NA MWANDISHI WETU
WAKALA wa Barabara Tanzania (TANROADs) wameeleza kuwa ujenzi unaoendelea katika Mradi wa Barabara za Mabasi yaendato Kasi (BRT) Awamu ya Tatu hautaondoa wala kugusa sanamu ya askari iliyopo katika makutano ya Mtaa wa Azikiwe na Samora.
Taarifa ya TANROADs imekuja wakati ambapo ujenzi wa huo ukiendelea katika barabara lililopo sanamu hilo na kuzusha hofu kwa baadhi ya watanzania kuwa na hofu ya kuondolewa kutokana na kuwepo katikati ya barabara.
Kwa mujibu wa taarifa ya TANROADS iliyotolewa Juni 11,2024 na Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma, imeleeza kuwa ujenzi unaoendelea katika Mradi wa BRT Awamu ya Tatu hautaondoa wala kugusa sanamu hilo.
”Hata hivyo, kutokana na ufinyu wa eneo la barabara katika makutano hayo, duara la bustani litapunguzwa bila kuathiri hadhi ya sanamu hiyo na usalama wa matumizi ya barabara
”Tunapenda kufafanua taharuki iliyozuka kwenye mitandao ya kijamii kuhusu Askari Monument ya Dar es Salaam ni kwamba ujenzi unaoendelea katika Mradi BRT Awamu ya Tatu hautaondoa wala kugusa sanamu la askari Monument ya Dar es salaam’’imeeleza taarifa hiyo
Hata hivyo sanamu hilo huchukuliwa kuwa ndio nembo inayolitambulisha Jiji la Dar es Salaam na mikoa mingine nchini Tanzania.
Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan imeendelea kuwekeza katika miundombinu ya barabara hasa katika Mkoa wa Dar es salaam ambapo miradi mingine ya BRT inaendelea kukamilika kutoka Kivukoni –Gongolamboto,Ubungo-Moroco kupitia Mwenge,Mwenge-Tegeta ,Gongolamboto-Mnazi mmoja-Posta na Gongolamboto-Moroco kupitia Buguruni-Karume.
Barabara nyingine ya BRT inayosubiri kuanza kazi ni Mbagala-Kivukoni,Mbagala Moroco kupitia Chang’ombe pamoja na Mbagala-Gerezani.
Miradi ya BRT inayofanya kazi hadi sasa ni Gerezani—Mbezi,Mbezi-Kivukoni,Mbezi-Moroco,Moroco Kivukoni na Moroco-Gerezani
Maeneo hayo ndio yenye barabara rasmi za BRT licha ya kuwa baadhi ya safari za mabasi hayo bado barabara zake hazijajengwa ikiwemo ya Gerezani-Muhimbili




Discussion about this post