• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Thursday, January 22, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Habari

Dkt.Mpango ataka Chuo cha Ulinzi cha Taifa (NDC) kuvutia washiriki kutoka mataifa mengine

Pia kuwa kitovu cha elimu ya usalama na masomo ya kimkakati kikanda

by bajeti
July 29, 2023
in Habari
0
Dkt.Mpango ataka Chuo cha Ulinzi cha Taifa (NDC) kuvutia washiriki kutoka mataifa mengine

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwa ameongozana na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob Mkunda (Kulia) pamoja na Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi Meja Jenerali Ibrahim Mhona (kushoto) wakati alipowasili kushiriki Mahafali ya Kozi ya 11 ya Chuo cha Taifa cha Ulinzi (NDC) yaliofanyika katika chuo hicho kilichopo Kunduchi Jijini Dar es salaam Julai 29,2023.(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Share on FacebookShare on Twitter

NA MWADISHI WETU

MAKAMU  wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango ametoa wito kwa Mkuu wa Chuo cha Ulinzi cha Taifa (NDC) pamoja na wahusika wengine kuweka mkakati wa kuvutia washiriki wengi zaidi kutoka mataifa mengine kusoma katika chuo hicho.

Makamu wa Rais ametoa wito huo wakati wa Mahafali ya Kozi ya 11 ya Chuo cha Ulinzi cha Taifa (NDC) yaliofanyika katika viwanja vya chuo hicho kilichopo Kunduchi Jijini Dar es salaam.

Amesema kwa kufanya hivyo kutaongeza wigo wa mwingiliano, kubadilishana uzoefu na kujifunza ikijumuisha uwezekano wa kubadilishana wafanyakazi kutoka vyuo vingine vya Ulinzi vya Kitaifa pamoja na Taasisi katika mafunzo maalum.

Aidha  ameongeza kuwa  uandikishaji wa idadi kubwa ya washiriki wa kozi hizo wenye uwezo mkubwa wa uongozi kutoka nchi nyingine utachangia katika kukuza viongozi rafiki wa Tanzania wa Nchi za nje.

Amebainisha kuwa wahitimu hao wa Chuo cha Ulinzi cha Taifa wana nafasi kubwa ya kuwa Mabalozi wa kipekee wa Tanzania katika masuala ya utalii, utamaduni, lugha ya Kiswahili na rekodi ya nchi ya kudumisha amani na utulivu wa kijamii na kisiasa tangu uhuru mwaka 1961 na kwamba NDC inapaswa kuwa kitovu cha elimu ya usalama na masomo ya kimkakati ya kikanda.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akihutubia Viongozi mbalimbali, Wakufunzi pamoja na Wahitimu (hawapo pichani) wakati wa Mahafali ya Kozi ya 11 ya Chuo cha Taifa cha Ulinzi (NDC) yaliofanyika katika chuo hicho kilichopo Kunduchi Jijini Dar es salaam Julai 29, 2023.(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Halikadhalika Makamu wa Rais amesema kwa lengo la mwendelezo na maendeleo ya Chuo cha Taifa cha Ulinzi upo umuhimu wa kuwatumia wahitimu wa chuo hicho.

“Kupitia uzoefu wa kimataifa inaonesha kwamba wanachuo huongeza thamani kubwa kwa Vyuo wanavyohitimu kwa kutoa ushuhuda wenye nguvu kwa niaba ya chuo na hivyo kufanya chuo kujulikana na kuvutia wengine”amesema Dkt.Mpango

Makamu wa Rais ametoa wito kwa Wahitimu wa Kozi ya 11 ya Chuo cha Taifa cha Ulinzi na wahitimu waliopita awali, kuchukua jukumu la kuendelea kukitumikia chuo kwa uaminifu popote watakapokuwa kwa maendeleo bora ya chuo hicho na kukitaka  NDC  kufanya utafiti wa kufuatilia maendeleo ya wahitimu popote pale wanapopangiwa hasa kuzingatia matokeo yao kulingana na elimu waliyoipata kupitia mafunzo chuoni hapo.

Hata hivyo Dkt.Mpango amebainisha kuwa bado idadi ya wanawake wanaopata mafunzo katika chuo hicho ni ndogo hivyo amemuagiza Katibu Mkuu Kiongozi kupitia kwa Makatibu Wakuu wa Wizara kuwahamasisha wanawake kujiunga na kozi mbalimbali zinazotolewa chuoni hapo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akiwa katika picha ya pamoja na Wahitimu mara baada ya kumalizika kwa Mahafali ya Kozi ya 11 ya Chuo cha Taifa cha Ulinzi (NDC) yaliofanyika katika chuo hicho kilichopo Kunduchi Jijini Dar es salaam leo tarehe 29 Julai 2023. (Wengine katika picha ni Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha NDC Balozi Moses Kusiluka, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Stergomena Tax, Mkuu wa Chuo cha NDC Meja Jenerali Ibrahim Mhona, Kansela wa Chuo cha NDC Dkt. Abdulhamid Mzee, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob Mkunda na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Faraj Mnyepe(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi (NDC) Meja Jenerali Ibrahim Mhona amesema Chuo hicho kinawaandaa wahitimu namna mpya ya kufikiri na kukabiliana na changamoto za kiusalama zaidi kwa kutumia akili kuliko silaha.

Amesema changamoto za kiusalama na matishio mbalimbali katika nchi, Bara la Afrika na duniani kwa ujumla yanatihaji kufikiri kwa kina na kuwa na maamuzi sahihi kwa kutoa suluhu zitazodumu kwa muda mrefu.

Meja Jenerali Mhina ameongeza kwamba mafunzo hayo yanatoa fursa kwa washiriki kukutana na viongozi wa juu kutoka serikalni, sekta binafsi na wataalamu mbalimbali ili kuelewa masuala ya kisiasa, kijamii na mikakati katika nchi husika.

Amefafanua kuwa NDC inahakikisha wahithimu wanafikiri vizuri na kufikiri nje ya mipaka ili kupata suluhu za muda mrefu katika matatizo yanayojitokeza na yale yasiotarajiwa kwa wakati huo.

Katika mahafali hayo washiriki saba (7) wamefanikiwa kufuzu Stashahada ya Usalama na Stratejia huku jumla ya washiriki 33 wakifanikiwa kufuzu Shahada ya Uzamili ya Usalama na Stratejia.

Next Post
TBA yatakiwa kujenga nyumba zenye ubora na kukidhi mahitaji ya soko

TBA yatakiwa kujenga nyumba zenye ubora na kukidhi mahitaji ya soko

Tutunze mazingira

Tutunze mazingira

RC Mtaka ataka kutangazwa zaidi fursa biashara ya Kaboni

RC Mtaka ataka kutangazwa zaidi fursa biashara ya Kaboni

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:18
  • Today's page views 18
  • Total visitors 13,277
  • Total page views 15,025

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In