mkaa Mbadala kilichopo Wilaya ya Kakonko.

Amesema ni muhimu kwa uongozi wa wilaya hiyo kuendelea kutoa elimu juu ya utunzaji wa mazingira pamoja na matumizi ya nishati safi ya  kupikia ili kupunguza ukataji holela wa misitu na uchomaji moto.

Mhandisi Masauni amesema wilaya hiyo ina utajiri mkubwa wa misitu ambayo wakiitumia vizuri jamii itanufaika na Biashara ya Kaboni ambayo baadhi ya Halmashauri nchini tayari zimeanza kunufaika.

“Ukataji wa miti na kutumia kuni kupikia kuna athari kubwa kuanzia kwa mtumiaji kwa kuwa moshi anaovuta una madhara yake, miti anayokata inaharibu ardhi na kusababisha athari kubwa zaidi,” amesema Mhandisi Masauni.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhandisi Hamad Yussuf Masauni akisalimiana na baadhi ya viongozi wa Wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma wakati alipowasili wilayani humo, Oktoba 16, 2026 kwa ajili ya ziara ya kikazi.Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali Evance Mallasa

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Kakonko, Kanali Evance Mallasa amesema Wilaya imeendelea kuimarisha juhudi za utunzaji wa mazingira kwa kutoa elimu kwa wananchi kuhusu uhifadhi wa misitu na matumizi ya nishati safi ya kupikia, ikiwa ni sehemu ya mikakati ya kupunguza ukataji holela wa miti na uchomaji moto.

Katika hatua nyingine, Wilaya kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo imefanikiwa kujenga kiwanda cha kuzalisha mkaa mbadala kinachotarajiwa kuzalisha wastani wa tani 730 za mkaa kwa mwaka na kuwafikia takribani wananchi 30,000 kila mwaka, hatua inayolenga kupunguza utegemezi wa mkaa wa kuni na kusaidia uhifadhi wa misitu.

Aidha, Wilaya imeanza kuchukua hatua za kutumia rasilimali za misitu katika kukuza uchumi kupitia Biashara ya Kaboni kwa kushirikiana na wadau mbalimbali huku Wilaya ikiwa imefanya tathmini ya awali ya maeneo yanayofaa kwa biashara hiyo na kubaini maeneo 97 yenye jumla ya hekta zaidi ya laki moja.

Next Post
Askofu Gwajima: aliyewapeleka waumini wetu mahabusu wametoka na hawaogopi mabomu ya machozi

Askofu Gwajima: aliyewapeleka waumini wetu mahabusu wametoka na hawaogopi mabomu ya machozi

Joseph Kabila,Rais Mstaafu wa Kongo, uliyewafanyia mema wakongo,shukrani yao ni kumhukumu kifo,na kumfilisi mali zake

Joseph Kabila,Rais Mstaafu wa Kongo, uliyewafanyia mema wakongo,shukrani yao ni kumhukumu kifo,na kumfilisi mali zake

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:2
  • Today's page views 2
  • Total visitors 22,590
  • Total page views 25,184

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In