NA MWANDISHI WETU
KAMPUNI ya Google kutoka nchini Marekani kwa mara nyingine tena imetambua mchango unaotolewa na tovuti ya habari ya BAJETI.CO.TZ baada ya kuitunuku vyeti vingine viwili vya pongezi kutokana na maelfu ya watu kutoka pembe mbalimbali za dunia kuifuatilia bila kupewa kiunganisho(link) kupata taarifa zake .
Bajeti.co.tz inayochapisha taarifa zake kutoka jijini Dar es Salam nchini Tanzania-Afrika Mashariki imekuwa ikifuatiliwa na maelfu ya watu kutoka pembe mbalimbali za dunia kutokana na usahihi wa taarifa zake za upekee
Akizungumzia jijini Dar es Salaam Desemba 2,2023 mara baada ya kupokea vyeti hivyo,Mkurugenzi wa Bajeti Communication inayoendesha tovuti hiyo, Goodluck Hongo ameelezea pongezi hizo za Google kuwa ni jambo la furaha kuona Kampuni kubwa duniani kama Google kuitunuku vyeti vingine viwili vya hongera tovuti yao ya BAJETI.CO.TZ kwa kuvuka viwango ilivyowekwa na Google.
“Duniani kuna maelfu kwa mamilioni ya tovuti zinazochapisha taarifa mbalimbali lakini ni kitu cha furaha kuona na sisi tumetambuliwa na Google kuwa ni miongoni mwa tovuti za habari maarufu duniani na kuona umuhimu wa kututunuku vyeti ambavyo kwa viwango vyao wameona kuwa tunastahili ”amesema Hongo
Hata hivyo Hongo ameongeza kuwa wao huchapisha taarifa zao kwa lugha ya Kiswahili nab ado hawajaweka mfumo wa lugha mbili lakini cha vyeti hivyo vinaonesha kuwa lugha ya Kiswahili inajulikana duniani kote hata kama hujaweka mfumo wa lugha nyingine watu kusoma taarifa zilizochapishwa
“Tutatendelea kuandika taarifa sahihi na zenye vyanzo sahihi kwa kufuata Sheria,Kanuni na Miongozi mbalimbali zinazohusu uchapishaji wa taarifa kama chombo cha habari na tunawaomba pia wadau wetu wanaotufuatilia waendelee kufanya hivyo”amesema Hongo

Bajeti.co.tz ni tovuti ya habari inayoendeshwa na Bajeti Communication yenye Makao Makuu jijini Dar es Salaam nchini Tanzania,Afrika Mashariki ambayo hutoa taarifa zake kwa lugha ya Kiswahili.
Vyeti hivyo vinafikisha idadi ya vyeti vitatu vya Google kuipongeza tovuti hiyo ambapo mara ya mwisho ilipokea mnamo mwezi Juni mwaka huu wa 2023.




Discussion about this post