• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Tuesday, January 13, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Mazingira

Wafanyabishara ya Kaboni watakiwa kusajili miradi yao

by bajeti
December 16, 2022
in Mazingira
0
Wafanyabishara ya Kaboni watakiwa kusajili miradi yao

Waziri wa Nchi Ofisi ya makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dkt. Selemani Jafo akizungumza na waandishi wa habari pamoja na sehemu ya Menejimenti ya Ofisi hiyo wakati akitoa taarifa ya uzingatiaji na utekelezaji wa Kanuni na Mwongozo wa Biashara ya Kaboni Desemba 16, 2022 jijini Dodoma.(Pcha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Share on FacebookShare on Twitter

NA MWANDISHI WETU,DODOMA

SERIKALI imewataka wadau wa biashara ya kaboni wahuishe miradi yao na kujisajili upya kupitia ili iendane na matakwa ya Kanuni na Mwongozo wa masuala hayo.

Wafanyabiashara hao wametakiwa kujisali upya kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais na Kituo cha Kitaifa cha Ufuatiliaji wa Kaboni (NCMC)kilichopo Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA),kilichopo mkoani  Morogoro

Kauli hiyo imetolewa Desemba 16,2022 jijini Dodoma na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dkt. Selemani Jafo wakati akitoa taarifa ya uzingatiaji na utekelezaji wa Kanuni na Mwongozo wa Biashara ya Kaboni.

Amesema uzingatiaji na utekelezaji wa kanuni na mwongozo huo utasaidia kuboresha usimamizi mzuri wa miradi ya biashara ya kaboni inayotekelezwa ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika sekta zote.

Ameongeza kuwa utekelezaji wa biashara ya kaboni utachangia kupunguza gesijoto zinazosababisha ongezeko la joto duniani na hatimae kupunguza athari za mabadiliko ya tabianchi, kuchangia katika utunzaji endelevu wa mazingira na kuleta maendeleo endelevu ya kijamii na kiuchumi.

Waziri Jafo amesisitiza kuwa uzingatiaji na utekelezaji wa Kanuni na Mwongozo wa Usimamizi wa Biashara ya Kaboni ni jukumu la wadau wote, ikiwemo Wawekezaji wa Kimataifa na wanaotoka ndani ya nchi, Wizara za Kisekta, Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa.

“Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazoathiriwa na athari za mabadiliko ya tabianchi na hali ya hewa isiyotabirika na hali hii inajidhihirisha kupitia matukio ya mvua zisizotabirika, ongezeko la joto, ukame na mafuriko.

“Athari hizi za mabadiliko ya tabianchi zimeathiri sekta za kijamii na kiuchumi na maendeleo kama vile kilimo, utalii, nishati, maji, afya, mifugo na mifumo ikolojia ya bahari na ardhi, hivyo kuathiri ongezeko la pato la taifa.

“Aidha, ukame wa muda mrefu na mafuriko yamechangia gharama kubwa za kiuchumi, kuathiri maendeleo na maisha ya jamii za vijijini na mijini,” amebainisha Dkt. Jafo.

Aidha, amefafanua kuwa kanuni na mwongozo huo vimejikita katika kuimarisha mchango wa nchi katika jitihada za kupunguza uzalishaji wa gesijoto na hivyo kupunguza athari za mazingira.

Ameongeza kuwa kanuni hizo zinalenga kuhakikisha kuwa jamii, wadau mbalimbali wanaohusika na biashara hiyo ikiwa pamoja na Serikali kunufaika kikamilifu kutokana na faida zilizopo katika biashara ya kaboni nchini.

Kutokana na hatua hiyo alielekeza Idara ya Mazingira, Kituo cha Ufuatiliaji wa Kaboni na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) katika Kanda zote kwa kushirikiana na Wizara za Kisekta, Sekretariati za Mikoa, Mamlaka za Serikali za Mitaa na wadau wa maendeleo kusimamia kwa ufanisi utekelezaji wa Kanuni na Mwongozo wa Usimamizi wa Biashara za Kaboni.

Next Post
PWANI

PWANI

Masanja:TAWA fanyeni kazi kwa ushirikiano kufikia malengo

Masanja:TAWA fanyeni kazi kwa ushirikiano kufikia malengo

NEPAL

NEPAL

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:6
  • Today's page views 6
  • Total visitors 13,062
  • Total page views 14,807

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In