• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Thursday, April 30, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Mazingira

Waandishi watakiwa kuandika habari za mazingira

by BAJETI
June 5, 2021
in Mazingira
0
Share on FacebookShare on Twitter

Na Mwandishi Wetu,MOROGORO

WAANDISHI wa habari nchini wametakiwa kujikita katika kuandika habari za mazingira ili kuunga mkono jitihada za serikali za kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi kwa faida ya kizazi cha sasa na kijacho.

Wito huo ulitolewa na Mkuu wa  Chuo cha Misitu,Wanyamapori na Utalii katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA)Prof. Suzana Augustino wakati akizungumza na waandishi wa habari za mazingira (JET) mkoani Morogoro juu ya biashara ya kaboni.

Amesema Tanzania ni nchi mwanachama wa Mpango wa Umoja wa Mataifa wa kuthibiti mabadiliko ya tabianchi (UNFCCC) ulioanzishwa mwaka 1992.

Amesema mpango huu unatoa wito kwa nchi wanachama kupunguza Gesi Joto (GHGs) katika anga ambazo ndizo sababu ya mabadiliko ya tabianchi.

“Athari za mabadiliko tabianchi ni pamoja na kuongezeka kwa ukame na mafuriko ya mara kwa mara, uhaba wa chakula na maji, kuenea kwa magonjwa ya kuambukiza kama Malaria na Homa ya Bonde la Ufa (RVF), kuyeyuka kwa seruji kwenye milima mirefu na kwenye ncha za Dunia na vile vile kutoweka kwa visiwa vidogo”amesema Prof.Augustino

Aidha amefafanua kuwa kuna juhudi za kitaifa na kimataifa za kushughulikia mabadiliko ya Tabianchi na  mojawapo ni  ni biashara ya kaboni (hewa ukaa).

Ameongeza kuwa biashara ya kaboni ya misitu ilikuwa inawezekana tu kupitia sera ya maendeleo safi (CDM) ya Itifaki ya Kyoto ya UNFCCC ambapo shughuli za upandaji miti mipya zinaruhusiwa.

“Licha ya kuwa na eneo kubwa la misitu, Tanzania haikupata miradi ya CDM ya kupanda miti chini ya Itifaki ya Kyoto kwa sababu ya ukosefu wa utaalam na teknolojia.”

“Mtu akiona misitu ajue ameona hela na mtu anatunza miti ili kupata fedha  hivyo hii nayo ni fursa ya kuuza Kaboni na ndio maana serikali iliamua kuanzisha pia Kituo cha Kitaifa cha Kufuatilia Kaboni”amesema Prof.Augustino.

Akifafanua kuhusu soko la Kaboni,Mkurugenzi wa Kituo cha Kitaifa cha Kufuatilia Kaboni  (NCMC) Prof.Eliakim Zahabu amesema katika soko huria la Kaboni kuna sehemu mbili ambapo moja  ni makampuni binafsi kuwekeza kwenye kufyonza gesi joto na ya pili ni Nchi inafuata vigezo vya  Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Kudhibiti Mabadiliko  ya Hali ya Hewa  duniani (UNFCC). 

“Ukiona mti umekuwa ujue umehifadhi kiwango kikubwa cha Kaboni na ukichoma misitu basi ujue kaboni inakwenda angani na kwa Tanzania matumizi ya kilimo ndio yameonekana kuzalisha Kaboni kwa wingi kutokana na watu kufyeka misitu na kuchoma moto ili kuandaa mashamba”amesema Prof.Zahabu

Prof.Zahabu amefafanua kuwa Nchi, Mashirika na Watu binafsi wanaweza kuanzisha  shughuli za kupunguza kiwango cha hewa ukaa(Kaboni) kwa kupanda miti mipya.

“Soko rasmi la Kaboni ni kwa kupitia Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Kudhibiti Mabadiliko  ya Hali ya Hewa  duniani (UNFCC)  hususani Sera ya Maendeleo  safi(CDM) ya Protokali  ya Kyoto ambayo inaruhusu shughuli za upandaji wa miti mipya na kwa Tanzania mikoa inayofanya miradi ya Kaboni ni Mbeya,Katavi na Arusha”

“Shughuli zingine kama utunzaji shirikishi wa misitu ya jamii (CFM) nchini unaohusisha misitu asilia ambayo ingetoweka ama kuharibika na kutoa hewa ukaa(Kaboni) inaweza pia kupata malipo kupitia Mpango wa Kupunguza Uzalishaji wa Hewa Ukaa kutokana na ukataji  miti hovyo na uharibifu wa misitu”amesema Prof.Zahabu

Kwa upande wake Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha SUA Dkt.Deo Shirima amesema kila kitu kinachofanyika lazima kichangie asilimia kadhaa ya fedha ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi kwa kuwa hata ukipanda ndege unachangia pia hewa ukaa.

Akizungumza kwa niaba ya waandishi wa habari,Mkurugenzi wa JET John Chikomo amesema JET itaendelea kuhakikisha kuwa wandishi wa habari wanajikita zaidi katika kuandika habari za mazingira ili kusaidia nchi kwa vizazi vya sasa na vijavyo.

“Kulinda mazingira ni suala la kila mmoja wetu hivyo sisi kupitia vyombo vya habari tuna jukumu kubwa la kuhakikisha kuwa mazingira yanalindwa kwa ajili ya sasa na vizazi vinavyo”amesema Chikomo

MWISHO

Next Post

Matumizi ya baiskeli yanahifadhi mazingira

Serikali yaanzisha NCMC kukabiliana na kaboni

The Coronavirus Exposes Education's Digital Generation Gap

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:10
  • Today's page views 11
  • Total visitors 15,995
  • Total page views 18,150

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In