• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Thursday, January 22, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Habari

Soko la Samaki Feri laelemewa na wafanyabishara

Lina uwezo wa kuhudumia wafanyabiashara 1500 lakini sasa wamefikia 300

by bajeti
September 24, 2023
in Habari
0
Soko la Samaki Feri laelemewa na wafanyabishara

Wafanyabishara katika Soko la Samaki la Kimataifa Feri lililopo Kivukoni jijini Dar es Salaam wakiendelea na shughuli zao kama walivyokutwa na mpigapicha wetu Septemba 22,2023.

Share on FacebookShare on Twitter

NA M,WANDISHI WETU

SOKO la Kimataifa la Samaki la Feri lililopo Kivukoni jijini Dar es Salaam linakabiliwa na changamoto ya ongezeko la idadi kubwa ya wafanyabiashara zaidi ya 3000 huku uwezo wake halisi ni kuwa na uwezo wa kuhudumia  1500.

Kuongezeka kwa wafanyabiashara hao kunachangia kuharibika kwa miundombinu ya soko hilo mara kwa mara huku Serikali ikiendelea kutatua kero hizo ikiwemo kulifanyia ukarabati.

Akizungumza katika mahojiano maalum mwishoni mwa wiki hii jijini Dar es Salaam ,Meneja wa soko hilo Seleman Mfinanga amesema mpango wa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan ni kuondoa adha inayojitokeza kwenye masoko hali inayofanya uongozi wa soko hilo kuwa na mikakati mizuri ya kuhakikisha wafanyabiashara hao wananufaika katika kujiingizia kipato  lakini serikali nayo inanufaika na kodi katika kufanya shughuli za kimaendeleo.

Amesema licha ya kuwepo kwa idadi kubwa ya wafanyabishara lakini wanaendelea kujitahidi kuhakikisha suala la usafi wa soko unafanyika ipasavyo ili kuzuia magonjwa ya mlipuko ambapo  taka za maeneo hayo zimekuwa zikiondolewa kwa wakati.

“Soko linakabiliwa na changamoto ya ongezeko la idadi kubwa ya wafanyabiashara zaidi ya 3000 huku uwezo wake halisi ni kuwa na uwezo wa kuhudumia  wafanyabishara 1500”amesema Mfinanga

Mfinanga amebainisha  kuwa Zoni namba mbili,tatu,nne tano,sita na saba zipo katika kuguswa na ukarabati ambapo ukikamilika hatua hiyo itaweza kupunguza kero kwa asilimia 50  au kumaliza kabisa kero zilizokuwa zikilalamikiwa na wafanyabiashara.

Hata hivyo Mfinanga  ameahidi kufanyia kazi changamoto endapo zitaendelea kujitokeza  huku akiwataka Wafanyabiashara wa soko hilo kuendelea kufanya kazi kwa bidii na kutambua kuwa Serikali ipo nyuma yao na inahakikisha inawatengenezea mazingira mazuri yakufanyia biashara.

Next Post
Elimu kwa wanafunzi

Elimu kwa wanafunzi

Kutunza mazingira

Kutunza mazingira

Tunapokea ndege yetu Boeing 737- MAX9

Tunapokea ndege yetu Boeing 737- MAX9

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:18
  • Today's page views 18
  • Total visitors 13,277
  • Total page views 15,025

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In