• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Tuesday, January 13, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Mazingira

Watanzania watakiwa kulinda amani,matunda yake yanawafaidisha wote

by bajeti
July 26, 2024
in Mazingira
0
Watanzania watakiwa kulinda amani,matunda yake yanawafaidisha wote

Watumishi wa Halmashauri na taasisi mbalimbali zilizopo Wilaya ya Magu mkoani Mwanza wakishiriki zoezi la usafi wa mazingira Julai 25,2024 katika eneo la Hospitali ya Wilaya ya Magu ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku ya Mashujaa inayoadhimishwa kila ifikapo Julai 25 ya kila mwaka.

Share on FacebookShare on Twitter

NA MWANDISHI WETU,MWANZA

WATANZANIA wametakiwa kuwaenzi Mashujaa waliopoteza Maisha yao Wakiutetea, Kuupigania na Kulinda  Uhuru wa Tanzania kwa kulinda amani iliyopo ambayo matunda yake yanamfaidisha kila mmoja.

Mbali na hilo lakini pia wametakiwa kuienzi misingi imara ya kizalendo ya amani na upendo iliyojengwa na waasisi wa Taifa  ikiongozwa na Baba wa Taifa Hayati Mwalimu  Julius Kambarage Nyerere na Sheikh Abeid Amani Karume.

Wito huo umetolewa Julai 25,2024 na Katibu Tawala wa Wilaya ya Magu mkoani Mwanza Jubilate win Lawuo wakati wa kuadhimisha siku ya mashujaa inayoadhimishwa kila ifikapo Julai 25 ya kila mwaka.

Lawuo amesema ni muhimu  kwa Wananchi wa Magu na maeneo mengine ya Tanzania kuendelea kuwaenzi Mashujaa kwa kuwa Wazalendo na kulinda amani ya nchi kwani ndio Msingi wa Maendeleo ya Taifa.

Amesema  watanzania wote wanatakiwa kuienzi misingi imara ya kizalendo ya amani na upendo iliyojengwa na waasisi wa Taifa ikiongozwa na Baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere na Sheikh Abeid Amani Karume, misingi ambayo matunda yake yanawafaidisha watanzania wote hivyo ni muhimu kujipanga ili kurithisha vizazi vijavyo.

“Tumekuja hapa kwa ajili ya kumbukumbu ya wazalendo wetu waliojitoa kipindi hicho katika kulipigania Taifa letu na matunda yake tunayaona hadi leo na vizazi vyetu vitakuja kufaidi matunda haya hivyo ni vema tujipange kurithisha vizazi vijavyo” amesema Lawuo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Magu Mohamed Ramadhani amebainisha kuwa Magu inawakumbuka mashujaa kwa kujitoa kwao na kusababisha Taifa kupata ukombozi ambao hadi sasa watanzania wanaendelea kufaidi matunda yaliyotokana na kujitoa kwao.

‘’Funzo kwetu ni kuwa wazalendo kwa nchi yetu kama walivyokuwa Mashujaa wetu ambao walijitoa kwa hali na mali’’ameongeza Ramadhani

Hata hivyo Ramadhani amewakumbusha  Wananchi kutunza mazingira ya Wilaya  kwa ajili ya Afya ya Jamii huku akiwahimiza kufanya usafi kuwa sehemu ya maisha yao ya kila siku na sio kusubiri matukio maalumu.

Akizungumza kwa niaba ya viongozi wa Dini na Shekh Mkuu wa Wilaya ya Magu,Shekh wa Kata ya Isandula Majaliwa Rashid ambaye amesema viongozi wa dini wataendelea kuwakumbuka mashujaa kwa kuwaombea dua kwa mazuri waliyofanya na kusema kuwa wataendelea kuliombea Taifa liendelee kuwa na amani, upendo na mshikamano.

Wilaya ya Magu katika kuadhimisha siku hiyo pia iliambatana  na shughuli mbalimbali kufanya usafi katika Hospitali ya Wilaya ya Magu na maeneo mengine ikiwemo dua na sala maalumu za kuwaombea Mashujaa waliopoteza maisha yao na walio hai na  kuombea Amani .

Kila ifikiapo Julai 25 ya kila mwaka,Tanzania huadhimisha siku ya kuwakumbuka Mashujaa waliopoteza Maisha yao Wakiutetea, Kuupigania na Kulinda  Uhuru wa Tanzania.

 

Next Post
Tani dawa za kulevya ‘zautikisa’ mwaka 2023.

‘Mapapa’ wa dawa za kulevya sasa yatumia drone,mitandao ya kijamii

Makamu wa Rais Dkt Mpango asafiri kwa Treni ya SGR

Makamu wa Rais Dkt Mpango asafiri kwa Treni ya SGR

Jeshi la Polisi Tanzania laonya watumiaji mitandao ya kijamii

Jeshi la Polisi Tanzania laonya watumiaji mitandao ya kijamii

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:9
  • Today's page views 9
  • Total visitors 13,065
  • Total page views 14,810

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In