• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Friday, November 20, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Habari

Tamasha la FFC linalowakutanisha maaskofu,mabalozi na viongozi wa Serikali kufanyika Desemba 6,2026

Familia na watoto wakaribishwa kufurahia pamoja

by bajeti
November 20, 2026
in Habari
0
Tamasha la FFC linalowakutanisha maaskofu,mabalozi na viongozi wa Serikali kufanyika Desemba 6,2026

Viongozi wa dini na Serikali wakiwa katika picha ya pamoja na Kwaya ya Flying Family (FFC) wakati wa tamasha la uimbaji lililofanyika katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere Posta jijini Dar es Salaam.

Share on FacebookShare on Twitter

NA MWANDISHI WETU

TAMASHA la Uimbaji linaloandaliwa na Kwaya ya Flying Family (FFC) na kuwatanisha watu wa aina mbalimbali wakiwemo,maaskofu, mabalozi na viongozi wa Serikali linatarajiwa kufanyika  Desemba 6,2026 mkoani Dar es Salaam.

Waimbaji wakitumbuiza kwa kutumia vyombo pekee wakati wa tamasha la FFC jijini Dar es Salaam

Tamasha hilo linalohusisha pia watu wazima na familia zao wakiwemo watoto,ni tamasha la tisa kufanyika nchini likijumuisha waimbaji kutoka madhehebu mbalimbali ya makanisa ya kikristo wenye vipaji vya uimbaji.

Mbali na hilo lakini pia tamasha hilo linakwenda sambamba na kusheherekea sikukuu ya Krismasi ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo zaidi ya miaka 1000 iliyopita  ambayo huadhimishwa kila ifikapo Desemba 25 ya kila mwaka na kuwahusisha mamilioni ya wakristo duniani kote.

Mwenyekiti wa Kwaya ya Flying Family (FFC) ambayo ndio waandaji wa tamasha hilo Innocent Fundisha

Akizungumzia tamasha hilo Novemba 19,2026 jijini Dar es Salaam,Mwenyekiti wa Kwaya ya Flying Family (FFC) ambayo ndio waandaji wa tamasha hilo Innocent Fundisha amesema FFC ni kwaya iliyoanzishwa mwaka 2018 ikijumuisha  waimbaji  kutoka makanisa mbalimbali ya kikristo ikiwa la lengo la kutengeneza umoja wa wakristo kupitia uimbaji.

Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dkt.Alex Malasusa akizungumza wakati wa tamasha la FFC jijini Dar es Salaam

Amesema tangu wakati huo walianza kufanya matamasha mbalimbali ambapo tamasha la kwanza walianza kulifanya mwaka 2018.

“Hili ni tamasha la 11 tangu tulipoanza kufanya tamasha hili na kwaya yetu inajumisha wanakwaya  kutoka madhehebu mbalimbali ya kikristo ambao wanatokea katika maeneo ya Mkoa wa Dar es Salaam,mikoani na baadhi kutoka nje ya nchi ikiwemo Uganda.

“Mwanzo tulikuwa tukifanya mara moja kwa mwaka lakini sasa hivi tunafanya kwa mwaka mara mbili na tumeshafanya katika kumbi za Kardinal Rugambwa,Mlimani City,Mwalimu Nyerere Posta ambapo mwaka huu tutafanyia katika ukumbi wa Skywave hall Msasani Beach.

“Tamasha hili litafanyika Desemba 6,2026 katika ukumbi wa Skywell Msasani Beach kuanzia saa 11.00 jioni na tutakuwa na uimbaji mzuri sana  wa classical music tukichanganya nyimbo nzuri za Krismasi,nyimbo ambazo zimeandikwa kwa umahiri  mkubwa sana wakiwemo watunzi nguli kama kina George Handel,W.Morzat,J.S.Bach,Mendelssohn  na  wengine wengi“amesema Fundisha

Kwaya ya FFC ikitumbuiza wakati wa tamasha

Fundisha ameongeza kuwa hilo ni tamasha kubwa la watu waliojaa vipaji vingi vya mziki ambapo pamoja na muziki,kutakuwepo  na chakula cha jioni pamoja na vinywaji.

Viongozi wa dini wakiwa na Mwenyekiti wa Kwaya ya FFC Innocent Fundisha (wa pili kushoto) kabla ya kuanza kwa tamasha la FFC jijini Dar es Salaam

“Tiketi za tamasha  ni Sh.50,000 kwa watu wazima,30,000 kwa watoto  na V.I.P itakuwa ni Sh.100,000 ambapo ndani ya bei hiyo kutakuwepo na chakula na vinywaji.

“Tunawaalika watu wote kuanzia watoto wadogo,familia na wengine kuja kusheherekea sikukuu ya Krismass  kwani tamasha hili linajumisha watu wote ikiwemo viongozi wa kidini ,viongozi wa Serikali ,mabalozi pamoja na watu wa kada mbalimbali wanakaribishwa kufika na kufurahia kwa kuwa linalofanyika kulingana na utamaduni wa sikukuu ya Krismasi.

“Tamasha hilo pia litakuwa na watumbuizaji wa Saxophone na wengine hivyo tunawakaribisha sana ndugu zetu watanzania tuje tufurahie umoja wetu na kusheherekea Krismass kwa kushiriki na familia zetu”amebainisha Fundisha

Waziri wa zamani wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Prof.Anna Tibaijuka katikatiakifuatilia kwa makini tamasha lililopita

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:20
  • Today's page views 24
  • Total visitors 23,096
  • Total page views 25,733

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In