NA MWANDISHI WETU,ZANZIBAR
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar kimesema hakitowavumilia baadhi ya watu wanaokwepa kulipa kodi kwa makusudi na kuisababishia hasara serikali. “
Kimesema CCM ikiwa ndio msimamizi mkuu wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020/2025 lazima ikemee vikali baadhi ya tabia ya ukwepaji wa kodi kwa baadhi ya wafanyabishara na wawekezaji.
Hata hivyo chama hicho kimezitaka taasisi zinazohusika na usimamizi wa masuala ya kodi nchini zikiwemo Mamlaka ya Mapato Zanzibar(ZRA),na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) zu=ikiwemo manispaa pamoja na vyombo vya ulinzi na usalama kuhakikisha wanachukua hatua kali kwa yeyote anayehusika na vitendo hivyo bila kujali cheo,dini,kabila na itikadi ya kisiasa.
Kauli hiyo imetolewa na Februari 24,2023 na Katibu wa Kamati Maalum ya NEC,Idara ya Itikadi na Uenezi CCM Zanzibar Khamis Mbeto Khamis wakati wa mahojiano maalum katika Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Jijini Zanzibar.
Amesema kila mwananchi ana jukumu la kupinga vitendo vya ukwepaji wa kodi kwani ni hujuma,usaliti na jinai katika maendeleo na ustawi wa uchumi wa nchi.
Khamis, ameeleza kuwa madhara ya vitendo hivyo ni makubwa kwani yanaikosesha serikakali fedha nyingi ambazo zingetumika katika kutatua kero na changamoto za wananchi.
“ CCM ikiwa ndio msimamizi mkuu wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020/2025 lazima tukemee vikali baadhi ya tabia ya ukwepaji wa kodi kwa baadhi ya wafanyabishara na wawekezaji.
“Fedha hizi zingetumika kujenga hospitali,maskuli,maji safi na salama na huduma za barabara za kiwango cha lami na huduma zingine muhimu za kijamii.”Khamis.
Aidha ameongeza kuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi, anafanya kazi kubwa ya kuleta maendeleo endelevu lakini kuna baadhi ya watu wachache wanakwamisha juhudi hizo kupitia vitendo vya ukwepaji wa kodi.
Khamis amewaleza wafanyabishara nchini kuwa hakuna haki bila wajibu hivyo ukusanyaji wa kodi ni lazima, kwani ikilipwa wanaijengea serikali uwezo wa kutoa huduma stahiki kwa wananchi.
“Serikali zote mbili ya Zanzibar nay a Jamhuri ya muungano wa Tanzania zimetoa fursa kwa wananchi kufuata taratibu za kisheria pale wanapoamua kufanya biashara.
“Ibara ya 47 hadi 49 za Ilani ya CCM ya mwaka 2020/2025 imeeleza kuwa CCM inatambua kuwa biashara ni kichocheo cha maendeleo ya viwanda na sekta nyingine za kijamii”amesema Khamis
Katika hatua nyingine Khamis ametoa wito kwa wananchi kuepuka kujihusisha na vitendo vya uhalifu wa kukwepa kulipa kodi na kuwataka kuendelea kuwa wazalendo,wachapakazi na waadilifu.




Discussion about this post