• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Tuesday, January 13, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Mazingira

Tanzania yaanzisha Shahada ya Hali ya Hewa na Mabadiliko ya Tabianchi

by bajeti
December 4, 2023
in Mazingira
0
Tanzania yaanzisha Shahada ya Hali ya Hewa na Mabadiliko ya Tabianchi

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dkt. Selemani Jafo (kushoto) akishiriki Mkutano wa Jukwaa la Mawaziri la Majadiliano ya Juu la Utekelezaji wa Tahadhari ya Mapema kwa Wote katika Mpango Kazi wa Afrika lililofanyika katika banda la Kenya pembeni ya Mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP28) Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu.(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Share on FacebookShare on Twitter

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dkt. Selemani Jafo amesema imeanzishwa Shahada katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM)kuhusu masuala ya Hali ya Hewa na Mabadiliko ya Tabianchi, kusaidia kuimarisha maendeleo ya rasilimali watu nchini hasa kwa wafanyakazi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA).

Jaffo ameyasema hayo wakati akizungumza kwenye Jukwaa la Mawaziri la Majadiliano ya Juu la Utekelezaji wa Tahadhari ya Mapema kwa Wote katika Mpango Kazi wa Afrika lililofanyika pembeni ya Mkutano wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP28) Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu.

Amesema kuwa Serikali ya Tanzania ilitunga Sheria ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania Na. 2 ya mwaka 2019, inayotoa maelekezo na kuimarisha mamlaka ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania kutoa Huduma za Tahadhari za Mapema.

Ameongeza kuwa Serikali pia ilikuja na Mifumo ya Kitaifa ya Huduma za Hali ya Hewa (NFCS), ambayo ilizinduliwa Agosti 2018 sanjari na kufunga rada saba za hali ya hewa na tatu za hali ya Hewa tayari zimeanza kufanya kazi.

Kutokana na taarifa za hali ya hewa kutoka TMA, amesema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu na Wizara na Wadau wote wenye dhamana iliandaa Mpango wa Taifa wa Dharura wa El Nino na hatua ya matarajio Agosti, 2023 ambao umechangia kupunguza athari za mvua hizo.

Hata hivyo Dkt.Jaffo amebainisha kuwa Serikali inahakisha inapunguza athari za majanga kwa kuboresha ustawi na uthabiti wa watu wake na jamii kama sehemu ya mkakati wa maendeleo kwani majanga matokeo ya maafa yanaathiri mipango na malengo ya maendeleo yake.

“Nachukua fursa hii kuthibitisha dhamira ya Tanzania ya kufanya kazi na WMO, wadau, na Wanachama wengine wa WMO katika kuboresha uwezo wa Mamlaka zetu za Hali ya Hewa kwa manufaa ya watu wetu na mataifa yetu,” amesema Dkt. Jafo huku akibainisha kuwa TMA inatoa usahihi wa utabiri wa hali ya hewa hadi zaidi ya asilimia 86”amefafanua Dkt.Jaffo

TMA inaboresha uwezo wa kufanya kazi kwa watumishi wake ambapo asilimia 14.5 wamepewa ujuzi na maarifa juu ya programu za hadhari katika taasisi mbalimbali za mafunzo ndani na nje ya Tanzania.

Aidha amebainisha kuwa Serikali imeweka kipaumbele katika kuimarisha huduma za hali ya hewa na mifumo ya tahadhari ya mapema kupitia mifumo, Sera na Teknolojia.

“Ni muhimu kujiandaa kupitia mifumo ya tahadhari ya mapema inaweza kupunguza kwa kiasi kikubwa athari na kuokoa maisha ya watu na mali nyingi na kwa umuhimu huo Tanzania imeandaa Mkakati wa Kitaifa wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (2021-2026) pamoja na Mchango wa Kitaifa wa Kukabiliana na Athari za Mabadiliko ya Tabianchi (NDC),” amesema Dkt. Jaffo.

 

 

Next Post
Mbinu za Ulinzi na Usalama Songwe

Mbinu za Ulinzi na Usalama Songwe

Mahakama yasimama kwa muda kuhakiki kitambulisho cha mwandishi

Hukumu kesi ya Lydia Lugaga dhidi ya Damas Ndumbaro yaahirishwa mara ya tatu

Mali,Burkifaso na Niger waanzisha Shirikisho lao (A.E.S)

Mali,Burkifaso na Niger waanzisha Shirikisho lao (A.E.S)

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:1
  • Today's page views 1
  • Total visitors 13,057
  • Total page views 14,802

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In