• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Sunday, October 18, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Makala

Joseph Kabila,Rais Mstaafu wa Kongo, uliyewafanyia mema wakongo,shukrani yao ni kumhukumu kifo,na kumfilisi mali zake

Hakuwa na chaguo lingine,wakongo wanapotoshwa kwa habari potofu.

by bajeti
October 17, 2026
in Makala
0
Joseph Kabila,Rais Mstaafu wa Kongo, uliyewafanyia mema wakongo,shukrani yao ni kumhukumu kifo,na kumfilisi mali zake
Share on FacebookShare on Twitter

NA GOODLUCK HONGO

NANI anasema Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Joseph Kabila ni mtu mbaya? Hana chaguo lingine zaidi ya kuanzisha vuguvugu jipya ili kuleta umoja, upendo miongoni mwa wakongo kama alivyofanya katika utawala wake wa miaka 18.

Alifukuzwa Kinshasa na kuporwa mali zake na kila alipojaribu kusuluhisha kwa amani ili arudi nchini kwake alizuiwa,hakuwa na chahuo lingine zaidi ya hilo aliloliamua.

Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC)  Joseph Kabila ametangazwa na vyombo vya habari  duniani  kuwa Kiongozi mpya wa Muungano mpya wa kisiasa na kijeshi, unaochukua nafasi ya ushirikiano wa AFC-M23 ambao unapambana na vikosi vya serikali ya Kongo mashariki mwa nchi hiyo, unaoitwa ‘Front for the Refounding of the Nation’ (FRN),

Kabila ambaye ni mwanajeshi (komandoo) na aliyelitumikia Jeshi la nchi hiyo kabla ya kuwa Rais alihukumiwa kifo akiwa hayupo mahakamani na mahakama ya kijeshi mnamo Septemba 2025.

Licha ya kuhukumiwa kifo na Serikali ya Kongo,Kabila pia alipokonywa mali zake,kuvuliwa useneta wa maisha  na ukatili mwingine mwingi ikiwemo kumfanya kushindwa kuishi katika nchi aliyoiongoza na kuondoa ukabila,udini,upendeleo na kuliimarisha jeshi la nchi hiyo lililokuwa limegawanyika vipande vipande.tangu Uhuru wa nchi hiyo.

Rais Mstaafu Kabila akisikiliza kero za wakongo

Hakuna ubishi kuwa uzee ni busara na ndio maana hata hayo mataifa yanayojigamba kuwa na demokrasia hayajawahi kuthubutu kuwashitaki marais wao wastaafu kwa kuwa wanajua uwezo wa viongozi hao na kazi kubwa waliyoifanya kuliunganisha Taifa na kusonga mbele.

Lakini kwa viongozi wa Afrika ndio hutumika kuwafunga marais wastaafu,kuwadhalilisha  huku wanaowatumia wakinywa mvinyo na kuwaacha wakisambaratisha nchi.

Kabila alikabidhi madaraka kwa amani ili kuiepusha nchi hiyo na machafuko kwa kuwa alikuwa na uwezo mkubwa wa kubakia madarakani kwa kutumia vyombo vya dola ili kuwakomesha wezi wa rasilimali za nchi hiyo na kutoa kipaumbele kwa watoto wa DRC kupata elimu itakayowasidia kuwaamsha kutoka usingizini na kuwa wahandisi wa mitambo na kusimamia rasilimali za nchi hiyo.

Rais Felix Tshisheked ambaye washauri wake wameonekana kumpotosha ili kumkomoa Kabila ameingia katika mtego huo wa chuki bila kutambua kuwa hawezi kufanya mabadiliko kwa haraka wakati amekikuta chama kilichoongoza nchi hiyo kwa zaidi ya miaka 15,hivyo alipaswa  kutoa ushirikiano ili kuwaunganisha wakongo.

Chuki iliyotengenezwa na viongozi wa sasa kwa kizazi cha Kongo haitawaacha salama  na familia zao  baada ya kuingia madarakani kwa Serikali mpya.

Hata hivyo bila kujua sababu zilizomfanya Kabila kutembelea eneo lililoshikiliwa na M23 ,haraka Serikali ya DRC kwa kushirikiana na mataifa yanayomezea mate utajiri wa nchi hiyo walimchukulia hatua kali na kusambaza taarifa za uongo ili aonekane mbaya mbele ya raia wa nchi kwa kile kilichoelezwa kuwa anashirikiana na waasi.

Hata hivyo Kabila hakupewa nafasi ya kujitetea na kueleza sababu za kufika Goma wakati Serikali ya DRC ilisababisha aondoke Kinshasa na kuiaminisha dunia kuwa Rais Mstaafu Kabila ni muasi ili hali wao ndio waliosababisha kuihama nchi yake.-

Makundi ya waasi nchini DRC hayakuanza baada ya utawala wa Kabila bali yalikuwepo miaka mingi ndani ya nchi hiyo ambayo usafiri wa gari kuelekea katika majimbo mengine ni sawa na kujitakia kifo na kuporwa kila kitu ulichonacho.

 

Makundi hayo ya waasi yalikuwepo hasa katika utawala wa Mobutu Sseseseko ambaye alijulikana kama Rais wa Kinshasa kutokana na mifumo yake ya utawala kutotembelea maeneo mengine ya nchi hiyo wala kujenga miundombinu ya barabara,reli,zahanati,maji safi ya kunywa na mengine zaidi ya kujenga katika Jiji la Kinshasa.

Licha ya DRC zamani Zaire kutawaliwa na marais watatu kabla ya Joseph Kabila ilikuwa ikipambana na mifumo iliyowekwa kwa ,makusudi ili kuiba mali za nchi hiyo yenye utajiri mkubwa wa madini adimu duniani.

Wezi wa madini ya nchi hiyo waliweka vikwazo vikali ili raia wa Kongo wasiwaze wala kufikiria madini yao kwa maendeleo ya nchi yao.

Jambo kubwa waliloliweka la kwanza ili waibe vizuri madini ya nchi hiyo ni kuwafanya raia wa Congo kuwa wanamuziki bora barani Afrika na Dunia kwa kuwapamba na mambo mbalimbali ikiwemo baadhi  ya nchi kuwaruhusu kuingia bure bila visa ili kuwasahaulisha kuhusu nchi yao.

Muziki

Wezi hao walihakikisha kuwa wananchi wa Congo vichwa vyao vinajaa muziki na si kitu kingine  ili wasikumbuke utajiri wao ambao ungewasaidia  kuikwamua nchi yao kupitia madini hayo na kuwa na maendeleo  makubwa barani Afrika.

Jeshi la Taifa dhaifu

Utawala wa Rais Joseh Kabila ulitoa fursa kwa askari wa kike kuajiriwa jeshini

Wezi hao pia walihakikisha kuwa Congo haitakiwi kuwa na jeshi bora lenye uwezo na umoja ambapo hilo walifanikiwa pakubwa na kuifanya nchi hiyo kubwa kabisa barani Afrika kubakia kulalamika kwa nchi ndogo kama Rwanda kuwa inawafadhili waasi wa M23 ambao wameteka eneo kubwa zaidi ya nchi ya Burundi hadi sasa.

Muundo wa vikosi vya usalama vya Kongo umeasisiwa kwa umakini mkubwa ili vikosi hivyo visiwe na nguvu wala akili ya kulinda rasilimali za nchi hiyo kwa moyo wa kizalendo ikiwemo kukoseshwa vifaa vya kisasa na malipo duni ambayo huwafanya askari hao kuvunjika moyo wa kujitoa muhanga kwa ajili ya Taifa lao.

Lugha

Wezi hao pia walihakikisha kuwa raia wa Kongo wanagawanywa kwa lugha zao ambapo asilimia kubwa ya raia wa nchi hiyo wanaoishi Kinshasa na maeneo mengine wanaongea lugha ya lingala na kifaransa huku baadhi yao wakiongea Kiswahili hali inayowafanya kushindwa kuwa na umoja.

Kuigawa vipande

Wezi hao walihakikisha nchi hiyo inagawanywa vipande vipande kwa mfumo wa majimbo ambapo viongozi kutoka katika majimbo hayo walikuwa kama marais kutokana na kupewa mamlaka  makubwa ya kiutawala ikiwemo kuwapatia makundi mengi ya raia wa nchi hiyo silaha na kuwafundisha jinsi ya kujilinda na kupigana huku wakiwaonesha kuvuna madini,miti na wanyamapori.

Dini

Wezi hao walihakikisha kuwa baadhi ya madhehebu ya dini yanakuwa wakala wao ili Kiongozi wa nchi akionekana kwenda kinyume na mifumo yao basi wao hujitokeza na wakati mwingine kushiriki hata maandamano ili kumfanya Rais aliyeko madarakani aonekana mbaya kwa kuwa tu ameanza kuvuruga mifumo ya mataifa ambayo wezi hao wameiweka

Hata hivyo viongozi hao wa dini walishindwa kuandamana wakati M23 ilipoanzisha uasi na kuchukua miji ya Goma na Bukavu lakini waliandamana ili kumuondoa madarakani Kabila.

Rais amesomea wapi

Wezi wa madini ya Kongo huangalia Rais anayetawala DRC ana elimu ya nchi za magharibi au kutoka nchi zingine ikiwemo China na Urusi ambapo wao huona kama maslahi yao hayawezi kuangaliwa ikiwa Rais huyo atakuwa anaelimu japo kidogo ya nchi zingine tofauti na nchi zao za magharibi.

Chuki binafsi na kusambaza uongo kupitia vyombo vyao vya habari

Wezi wa madini ya Kongo wamekuwa wakitengeneza mazingira ya kuwaaminisha wananchi wa Kongo na dunia kupitia vyombo vyao vya habari kuwa baadhi ya viongozi wao ni watu wabaya,wezi na wasiofanya mema katika Taifa lao ili kuhalalisha kile wanachokitaka wao kwa kuhakikisha kuwa nchi hiyo inaendelea kuwa na migogoro badala ya kushikamana na kulijenga Taifa hilo.

Mizizi hiyo ambayo imeshindiliwa kwa miongo kadhaa na wezi wa rasilimali za nchi hiyo kabla ya kupata uhuru na baada ya kupata uhuru wake imekuwa vigumu kuiondoa kwa miaka 10 au 15 kutokana na kwamba wahusika bado wapo na wanaendelea kuhakikisha kuwa hakuna kiongozi wa DRC anayekuja kuharibu mifumo hiyo.

Hata hivyo Rais Laurent Desire Kabila baada ya kuonekana anataka kuhakikisha kuwa nchi hiyo inajitawala yenyewe na kufanya maamuzi yake ikiwemo rasilimali za nchi hiyo zinaimarisha uchumi na kuondoa umaskini kwa raia wa Kongo  alitengenezewa waasi ambao walikaribia kuingia jijini Kinshasa kabla ya Kabila kuomba msaada wa kijeshi kutoka baadhi ya nchi za Afrika ikiwemo Angola na Zimbabwe ambao walipekeleka majeshi yao kupambana na waasi hao na kuwashinda.

Hata hivyo licha ya kuwashinda waasi hao Rais Laurent Kabila aliishi muda mfupi na kisha kuuawa kwa kupigwa risasi ili kuzima ndoto za kuwakomboa wakongo kutoka katika mifumo ya unyonyaji ya kuiba rasilimali za asili za nchi hiyo huku wakitumia vyombo vyao vya habari kutangaza mabaya na uongo ili kuhalalisha wanachokitaka.

Baada ya kuuawa kwa Rais Laurent Kabila Ikulu jijini Kinshasa,Rais Mstaafu wa DRC Meja Jenerali Joseph Kabila  aliteuliwa na jopo la makamanda wa kijeshi na viongozi wengine wa kisiasa kushika madaraka ya kuongoza nchi hiyo akiwa na umri mdogo kabisa kuanzia mwaka 2001 hadi 2019 alipokabidhi madaraka kwa amani kwa Rais wa sasa Felix Tshisheked ambaye ni mtoto wa mwanasiasa mkongwe wa nchi hiyo hayati Etiene Tshisheked.

Kabila ambaye alichukua  madaraka siku kadhaa baada ya kifo cha baba yake Hayati Rais Laurent Kabila amefanya mambo makubwa nchini humo lakini wezi wa rasilimali za nchi hiyo walimuona kiongozi mbaya na hafai tena kuongoza nchi hiyo ambapo Taifa hilo lilianza kusimama vizuri kiuchumi na kidiplomasia kwa mataifa mengine duniani.

Rais Mstaafu Kabila akiwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) Hayati Koffi Annan (katikati) na Rais wa Rwanda Paul Kagame katika kusuluhisha migogoro kwa njia za kidiplomasia na sio visasi

Tangu Rais Mstaafu Joseph Kabila achukue madaraka alikuwa akipambana kwa muda mrefu katika kuiunganisha nchi hiyo iliyokumbwa na vita huku ikiwa na jeshi dhaifu lisiloweza kupambana kivita.

Kabila alikuwa na mzigo mkubwa wa kuhakikisha kuwa yeye anakuwa Rais wa nchi nzima ya Congo na hakuwa Rais anayetoa matamko akiwa jijini Kinshasa baada ya kupokea kijiti cha uongozi katika nchi iliyogawanyika.

Hata hivyo Kabila asingeweza kumaliza matatizo ya nchi hiyo kwa miaka 20 pekee bali zaidi ya miaka 40 ili kuweka misingi imara ya kitaifa kutokana na nchi hiyo kugawanywa ili wasiwe na umoja na nguvu ya kukumbuka rasilimali zao.

Kabila ambaye anadaiwa kuishi Tanzania na kusoma  na kuishi katika baadhi ya nchi za Afrika Mashariki ikiwemo Tanzania amekuwa Rais bora wa DRC baada ya Waziri Mkuu wa kwanza wa nchi hiyo Hayati Patrice Lumumba ambaye naye anadaiwa kuuawa na wezi wa madini ya DRC baada ya kuonekana kuwa na mifumo ya kuwaziundua raia wa nchi hiyo dhidi ya wizi wa rasilimali za nchi yao ambazo zimewafanya kubakia masikini na kuwa maarufu kwa mapigano badala ya utulivu huku maiti ya Shujaa wa Taifa hilo ikishindwa kuonekana hadi sasa.

Wezi wa rasilimali huuwa kizazi chote cha wakombozi wa wananchi ili kusiwepo na imani na kumbukumbu zao kwa vizazi vijavyo kama nembo ya umoja na mshikamano.

Ni muhimu kila raia wa kiafrika kutambua kuwa wezi wa rasilimali za mataifa mbalimbali ya kiafrika huwa na tabia ya kuuwa viongozi wa nchi husika na familia zao zote ili kuangamiza kabisa kizazi chao ambacho kinaonekana kama  kitaendeleza ndoto za wazazi wao au ndugu zao kuwakomboa ndugu zao kifikra,kiuchumi na hata kiteknolojia.

Kuumaninisha ulimwengu uongo

Wezi wa rasilimali huuma na kupuliza ambapo kwa wakati mmoja hujifanya kuunga mkono jitihada za Serikali au viongozi waliopo madarakani lakini pindi viongozi hao wanapoanza kuwainua wananchi wao kifikra,kiuchumi na kimaendeleo basi visa huanzia hapo na mwishowe hutafutiwa sababu na kuwauwa wao na vizazi vyao na ikiwemo hata maiti zao kutookena tena ili kusiwepo na ushahidi katika siku zijazo

Meja Jenerali Joseph Kabila

Meja Jenerali Kabila kabla ya kuwa Rais alikuwa mwanajeshi wa nchi hiyo na alishika vyeo mbalimbali katika Jeshi la DRC wakati wa utawala wa hayati Rais Laurent Kabila ambapo yeye akiwa  ni mmoja wa askari aliyepata mafunzo ya kijeshi nchini China.

Kabila alishiriki oparesheni mbalimbali za kijeshi  na kupanda vyeo hadi kuwa Meja Jenerali na kuhudumu kama Mkuu wa kijeshi wa Kambi ya Kivu nchini humo.

Kutokana na uzoefu wa kijeshi,Kabila aliposhika madaraka alianza kubadilisha mifumo iliyozoeleka ya raia wa nchi hiyo wakiwemo wanamuziki wengi wenye fedha kuonesha kutoheshimu mamlaka akiwemo Rais kisa tu fedha walizokuwa nazo.

Meja Jenerali Kabila aliongoza nchi hiyo huku akikumbana na vikwazo kutoka kwa wezi wa rasilimali lakini kutokana na kuishi katika nchi za maziwa makuu,Meja Jenerali Kabila alianza kufanikiwa kutuliza ghasia na makundi mbalimbali ya waasi waliokuwa wakitishia usalama wa nchi hiyo.

Utawala wa Meja Jenerali Kabila ndio utawala pekee uliofanikiwa kupunguza makundi mengi ya waasi kupigana na Serikali ambapo amani ilitawala kwa kiasi kikubwa katika Taifa hilo ambapo wakati mwingine Kabila alitembelea hata vijiji vilivyokuwa na vita kabla ya utawala wake.

Utawala wa Kabila ulisaidia kuwepo kwa umoja wa kitaifa wa wakongo ambao kupitia kazi kubwa aliyoifanya Rais Joseph Kabila raia wa Kongo walianza kuona matunda ya uhuru wao kwa kusafiri na kufanya biashara hata katika maeneo ambayo yalikuwa hayafikiki kutokana na makundi ya waasi.

Alitoa fursa kwa wanawake  

Katika uongozi wa Meja Jenerali Kabila alitoa fursa kwa wanawake wengi kashika nyadhifa mbalimbali katika nchi hiyo kwa kufuata vigezo vya Umoja wa Mataifa  ambapo moja kati ya mashirika ya Serikali ya DRC yaliyoongozwa na wanawake ni Shirika la Utangazaji la DRC ambalo pia alihakikisha kuhakikisha kuwa kituo cha Taifa cha luninga na redio vinasikika vizuri na kuwa na vifaa bora kabisa tofauti na  ilivyokuwa kwa watangulizi wake.

Alijenga miundombinu

Moja ya barabara zilizojengwa enzi ya utawala wa Rais Joseph Kabila

Meja Jenerali Kabila alijitahidi sana katika ujenzi wa barabara ambapo kutokana na ukubwa wa nchi hiyo na hali aliyoikuta asingeweza kumaliza ujenzi kwa kila sehemu lakini alijenga pale ilipowezekana ikiwemo barabara kubwa kabisa ya njia nane inayopita katika Jiji la Kinshasa pamoja na madaraja ambayo sasa yanatumika na wananchi wa nchi hiyo

Aliitangaza DRC kimataifa

Rais Mstaafu Kabila akiwa na aliyekuwa Rais wa Libya Hayati Muamar Gaddaf aliyeuawa baada ya majeshi ya nchi za magharibi (NATO) kuivamia nchi hiyo na kushindwa kutawalika hadi sasa

Meja Jenerali Kabila aliitangaza DRC katika maeneo mbalimbali duniani ikiwemo kukutana na viongozi wengi kutoka mataifa tofauti ambapo alifanikiwa pia kuushawishi Umoja wa Mataifa kupeleka askari wa kulinda amani nchini humo.

Rais Mstaafu Joseph Kabila akiwa na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Dkt.Koffi Annan

Meja Jenerali Kabila alifanikiwa pia kuishawishi Troika iliyoundwa na nchi tatu ikiwemo Tanzania na Afrika Kusini ambapo kikosi hicho cha askari kiliruhusiwa kushambulia waasi moja kwa moja hali iliyofanikisha kuwepo kwa amani mashariki mwa nchi hiyo

Hata hivyo kuwepo kwa kikosi hicho cha Troika kuliwaudhi wezi wa rasilimali za nchi hiyo ambao walizoea kuona vikosi vya askari wa Umoja wa Mataifa ambavyo haviruhusiwi kushambulia waasi  hali iliyowafanya waasi hao kuwa na kiburi kabla ya kudhibitiwa na troika iliyoundwa na askari kutoka nchi tatu ikiwemo Tanzania na Afrika Kusini

Elimu

Rais Kabila akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa shule ya msingi alipowatembelea kujua changamoto zao

Meja Jenerali Kabila alijenga majengo mengi mapya ya shule ili watoto wa DRC wapate elimu bora na sio ya kuishia kucheza muziki huku wakisahaulishwa juu ya rasilimali zao za madini,misitu na maji ambapo katika vyuo vikuu vya nchi hiyo idadi ya wahitimu na wanafunzi iliongozeka kwa kiasi kikubwa hali iliyotoa fursa kwa vijana kujipatia ajira.

Rais Kabila akisalimiana na wanafunzi wa shule ya msingi aliwatembelea kujua changamoto zao

 

Huduma za afya

Meja Jenerali Kabila licha ya kukabiliwa na hali ngumu ya kuiunganisha nchi hiyo iliyogawanywa na wezi wa rasilimaliza za Kongo, amejenga hospitali na zahanati nyingi katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo ili ndugu zake waweze kupata huduma za matibabu kwa urahisi

Utawala wa Kabila umejenga hospitali kubwa Afrika Magharibi ambapo wakandarasi wa Korea Kusini ndio waliojenga hospitali hiyo yenye uwanja wa ndege aina ya helikopta inayoweza kutua moja kwa moja ndani ya eneo hilo la hospitali.

Hospitali hiyo iliyokuwa imepewa jina la Miaka 50 ya Uhuru wa DRC ilikuwa imetoa maelfu ya ajira kwa raia wa nchi hiyo kutokana na ukubwa wake huku ikiwa na uwezo wa kuhifadhi magari ya kubebea wagonjwa makubwa na madogo yanayofikia 15 kwa wakati mmoja.

Meja Jenerali Kabila alihakikisha kuwa wahudumu wa hospitali hiyo ni raia wa DRC ambapo wakati ikiendelea kujengwa makumi ya vijana walipelekwa Korea Kusini kujifunza jinsi ya kutumia mitambo iliyofungwa ndani ya hospitali hiyo huku ikitoa huduma kwa maelfu ya wananchi.

Mitambo ya maji kusambaza maji katika Jiji la Kinshasa enzi za utawala wa Rais Kabila

Kuimarisha Jeshi      

Meja Jenerali Kabila alijitahidi kuimarisha vikosi vya usalama wakiwemo wanajeshi wa Taifa hilo kutokana na kwamba yeye anafahamu mahitaji yao na alikuwa mmoja wa makamanda wa vikosi hivyo, alihakikisha kuwa Mkuu wa Majeshi anapotoa amri kutoka Kinshasa basi agizo hilo linafuatwa na makamanda wote katika nchi hiyo.

Askari wa kike wa DRC enzi za utawala wa Rais Joseph Kabila

Hata hivyo bado alikuwa na kazi kubwa ya kulijenga jeshi kutokana na kuvurugwa kwa mfumo wake huku makundi mengi yakiwa na silaha kabla ya utawala wake lakini wezi wa rasilimali za nchi hiyo humuona hajafanya lolote na kuendelea kueneza chuki na visasi ili waendelee kuiba utajiri wa nchi hiyo.

Aliwaalika waandishi wa habari kutoka mataifa ya Afrika 

Rais  Mstaafu  Kabila anabaki kuwa Rais pekee barani Afrika ambaye alialika waandishi wa habari kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika kufika nchini DRC kujionea maendeleo makubwa aliyoyafanya katika utawala wake.

Wapo waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya utangazi vya Afrika Mashariki lakini pia Afrika Magharini waliofika nchini DRC na kuona amani,upendo na maendeleo yakitawala katika nchi hiyo.

Jambo kubwa walilojifunza waandishi hao lilikuwa ni kutangazwa vibaya kwa nchi hiyo na vyombo vya habari vya kimataifa kuwa ni nchi ya vita ili hali sio kweli.

Enzi za utawala wa Kabila vita ilikuwa sehemu ndogo tena katika mipaka huku juhudi za kuzimaliza zikiendelea.

Aaanza kunyanyaswa

Kabila alianza kuandamwa na Serikali ya DRC mara tu alipokabidhi madaraka kwa amani ambapo hali hiyo ilimlazimisha kuihama nchi yake aliyoipenda na kukabidhi madaraka kwa amani huku akibakia kama Mzee wa kutoa busara kwa vijana.

Apewa zawadi ya kifo na kufilisiwa mali

Katika hali ya kushangaza na kusikitisha,Serikali ya DRC inayoongozwa na Rais  Felix Tshisheked iliamua kumzawadia zawadi ya hukumu ya kifo kwa kile walichodai kuwa anawaunga mkono waasi wa kundi la M23 bila kujali athari zake kwa Taifa.

Kabila alihukumiwa kifo licha ya yeye kuondoka ndani ya Taifa lake kwa zaidi ya miaka sita akiwa ametulia na hajulikani alipo lakini bado aliendelea kuandamwa hadi alipohukumiwa adhabu ya kifo.

Serikali ya DRC ilishindwa hata kukumbuka kauli ya Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Baba Mtakatifu Fransisco aliyeitembelea nchi hiyo na kuiambia dunia kuwa iache kuiba rasilimali za nchi hiyo.

Ujumbe wa Papa ulikuwa jibu tosha la viongozi wa nchi hiyo kuanza ukurasa mpya wa kukaa pamoja na kushirikiana ili kujenga Taifa moja lenye upendo na maelewano na sera thabiti za kuifanya nchi hiyo kuwa imara zaidi duniani.

Hakuna Kiongozi anayeoondoka madarakani bila kuwa na mali

Haitatokea popote duniani kwa Rais aliyekuwa madarakani,Makamu wa Rais,Waziri Mkuu na Spika wa Bunge ambaye ataondoka madarakani bila kuwa na mali kama nyumba na biashara zake zingine kutokana na kwamba mshahara anaoupokea ni mkubwa kuliko viongozi na wananchi wa kawaida.

Viongozi wanapopewa madaraka kutoka kwa warithi wao ni vema mkashirikiana ili kuliendeleza Taifa lenu ambapo chuki na visasi husababisha mgawanyiko wa wananchi na kupelekea kulipizana visasi

Ni lazima jamii itambue kuwa ni muhimu viongozi hao wastaafu kukaa nao meza moja na kuangalia mustakabali wa Taifa lao badala ya kuonesha ubabe ili waonekane wazuri kwa mataifa ya nje yanayotumika kuwachochea

Jambo gani baya amelifanya Kabila hadi ahame nchi yake alikozaliwa

Kabila aliondoka DRC muda mrefu kutokana na chokochoko alizokuwa akifanyiwa na wafuasi wake za kutengeneza mazingira ya kumchafua ili wamkamate na kumfungulia mashitaka hivyo ili kuepusha hayo yote aliamua kuondoka na kuwaachia wajitawale.

Pamoja na Kabila kuondoka na kukaa kimya,bado alishutumiwa sana huku watu wake wa karibu wakinyanysawa na wengine kufungwa gerezani.

Serikali ya DRC yaaachia huru waliohusika na kifo cha Rais wa nchi hiyo Hayati Laurent Kabila

Hata hivyo Serikali ya sasa inaonekana kuwa na chuki kubwa dhidi ya Kabila jambo ambalo lilidhihirika baada ya kuwaachia huru watu waliohusika na kifo cha Rais wa nchi hiyo Laurent Desire Kabila aliyeuawa ndani ya Ikulu ya nchi hiyo.

Kaburi alikozikiwa Hayati Rais Laurent Kabila lililopo Ikulu nchini humo,hata hivyo kutokana na chuki zilizopo linaweza kuwa limeshaondolewa ndani ya eneo hilo la Ikulu

Watu hao waliachiwa huru tena kwa mbwembwe huku makumi ya vyombo vya habari vikiripoti tukio hilo ambapo baadhi ya watu waliojitambua walionesha kushangazwa.

Kuwaachia huru watu waliohusika na mauaji ya Rais ni jambo la kushangaza wakati katika magereza ya nchi hiyo yamejaa raia wenye makosa ya kawaida wakiwemo wanasiasa wanaopaswa kuachiwa huru.

Wakati Serikali ya sasa ikiongoza chuki na visasi dhidi ya viongozi walioongoza na kuleta mafaniko katika nchi hiyo basi watambue kuwa kisasi hicho nacho kitawafikia popote watakapokimbilia ikiwemo kwa hao wanaowasaidia kubakia madarakani.

Serikali ya sasa ya Kongo itambue kuwa Umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu kuwashughulikia viongozi wastaafu sio suluhisho la mgogoro huo bali kuwahusisha zaidi mataifa ya nje ndio kunakoongeza zaidi ,mgogoro huo kwa mataifa hayo kuingiza mamluki na silaha kali ili kuiba vizuri mali za nchi hiyo na kisha kuachiwa mashimo huku nchi zao zikiwa na barabara nzuri,uchumi ukikuwa,amani ikitawala,wakilinda utamaduni wao,wakipata elimu bora,shule na hospitali zikijengwa,vikosi bora vya ulinzi

 Serikali ya DRC msitumie demokrasia kuwaumiza ndugu zenu wa damu

Demokrasia imekuwa ikiwaumiza sana waafrika kuliko walioianzisha hivyo busara na hekima ni muhimu kutumia  kuliko  kuwaumiza ndugu zenu na mtambue kuwa wanaofaidika na migogoro hiyo wako nchini kwao wakiendelea kutoa ajira kwa raia,kuinuka kiuchumi kwa kuzalisha bidhaa na kuuza nje,kuendelea kuwauzi silaha,kuishi kwa amani na starehe,kulinda utamaduni wao na huku wakiwacheka

Ni muda umefika kwa viongozi wa Kongo kuungana kwa pamoja na kushirikiana katika masuala mbalimbali ya kuijenga nchi yenu kwani wezi wa rasilimali zenu hawapendi kuwaona mkiishi kama ndugu,mkiwa na furaha na kuendeleza tamaduni zenu na kuheshimiana.

Rais Tshisheked na Kabila wanaweza kukutana na kuishi   maisha ya umoja na mshikamano kwa maslahi ya Taifa la Congo kwani Kabila alikuwa na uwezo wa kutomkabidhi madaraka Rais Tshisheked na kumpatia mwingine  lakini alifanya kwa upendo  ili DRC iendelee mbele lakini badala yake amepewa adhabu ya kifo na asikanyage tena katika Taifa hilo alilolitumikia kwa zaidi ya miaka 15 jambo ambalo  wezi wa rasilimali walifurahia.

Hawapendi kuona DRC ina rais Mstaafu ambaye busara zake zitatumika kuliongoza Taifa hilo.

Kabila atabakia kuwa mwanasiasa mwenye nvuvu na ushawishi hadi kifo kitakapomkuta kutokana na mema aliyoyafanya kwa raia wa nchi hiyo na majirani zake.

Kabila alitumia sana viongozi wa Afrika katika kushughulikia migogoro ya Taifa hilo bila kusaini mikataba ya kifikicho na mataifa makubwa ikiwemo Marekani  nje ya Taifa hilo.

Mitandao ya kijamii yajaa pongezi kwa Kabila

Katika hali ya kustaajabisha,mitandao mbalimbali ya kijamii inawaonesha wananchi wa DRC wakifurahia Kabila kujiunga na kundi la waasi ambapo wameenda mbali zaidi hadi kumtungia wimbo maalum wakionesha furaha yao na kumkaribisha Kinshasa.

 

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:2
  • Today's page views 2
  • Total visitors 22,590
  • Total page views 25,184

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In