• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Monday, May 25, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Habari

Tani dawa za kulevya ‘zautikisa’ mwaka 2023.

Ni ukamataji mkubwa kutokea tangu Tanzania ipate uhuru.

by bajeti
July 13, 2024
in Habari
0
Tani dawa za kulevya ‘zautikisa’ mwaka 2023.

Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kuthibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Tanzania Aretas Lyimo

Share on FacebookShare on Twitter

NA MWANDISHI WETU

KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida tani 1965.34  za dawa za kulevya  ikiwemo heroin zilikamatwa katika kipindi cha mwaka wa 2023 peke yake.

Kiwango hicho kinatajwa kuwa ni mara tano kwa miaka tisa iliyopita ambapo  bangi imeongoza ikifuatiwa na heroin,mirungi  na dawa mpya aina ya methamphetamine zikifikisha uzito kuanzia tani moja na kuendelea.

Kukamatwa kwa tani hizo nchini kwa mwaka mmoja pekee wa 2023 kunaonesha mafanikio kwa mamlaka husika za kupambana na dawa hizo lakini pia ongezeko kubwa la wafanyabiashara hiyo nchini.

Kwa mujibu wa Taarifa ya Hali ya Dawa za Kulevya ya Mwaka 2023 iliyotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu(Sera,Bunge na Uratibu) kupitia Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini (DCEA) imeeleza kuwa kiasi cha tani 1965.34 za dawa za kulevya za aina mbalimbali zilikamatwa nchini kwa mwaka 2023 pekee.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa ukamataji huo ni mkubwa kuwahi kutokea nchini katika historia ya mapambano dhidi ya dawa za kulevya tangu nchi ipate uhuru wake.

‘’Takwimu zinaonesha kuwa mwaka 2023 kiasi cha heroin tani 1.31 ambacho ni sawa na kilogram 1,314.28 zilikamatwa,ukamataji huu ni mkubwa kuwahi kutokea tangu nchi yetu ipate uhuru,na mafanikio haya yamechangiwa na juhudi kubwa zilizofanywa na vyombo vya ulinzi na usalama na ushiriki wa wananchi katika kutoa taarifa.

‘’Kiasi cha bangi tani 1757.56 kilichokamatwa  mwaka 2023 ni zaidi ya mara tano ya kiasi kilichokamatwa kwa miaka tisa iliyopita kuanzia mwaka 2014 hadi 2022 ambacho kilikuwa tani 326.09

‘’Kiasi cha Mirungi tani 202.74 kilichokamatwa kwa mwaka mmoja wa . mirungi kilichokamatwa kwa miaka tisa iliyopita kuanzia 2014 hadi 2022 kikiwa ni tani 177.78’’imeeleza taarifa hiyo

Hata hivyo kiasi cha dawa mpya za kulevya aina ya Methamphetamine kilichokamatwa kwa 2023 pekee kilifikia tani 2.4 ambayo hutengenezwa kwa kutumia kemikali bashirifu huku ukamataji nao ukitajwa kuwa ni  mkubwa kuwahi kutokea katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya.

Katika taarifa yake DCEA inayoongozwa na Kamishna Jenerali Aretas Lyimo imefafanuwa kuwa dawa za kulevya aina ya Cocaine  ilikamatwa kiasi cha kilo3.04 mwaka wa 2023 pekee ambapo hali hiyo inaashiria kuwa dawa hiyo haipatikani kwa wingi hapa nchini ambapo mwaka 2016 zilikamatwa kilo 18.52

DCEA imeongeza kuwa vitengo vya afya ya akili kwenye vituo vya  huduma za afya viliwahudumia watu wenye uraibu wa dawa za kulevya wapatao 903,062

Mkazi wa Ilala jijini Dar es Salaam Hamis Jumanne amesema hizo ni tani nyingi sana na kama zingefika zote kwa watanzania maana yake hata wale waliofika kutibiwa wangeozeka mara mbili

‘’Mifuko 20 ya saruji inatengeneza tani moja sasa tani 1965.34 sawa na mifuko mingapi ya saruji? Kwa ufupi kazi imefanyika kubwa na wanapaswa kupongezwa waliohusika na oparesheni hiyo’’amesema Jumanne

Next Post
Kigoma-Tanzania

Kigoma-Tanzania

TARI yagundua mbegu mpya 16

TARI yagundua mbegu mpya 16

Rais Samia Suluhu Hassan ahutubia Kilele cha Wiki ya Wazazi- Katavi

Rais Samia Suluhu Hassan ahutubia Kilele cha Wiki ya Wazazi- Katavi

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:0
  • Today's page views 0
  • Total visitors 16,454
  • Total page views 18,665

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In