• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Thursday, January 22, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Habari

Mwanamfalme Harry wa Uingereza apokonywa nyumba baada ya kuikosoa familia yake

by bajeti
July 1, 2023
in Habari
0
Mwanamfalme Harry wa Uingereza apokonywa  nyumba baada ya  kuikosoa familia yake

Mwanamfalme Harry wa Uingereza

Share on FacebookShare on Twitter

LONDON,UINGEREZA

DEMOKRASIA  haivunjwi na nchi za kiafrika pekee kama ilivyozoeleka bali hata nchi zinazodai kufuata uhuru wa kutoa maoni ambazo huchukua hatua baada ya kukosolewa hadharani.

Hivyo ndivyo unavyoweza kusema baada ya Maafisa wa Jumba la Familia ya Mfalme wa Uingereza (Kasri la Buckingham), kutangaza kuwa Mwanamfalme Harry na mkewe Meghan hatimaye wamehama nyumba waliokuwa wakiishi kwenye kasri ya familia ya kifalme ya Windsor, iliyoko magharibi mwa London  baada ya kutakiwa kufanya hivyo.

Kunyan’ganywa nyumba hiyo kunawafanya wanandoa hao kutokuwa na makazi ya kudumu nchini Uingereza walikozaliwa.

Kwa mujibu wa taarifa ya Sauti ya America (VOA) ya Juni 29,2023 ilieleza kuwa nyumba hiyo, inayofahamika kama Frogmore Cottage, ilikuwa zawadi ya harusi waliyopewa wanandoa hao na bibi yake Harry, marehemu Malkia Elizabeth II, mwaka 2018.

Lakini ililiripotiwa walitakiwa kuondoa vitu vyao vyote vilivosalia siku chache baada ya Harry, mtoto wa mwisho wa Mfalme Charles III, kuanza kuikosoa vikali familia yake katika kitabu chake cha kumbukumbu chenye utata cha “Spare” mwezi Januari 2023.

“Tunaweza kuthibitisha kwamba Duke na Duchess wa Sussex wameondoka Frogmore Cottage,” Afisa Mkuu wa kasri hilo Michael Stevens alisema kama ripoti ya kila mwaka ya fedha ya kifalme ilichapishwa Alhamisi.

“Hatutaelezea kwa undani kuhusu mipango iliyopo,” alisema Stevens, ambaye ni mweka hazina wa mfalme.

Aliongeza kusema kuwa wanandoa hao ambao kwa sasa wanaishi California nchini Marekani wameshalipa Pauni Milioni 2.4 ambazo ni kodi na gharama za kukarabati kasri hiyo, ambayo ni mali ya mfalme.

Hata hivyo kitendo hicho kinaonesha ni jinsi gani matendo kama hayo hayako katika nchi za kiafrika pekee bali hata katika nchi zinazoonesha kuwa na demokrasia iliyokomaa ambapo mara nyingi viongozi wake hawapendi kuambiwa ukweli juu ya makosa yao.

 

Prince Harry aliwahi kuiambia kituo cha habari cha  ITV kuwa mengi ya mambo ambayo yanachapishwa katika magazeti ya udaku siyo ya kweli, akiongeza kuwa hatakubali kuingizwa katika hujuma iliyomuua mama yake.”

Harry amesema kumbukumbu ya kifo cha Princess Diana ilikuwa bado ingaliipo kila siku kunavyokucha.

Next Post
Shoroba zifunguliwe kupunguza athari za  wanyamapori wakali na waharibifu

Shoroba zifunguliwe kupunguza athari za wanyamapori wakali na waharibifu

Dkt.Mpango aitaka JKT kuwekeza matumizi ya teknolojia

Dkt.Mpango aitaka JKT kuwekeza matumizi ya teknolojia

Waziri Mkuu wa India Narendra Modi ndani ya usafiri wa umma

Waziri Mkuu wa India Narendra Modi ndani ya usafiri wa umma

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:18
  • Today's page views 18
  • Total visitors 13,277
  • Total page views 15,025

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In