• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Tuesday, January 13, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Habari

TCB kutoa mikopo ya Sh.Bilioni 300

Yajipanga kuchangia ukuaji wa uchumi

by bajeti
April 9, 2024
in Habari
0
TCB kutoa mikopo ya Sh.Bilioni 300

Mkurugenzi Mtendaji wa  Benki ya Biashara Tanzania (TCB), Adam Mihayo akizungumza na Wahariri wa Vyombo vya Habari (hawapo pichani) jijini Dar es Salaam Aprili 9,2024 katika mwendelezo wa mikutano ya Wahariri wa vyombo vya Habari na Taasisi na Mashirika ya Umma inayoratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina(Picha na mpigapicha wetu)

Share on FacebookShare on Twitter

NA MWANDISHI WETU

BENKI ya Biashara Tanzania (TCB) imesema mwaka huu wa 2024 inatarajia  kutoa mkopo wa Sh Bilioni 300 ili kuinua uchumi wa nchi hasa kwa wajasiriamali.

Hayo yamesemwa Aprili 9.2024 jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa TCB, Adam Mihayo wakati akizungumza na wahariri na waandishi wa habari  ikiwa ni mwendelezo wa mikutano ya taasisi zilizo chini ya Ofisi ya Msajili wa Hazina.

Amesema benki hiyo ambayo mwaka 2025 inafikisha miaka 100 tangu kuanzishwa mwaka 1925, imepitia mengi ingawa sasa inaendelea vizuri na pamoja na mikopo hiyo, imedhamiria ndani ya miaka mitatu kushika nafasi ya tatu kwenye taasisi za fedha nchini.

”TCB inahudumia Watanzania wa makundi zaidi ya Milioni mbili, hivyo ili kufanikisha lengo la kukua kibiashara na huduma, mwaka huu tutatoa mikopo ya Sh.Bilioni 300 kwa wafanyabiashara na wajasiriamali 2,000.

”TCB tumejipanga kuchangia ukuaji uchumi na biashara kwa kufikia watu wengi hasa wajasiriamali. Lakini pia tunarajia faida ya benki yetu kabla ya kodi itaongezeka hadi Sh bilioni 40 na hilo limeoineka kwani katika robo ya kwanza ya mwaka 2024 tumepata faida ya zaidi ya Sh bilioni 10 kutoka Sh bilioni 3 robo ya kwanza ya mwaka 2023,” amesema Mihayo.

Aidha ameongeza kuwa dhamira ya TCB kuwa benki namba tatu kwa ukubwa nchini, itafanikiwa kwani inafikia watu wengi wanaohitaji huduma za kibenki, hivyo kuomba Watanzania kuitumia ili kunufaika kiuchumi.

”Hadi sasa TCB ina matawi 82, ATM 1,031, wakala 6,000 ikiwa  ni ongezeko la wakala 4,416 na mipango yetu ni kuongeza wakala hadi 10,000 na huduma zao zimejiunga na M-KOBA”amebainisha Mihayo

Amefafanua kuwa robo ya mwaka 2023 benki ilitoa mikopo inayofikia Sh bilioni 852 na mwaka huu wametoa Sh bilioni 983 likiwa ni ongezeko la asilimia 15.4, huku ikiwa imeajiri zaidi ya wafanyakazi 1,080.

“Mali za benki yetu zina thamani ya Sh trilioni 1.4 na lengo ni hadi mwisho wa mwaka iwe Sh trilioni 1.7, ila mapato ya robo ya kwanza ya mwaka huu yamefikia Sh bilioni 56.8 ikiwa ni ongezeko la Sh bilioni 13.1 sawa na asilimia 30 ikilinganishwa na mwaka jana ilipokuwa Sh bilioni 43.7.

‘’Gharama kwa ujumla za TCB katika robo ya kwaka 2024 zimefikia Sh.Bilioni 43.2 ikiwa ni ongezeko la Sh.Bilioni 2.5 sawa na asilimia 6.1, huku mwaka 2023 ikiwa Sh ‘’Bilioni 40.7 na kuwa kasi ya ukuaji wa benki hiyo inashajihishwa na maandalizi ya kuelekea maadhimisho ya miaka 100 tangu benki hiyo kuanzishwa”amesema Mihayo

 

Next Post
Rais Samia ashiriki ibada ya Eid El Firti

Rais Samia ashiriki ibada ya Eid El Firti

Arusha-Tanzania

Arusha-Tanzania

Tembo kinara wa migongano baina ya binadamu na wanyamapori

Tembo kinara wa migongano baina ya binadamu na wanyamapori

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:1
  • Today's page views 1
  • Total visitors 13,057
  • Total page views 14,802

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In