• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Wednesday, April 29, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Mazingira

Tembo kinara wa migongano baina ya binadamu na wanyamapori

Serikali yatoa Sh.Milioni 399.4 kwa wananchi walioathiriwa na wanyamapori

by bajeti
April 12, 2024
in Mazingira
0
Tembo kinara wa migongano baina ya binadamu na wanyamapori

Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi Mohamed Nassoro Moyo

Share on FacebookShare on Twitter

 

NA MWANDISHI WETU,LINDI

SERIKALI kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imetoa kifuta jasho cha Sh.Milioni 399 kwa wananchi 1,658 walioathiriwa na wanyamapori wilayani Nachingwea Mkoa wa Lindi.

Hayo yamezungumzwa na Mkuu wa Wilaya hiyo Mohamed Hassan  Moyo wakati akizungumza na waandishi wa habari Aprili 9, 2024 katika ziara ya kuelezea jitihada zinazofanywa na Serikali kupitia Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) katika kukabiliana na migongano baina ya Binadamu na Wanyamapori.

Amesema Serikali kupitia utaratibu wake wa kifuta jasho na kifuta machozi, wananchi zaidi ya 1658 wa wilaya hiyo walipatikana na kugawiwa fedha hizo ambazo zilitoka mwaka 2023 kiasi cha  Sh.Milioni 399.4, ambapo wote waliostahili walipatiwa.

”Wilaya yangu imekuwa ikikabiliwa na changamoto kubwa ya mgongano baina ya Binadamu na Wanyamapori na Tembo ndio anayetajwa kuhusika zaidi kwenye migongano hiyo.

”Tembo wanaathiri mali na maisha ya wananchi, lakini pamoja na changamoto hizo kumekuwepo na jitihada nyingi zinazofanywa na Serikali kupitia Mamlaka ya Hifadhi ya Wanyamapori Tanzania(TAWA) na Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori (TAWIRI) katika kuelimisha wananchi mbinu mbalimbali za kukabiliana na wanyamapori pamoja na kuwadhibiti.

“Jitihada za TAWA zimefanyika mara nyingi na mimi mwenyewe nimekuwa nikishiriki, jitihada moja ni kwa kutumia helikopta katika kuwaswaga tembo ili warudi hifadhini ,” amesema Moyo

Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea mkoania Lindi Mohamed Hassan Moyo mwenye (kanzu) akiwa na maofisa wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori nchini (TAWA) Aprili 9,2024

Akizungumzia kuhusu jitihada zinazofanywa na TAWA Katika kukabiliana na migongano baina ya Binadamu na Wanyamapori  Kanda ya Kusini Mashariki, Mhifadhi Mkuu Kitengo cha Oparesheni, Linus Chuwa amesema TAWA imeanzisha vituo 10 vya Askari wa kukabiliana na wanyamapori hao ambapo vitano kati ya 10 ni vya kudumu  na vingine  vitano ni vya muda mfupi hasa pale matukio ya wanyamapori hao yanapojitokeza.

Ameongeza kuwa TAWA imenunua gari jipya katika Kituo cha Malola ambalo hutumiwa na Askari wa kituo hicho,kununua ndege nyuki (drones) maalumu kwa ajili ya kuswaga tembo ambazo zilitumika katika zoezi la kurudisha tembo hifadhini mwaka 2023, zoezi ambalo linatajwa kufanikiwa kwa kiasi kikubwa.

Chuwa amebainisha kuwa TAWA  imepeleka Askari wa Wanyamapori wa vijiji 41 (VGS)  katika Chuo cha Likuyu Sekamaganga kwa ajili ya kupatiwa elimu ya kudhibiti wanyamapori ambapo wakati mwingine askari hao hutumiwa na Mamlaka hiyo katika matukio mbalimbali ya kudhibiti wanyamapori hao.

Kwa upande wake, Afisa habari wa TAWA, Beatus Maganja amesema lengo kuu la ziara hiyo mkoani humo ni kuelezea jitihada mbalimbali zinazofanywa na Serikali kupitia TAWA katika kukabiliana na wanyamapori na kuwahakikishia wananchi kuwa TAWA iko kazini na inafanya kila iwezalo kuwadhibiti wanyamapori hao kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kama vile TAWIRI, GIZ na TANAPA.

Aidha Maganja amefafanua kuwa jitihada zingine zilizofanywa na TAWA kwa kushirikiana na wadau ni pamoja na kuwafunga visukuma mawimbi tembo watatu ambao ni  viongozi wa makundi  na hivyo kufuatilia mienendo yao ili kuwadhibiti kabla hawajafika katika makazi ya binadamu

Next Post
Iran yalipiza kisasi kwa kuishambulia Israel kwa makombora

Iran yalipiza kisasi kwa kuishambulia Israel kwa makombora

Utafiti:Watoto walionyonya maziwa ya mama hufaulu zaidi shuleni

Vituo binafsi vyaongoza kuwafanyia upasuaji wanawake wanaojifungua.

Kuelekea Miaka 60 ya Muungano

Kuelekea Miaka 60 ya Muungano

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:10
  • Today's page views 11
  • Total visitors 15,978
  • Total page views 18,129

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In