• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Thursday, January 22, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Mazingira

Tanzania kutumia Nyuklia kuzalisha umeme,mahitaji yanakua kwa asilimia 10 hadi 15 kwa mwaka

Mashapo ya madini ya urani yafikia tani 58,500

by bajeti
September 12, 2024
in Mazingira
0
Tanzania kutumia Nyuklia kuzalisha umeme,mahitaji yanakua kwa asilimia 10 hadi 15 kwa mwaka

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Dotto Biteko akiwasilisha Mpango wa Tanzania katika Mkutano wa Pili wa Masuala ya Nishati ya Nyuklia kati ya Marekani na nchi za Afrika (US-Africa Nuclear Energy Summit) unaofanyika jijini Nairobi,Kenya Agosti 29,2024.(Picha na mpigapicha Maalum)

Share on FacebookShare on Twitter

NA ONWM -WN

TANZANIA imeeleza mpango na utayari wake katika uendelezaji wa nishati ya nyuklia ikiwa ni moja ya vyanzo mbadala vya nishati safi ya umeme kwa maendeleo ya kiuchumi na ustawi wa jamii.

Hayo yamebainishwa Agosti 29,2024 na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko wakati akiwasilisha Mpango wa Tanzania katika Mkutano wa Pili wa Masuala ya Nishati ya Nyuklia kati ya Marekani na nchi za Afrika (US-Africa Nuclear Energy Summit) unaoendelea jijini Nairobi,Kenya.

Amesema Tanzania iko tayari kuendeleza nishati ya nyuklia ikiwa ni moja ya vyanzo vitakavyoiwezesha nchi kuwa na umeme wa kutosha na wa uhakika ambayo inakidhi viwango vya kimataifa katika uhifadhi wa mazingira.

 “Utayari wa Tanzania katika kuendeleza na kutumia nishati ya nyuklia unatiliwa mkazo katika Sera ya Nishati ya mwaka 2015, Sera ya Madini ya mwaka 2009,

”Mpango Kabambe wa Kuendeleza Sekta ya Umeme na Mkakati wa Nishati Jadidifu ambapo nyaraka zote hizi zinatambua umuhimu wa nyuklia kukidhi mahitaji ya nishati nchini.” amesema Dkt. Biteko 

Amebainisha kuwa  chini ya uongozi wa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, Serikali inaendelea kuchukua hatua muhimu zitakazowezesha matumizi ya nishati ya nyuklia kama moja ya vyanzo vya nishati safi ambapo hadi sasa Tanzania ina mashapo ya madini ya urani takriban tani 58,500 ambayo yanaweza kutumika kama chanzo cha uzalishaji wa nishati ya nyuklia.

Amefafanua kuwa, uwepo wa vyanzo mbadala vya umeme utawezesha nchi kuboresha mashirikiano yake ya kibiashara na nchi nyingine ndani na nje ya Bara la Afrika na hivyo kuboresha uchumi wa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.

“Mpango huu wa kuwa na umeme wa kutosha utawezesha hatua ya kuunganisha gridi za umeme miongoni mwa nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika na baadaye katika maeneo mengine ya Bara hili.” ameongeza Dkt.Biteko

Ametumia mkutano huo kueleza nia ya Tanzania kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo nchi ya Marekani na Bara la Afrika ili kuendeleza nishati ya nyuklia hasa ikizingatiwa kuwa takriban watu milioni 600 barani Afrika na biashara ndogondogo zipatazo  milioni 10 bado zinakabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa umeme wa uhakika.

Hata hivyo Dkt.Biteko ameeleza kuwa mahitaji ya umeme nchini Tanzania yanakua kwa asilimia 10 hadi 15 kwa mwaka na ili kufikia malengo ya maendeleo endelevu, Tanzania imepanga kuzalisha megawati 10,000 za umeme ifikapo mwaka 2030.

Kwa upande wake, Msaidizi Maalum wa Rais wa Marekani wa Masuala ya Uhifadhi wa Mazingira, Fedha na Uvumbuzi, Nana Ayensu amesema kuwa mkutano huo ni muhimu kwa nchi washiriki katika kufungua milango ya uendelezaji wa nishati ya nyuklia ambayo ni rafiki kwa matumizi ya binadamu na hifadhi ya mazingira ikiwemo kuimarisha ushirikiano miongoni mwa nchi husika.

Ameongeza kuwa nishati ya nyuklia itafanikisha ajenda za kimataifa za nishati safi zinazoendelea ikiwemo nishati safi ya kupikia inayopigiwa chapuo kimataifa huku kinara wake akiwa ni Rais, Dkt.Samia Suluhu Hassan.

Akizungumzia utayari wa nchi yake, amesema Marekani ipo tayari kushirikiana na nchi za Afrika ili kuendeleza matumizi ya nishati ya nyuklia ambayo inatoa uhakika wa upatikanaji  nishati na kuchochea maendeleo ya kiuchumi.

Mkutano huo unaojumuisha viongozi katika Sekta ya Nishati, Watunga Sera na Wataalam kutoka nchi mbalimbali barani Afrika.

Next Post
DCEA yamnasa wakala wa dawa za kulevya Tanzania,yumo bibi wa miaka 70

DCEA yamnasa wakala wa dawa za kulevya Tanzania,yumo bibi wa miaka 70

Kamishna Jenerali Lyimo:Tutavunja mitandao yote mikubwa ya dawa za kulevya

Kamishna Jenerali Lyimo:Tutavunja mitandao yote mikubwa ya dawa za kulevya

Mamlaka ya Rufani ya Zabuni za Umma(PPAA) kutoa elimu kwa wazabuni

Mamlaka ya Rufani ya Zabuni za Umma(PPAA) kutoa elimu kwa wazabuni

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:18
  • Today's page views 18
  • Total visitors 13,277
  • Total page views 15,025

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In