• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Tuesday, January 13, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Habari

Mapya yaibuka kesi ya Lydia Lugaga dhidi ya Damas Ndumbaro

Ni miezi sita imepita,faili halijafikishwa Mahakama ya Wlaya

by bajeti
July 17, 2024
in Habari
0
Mahakama yasimama kwa muda kuhakiki kitambulisho cha mwandishi
Share on FacebookShare on Twitter

NA MWANDISHI WETU

LICHA ya Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Ardhi kufuta hukumu iliyotolewa na Mahakama ya Wilaya ya Ilala inayomhusu Lydia Paulo Lugaga dhidi ya Damas Daniel Ndumbaro na kuamuru kusikilizwa upya chini ya Mwenyekiti mwingine, faili la kesi hiyo halijapekekwa Mahakama ya Wilaya  hadi sasa.

Hukumu hiyo ya kesi ya Rufaa namba 253/2022 ilitolewa Desemba 5,2023 iliamuru kesi hiyo kusikilizwa upya chini ya Mwenyekiti mwingine  katika Mahakama ya Wilaya lakini faili hilo halijapelekwa hadi sasa kama Mahakama Kuu Division ya Ardhi ilivyoamuru  ambapo limetimiza miezi sita na siku kadhaa.

Kesi hiyo ya mgogoro wa ardhi iliyokuwa chini ya Naibu Msajili Mfawidhi wa Mahakama Kuu Division  ya Ardhi  Crecensia Kisongo ilisikilizwa kwa njia ya maandishi kwa pande zote kukamilisha taratibu zilizohitajika.

Uamuzi wa kusikilizwa shauri hilo kwa njia ya maandishi ulifikiwa Septemba 11,2023 baada ya wakili wa Damas Ndumbaro,Neema Massame  kuiomba Mahakama hiyo kusikiliza shauri hilo kwa njia ya maandishi.

Akizungumzia uamuzi wa Mahakama Kuu Divisheni ya Ardhi ,jijini Dar es Salaam Wakili wa mlalamikaji Lydia Paulo Lugaga,Pasensa Dickson amesema wao walikuwa na sababu zaidi ya nane za kupinga hukumu hiyo iliyotolewa na Mahakama ya Wilaya ya Ilala.

Amesema waliwasilisha rufaa yao ya mgogoro wa ardhi kutokana na hukumu iliyotolewa na Mahakama ya Wilaya ya Ilala chini ya Mheshimiwa Kirumbi.

Dickson ameongeza kuwa walikataa rufaa hiyo wakiwa na sababu zisizopungua nane na baada ya kuiwasilisha  kwa Mahakama Kuu ilisikilizwa kwa njia ya maandishi.

“Mahakama Kuu ilikubaliana na rufaa yetu na ilitoa hukumu tarehe 5 Desemba 2023 ambapo Mahakama ilijiridhisha kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Ardhi la Wilaya alishindwa kuzingatia Kanuni 19 (2).

“Ni takwa la kisheria kwamba katika maamuzi lazima Wazee wa Baraza watoe maoni yao kwa njia ya maandishi ambayo ni maelezo ya kisheria na Mwenyekiti atatoa hukumu kutokana na maelezo ya wazee wote hao.

“Sasa Jaji kapitia hukumu na kagundua kuwa Mzee mmoja wa Baraza hakuandika maoni yake hivyo ameamuru shauri hilo lisikilizwe upya chini ya Mwenyekiti mwingine katika Mahakama ya Wilaya na mteja wangu alipwe gharama zote za kesi hiyo”amesema Dickson

Akizungumzia kuhusu faili hilo kupelekwa Mahakama ya Wilaya,Dickson amesema bado wanaendelea kufuatilia hadi sasa ili faili hilo liweze kupelekwa Mahakama ya Wilaya kama hukumu ilivyoeleza ingawa ni muda mrefu umepita.

Amesema amekuwa akifuatilia kwa muda mrefu na kuahidiwa kuwa faili hilo lingepelekwa ili kesi ianze kusikilizwa lakini kila anapofuatilia kujua kama limepelekwa anaambiwa bado.

‘’Tunaiachia Mahakama kwa kuwa jambo hili ni la kisheria hivyo tunaamini ipo siku faili hilo litapelekwa Mahakama ya Wilaya na kesi itasikilizwa upya ”amesema Dickson

Katika maelezo ya hukumu hiyo iliyoandikwa kwa lugha ya kiingereza, Naibu Msajili Mfawidhi wa Mahakama Kuu Division  ya Ardhi  Crecensia Kisongo alikubaliana na hoja ya nane ya mkata rufaa.

Naibu Msajili Mfawidhi wa Mahakama Kuu Division  ya Ardhi  Crecensia Kisongo ameleza kuwa:

Hearing of the appeal proceeded by way of written  submissions,where,the appellant was represented by Mr.Pasensa Dickson Kurubone,learned advocate and respondent  was represented by Ms Neema Massame,Learned advocate.

“For the reasons that will be advanced later, I will start with the 8th ground  of appeal that, the honorable tribunal erred in law by conducting a case in contravention of regulation 19(2) of the Court (District Land and Housing Tribunal)Regulation,G.N.No,174 of 2002.

“Arguing in support of the 8th ground of appeal, Mr. Kurubone submitted that, the trial Chairperson did not require assessors to give their opinion  in writing and their opinion were note read to the parties as require by law contrary to regulation  19(2) of the District Land and Housing Tribunal)Regulation ,GN No.174/2002

“I further took time to go through  the proceeding of the tribunal and found that ,during the hearing of the matter, the tribunal was composed of two assessors namely ,Mwakalasya and Jokha”ameeleza Naibu Msajili Mfawidhi Kisongo

Naibu Msajili Mfawidhi  Kisongo‘ amebainisha kuwa the proceedings of 03rd October,2022 reveal that, the tribunal made an order for the assessors to give their opinion before 07 November,2023.However ,only MWAKALASYA gave his opinion in writing on 03 October.

“I could not find the opinion of Jokha in the proceedings of the tribunal .Regulation 19(2) of the Court(District Land and Housing Tribunal)Regulation ,(Supra)provides that

“Notwithstanding sub-regulation (1)the Chairman shall before making his judgment, require every assessor present at the conclusion of hearing to give his opinion in writing and assessor may give his opinion in Kiswahili,I declare both the proceedings and judgment of the tribunal a nullity and are accordingly nullified.”amebainisha Naibu Msajili Mfawidhi Kisongo

Next Post
RUKWA GIRLS

Rais Dkt.Samia:Amani,utulivu na usalama tulionao ni kwa sababu walimu mnatengeneza watu wazuri

Maelfu ya wananchi wa Rukwa  walivyomlaki Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan

Maelfu ya wananchi wa Rukwa walivyomlaki Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan

RC Makonda ateta na Kiongozi wa Kanisa Halisi la MUNGU BABA

RC Makonda ateta na Kiongozi wa Kanisa Halisi la MUNGU BABA

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:9
  • Today's page views 9
  • Total visitors 13,065
  • Total page views 14,810

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In