• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Tuesday, January 13, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Mazingira

Mtanzania agundua mashine kuvunia sumu ya nyuki

by bajeti
March 11, 2023
in Mazingira
0
Mtanzania agundua mashine  kuvunia sumu ya nyuki

Mratibu wa Mafunzo ya Uandishi wa Habari za Sayansi,Teknolojia na Ubunifu kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi,Teknolojia(COSTECH)Deusdeth Leonaed akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari na watafiti juu ya umuhimu wa kuandika taarifa za Sayansi,,Tekonolojia na Ubunifu Machi 7,2023 jijini Dar es Salaam.(Picha na Goodluck Hongo)

Share on FacebookShare on Twitter

NA GOODLUCK HONGO

SERIKALI kupitia Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) imeendelea kuwaibua wabunifu wa teknolojia mbalimbali nchini ambapo sasa imemsaidia Mtanzania Patrick Kitosi kuendeleza mashine aliyoibuni kuvunia sumu ya nyuki.

Hata hivyo mbunifu huyo amebainisha kuwa sumu ya nyuki mara nyingi inatumika katika matibabu ya magonjwa mbalimbali lakini ilikuwa vigumu kuivuna bila kuwaathiri nyuki na shughuli zao za kila siku katika uzalishaji wa asali na kulinda mazingira.

Akizungumza jijini Dar es Salaam Machi 8,2023 wakati wa Mafunzo ya Uandishi wa Habari za Sayansi,Teknolojia na Ubunifu kati ya waandishi wa Habari na Watafiti yaliyoandaliwa na COSTECH,Kitosi amesema alianza kufanya utafiti wa mashine hiyo mwaka 2017 na kufanya majaribio 16 kabla ya kufanikiwa kuwa na mashine ambayo huvuna sumu ya nyuki bila kuwaathiri.

Amesema   nyuki wapo wa aina tofauti kulingana na mazingira na nchi wanakotoka yakiwemo ya joto na baridi hivyo teknolojia ya mashine yake lazima izingatie hali hiyo ili wasiweze kudhurika ikiwemo kuuawa na kukatika mikia wakati zoezi la uvunaji wa sumu hiyo ukifanyika .

“Ili nyuki atoe sumu lazima akasirike ambapo katika mkia wake anaotumia kung’ata unakuwa na majimaji ambayo ndio sumu yenyewe,sasa sisi mashine yetu tumetumia  teknolojia ya eletroniki na umeme hivyo nyuki anapotua hupigwa shoti na hapo ndipo hukasirikika na kutoa sumu.

“Wakati anatoa sumu hiyo mkia wake hubakia bila kukatika tofauti aking’ata kawaida ambapo mkia wake hukatika,mashine pia inakuwa na kioo baada ya nyuki kung’ata waya zilizowapiga shoti ndipo majimaji hayo yenye sumu hudondoka kwenye kioo  kwa uzito wa 0.6 gram kwa kutegemea na kundi la nyuki  na  huchukua dakika 30 kuvuna sumu hiyo “amesema Kitosi

Kitosi ameishukuru COSTECH kwa kuhakikisha kuwa ubunifu wake unaendelea kusaidia wafugaji wa nyuki bila kuathiri mazingira yao ambapo hadi sasa ameshauza mashine 107 nchini huku kila moja ikiwa na thamani ya Sh.750,000 ambapo mashine  kama hiyo kutoka nje ya nchi inagharimu zaidi ya Sh.Milioni mbili.

“Licha ya Nyuki kutoa asali lakini pia sumu yake inauzwa bei ghali sana nje ya nchi lakini pia hutoa Nta na Maziwa na hiyo inatokana na vitu vyote wanavyovizalisha hutokana na mimea.

“Nyuki wanaakili sana lazima utafiti wa kina ufanyike ili kugundua mashine hiyo lakini changamato kubwa iliyopo ni wafugaji kutojua sumu ya nyuki kama inaweza kuuzwa na jinsi ya kuivuna ikiwemo  uhaba wa mashine hizo za kuvunia”amebainisha Kitosi

Hata hivyo Kitosi ameongeza kuwa ubunifu wa mashine hiyo utasaidia katika upatikanaji wa madawa ya kutibu magonjwa mbalimbali na kupunguza gharama za matibabu.

Awali  Mkurugenzi wa Menejimenti ya Maarifa kutoka COSTECH Mhandisi Samson Mwela amesema mtu yeyote mwenye bunifu yake anakaribishwa kuzipeleka COSTECH ili ziweze kuendelezwa na kutatua changamoto kwa jamii.

“Kazi ya Serikali ni kuweka mazingira mazuri ya Sayansi,Teknolojia katika kutatua changamoto zinazowakabili wananchi na kuleta maendeleo kwa Taifa letu”amesema Mhandishi Mwela

Next Post
Miche 500,000 ya Mkonge kuzalishwa kwa njia ya chupa

Miche 500,000 ya Mkonge kuzalishwa kwa njia ya chupa

Spika Dkt.Tulia aieleza IPU juhudi za serikali katika kudumisha amani

Spika Dkt.Tulia aieleza IPU juhudi za serikali katika kudumisha amani

Kamati ya Bunge

Kamati ya Bunge

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:1
  • Today's page views 1
  • Total visitors 13,057
  • Total page views 14,802

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In