TOKYO,JAPANI
JAPANI inaadhimisha miaka 77 tangu mji wa Nagasaki uliopo nchini humo kushambuliwa kwa bomu la atomiki(nyuklia) wakati wa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia mnamo Agosti 9,1945.
Tangu mapema leo Jumanne asubuhi, watu walikusanyika kuwaenzi waathiriwa wa shambulio hilo katika maeneo mbalimbali ya nch hiyo ikiwemo Bustani ya Amani ya Nagasaki iliyojengwa karibu na kitovu cha shambulio hilo.
Shirika la Habari la nchi hiyo NHK lilieleza kuwa watu wapatao 1,600 walishiriki hafla ya makumbusho ya kila mwaka iliyofanyika katika bustani hiyo.
Kwa mujibu wa NHK watu walionusurika katika shambulio hilo na Waziri Mkuu wa Japani Kishida Fumio walikuwepo, pamoja na wajumbe kutoka mataifa na maeneo 83 kutoka kote duniani.
Faili linalojumuisha majina ya waathiriwa 192,310 iliwekwa ndani ya makumbusho moja ambapo pia inajumuisha majina ya watu 3,160 walioongezwa mwaka mmoja uliopita.
Washiriki walikaa kimya saa 5:02 asubuhi, huu ukiwa muda ambao bomu lilidondoshwa Agosti 9, 1945.
Meya wa Nagasaki Taue Tomihisa alitoa tangazo la amani wakati wa hafla hiyo na kuongeza kuwa na dunia isiyokuwa na silaha za nyuklia
Agosti 9,1945, ndege ya kijeshi ya Marekani ikiwa imejihami kwa silaha zenye nguvu za nyuklia ilidondosha bomu la pili kuwahi kutupwa katika uwanja wa kivita katika mji wa , Nagasaki ambao ulikuwa ndio kitovu cha uzalishaji wa viwanda nchini Japan na kuilazimisha nchi hiyo kusalimu amri siku baada ya tukio hilo ambalo liliangamiza zaidi ya watu 70,000 katika eneo hilo mbali na Hiroshima ambako bomu kama hilo lilidondoshwa.
Hata hivyo inakadiriwa kuwa zaidi ya watu 200,000 walifariki baada ya miji hiyo ya Hiroshima na Nagasaki kushambuliwa na mabomu hayo kwa kuiangamiza kabisa miji hiyo na kuepelea watu wengi kuendelea kufariki kutokana na miale ya mabomu hayo.




Discussion about this post