• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Tuesday, January 13, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Mazingira

Serikali yaanza kutatua mgogoro wa vijiji na hifadhi ya Wembere

by bajeti
December 6, 2022
in Mazingira
0
Serikali yaanza kutatua mgogoro wa vijiji na hifadhi ya Wembere

Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Ujungu Wilaya ya Iramba mkoani Singida wakimsikiliza Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii , Mary Masanja (hayupo pichani) wakati akizungumzia kuhusu Serikali kuunda kamati ya kutatua migogoro ya mipaka katika Hifadhi ya Bonde la Wembere katika mkutano uliofanyika leo Desemba 6,2022.(Picha na Wizara ya Maliasili na Utalii)

Share on FacebookShare on Twitter

NA MWANDISHI WETU,SINGIDA

NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja amesema Serikali itaunda Kamati ya kuangalia migogoro ya mipaka na vijiji vinavyozunguka Msitu wa Hifadhi wa Bonde la Wembere uliopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Iramba mkoani Singida.

Ameyasema hayo leo Desemba 6,2022 wakati alipokuwa akizungumza na wananchi kuhusu mgogoro wa mipaka kwenye eneo la ardhioevu katika Kijiji cha Msai na Ujungu mkoani Singida.

Amesema Kamati hiyo itaishauri Serikali endapo kuna umuhimu wa kurekebisha mipaka na kama eneo hilo litafaa kwa ajili ya shughuli za kibinadamu au la.

“Kuanzia leo tunaunda Kamati ambayo itajumuisha wataalam kutoka ngazi ya Wizara,Mkoa na Wilaya na zoezi hilo litaanza mara moja na itapitia mipaka kwa kushirikiana na wananchi ili kuainisha mipaka halisi kwa kuzingatia ramani iliyopo ili kumaliza mgogoro huo”amesema Masanja.

Hata hivyo Masanja amewataka wananchi hao kuzingatia sheria za kutovamia maeneo ya hifadhi na kuwa walinzi wa eneo hilo mara tathmini itakapokamilika.

Kuhusu changamoto ya wafugaji wanaopitisha ng’ombe katikati ya hifadhi kwa ajili ya kupeleka mifugo yao kunywa maji amesema, Serikali itaangalia namna iliyo bora ya kutatua changamoto hiyo ili wananchi wasiingiliane na masuala ya uhifadhi.

Hata hivyo Msanja amewataka wananchi kuacha tabia ya kukata miti hovyo na kukubaliana na mradi wa upandaji miti ulioletwa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kwa lengo la kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi.

Naye, Mbunge wa Iramba Magharibi ambaye pia ni Waziri wa Fedha na Mipango,Dkt. Mwigulu Nchemba amewataka viongozi wa Kata na vijiji kushirikiana na Kamati iliyoundwa wakati wa kupitia upya usahihi wa vigingi zilizowekwa.

Next Post

DODOMA

Zanzibar

Zanzibar

DODOMA

DODOMA

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:1
  • Today's page views 1
  • Total visitors 13,057
  • Total page views 14,802

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In