• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Tuesday, January 13, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Mazingira

REA kugawa majiko banifu 790 kwa wananchi Gairo

katika Maonesho ya Samia Kilimo Biashara Expo 2024

by bajeti
October 7, 2024
in Mazingira
0
REA kugawa majiko banifu 790 kwa wananchi Gairo

Mhandisi wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Deusdedith Malulu akiwaonesha wananchi wa Wilaya ya Gairo mkoani Morogoro majiko sanifu yanayotunza mazingira na afya za binadamu Oktoba 6,2024 wakati wa Maonesho ya Samia Kilimo Biashara Expo 2024 yanayofanyika katika Kijiji cha Leshata wilayani humo.(Picha na mpigapisha wetu)

Share on FacebookShare on Twitter

NA MWANDISHI WETU,MOROGORO

WANANCHI wa Wilaya ya Gairo mkoani Morogoro wametakiwa kutumia Majiko  Banifu yanayotolewa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) katika Maonesho ya Samia Kilimo Biashara Expo 2024, kwa kuwa yanatunza mazingira na rafiki kwa afya ya watumiaj.

Hayo yamebainishwa Oktoba 6, 2024 na Mkuu wa Wilaya ya Gairo mkoani Morogoro,Jabir Makame wakati akizungumza na wananchi mara baada ya kutembelea banda la REA yanapofanyika maonesho hayo kwa msimu wa tatu katika kijiji cha Leshata wilayani humo.

Makame ameeleza kuwa, majiko banifu ni rafiki na salama kwa afya ya watumiaji nchini na kuwasisitiza wananchi kuyatumia kwa kuwa yanauzwa na kupatikana kwa gharama  nafuu.

Makame amesema wananchi hao wanakwenda kushuhudia mageuzi makubwa ya utunzaji wa mazingira kupitia Mkakati wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia ambao kinara wake ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Aidha ameeza kuwa  Gairo inatekeleza kampeni ya ‘’URITHI WA KIJANI yenye lengo la kukabiliana na changamoto ya mabadiliko ya tabianchi ambayo yana athari katika Sekta ya Kilimo na Mifugo.

Ametaja wadau wanaoshiriki kuwa ni pamoja na Mashirika ya Mazingira, Kampuni za Gesi, Kampuni zinazotengeneza mkaa mbadala, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira pamoja na Wizara ya Nishati.

Naye, Mhandisi wa REA Deusdedith Malulu ameongeza kuwa, majiko hayo yanatunza mazingira kwa kutumia kiasi kidogo cha mkaa na ufanisi wake ni mkubwa.

“Majiko haya hayaruhusu hewa ya mkaa ambayo ni hatari kwa watumiaji kutoka nje kwa aina ya muundo wake na hivyo kuwa rafiki kwa mazingira” amesema Mhandisi Maluku

Mhandisi Malulu ameongeza kuwa kupitia maonesho hayo  wananchi wa wilaya hiyo wameanza kupatiwa majiko banifu na REA imeaza kutoa majiko 790 ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha ajenda ya matumizi ya nishati safi ya kupikia nchini.

Next Post
IGP Wambura atua Katavi kuangalia hali ya usalama

IGP Wambura atua Katavi kuangalia hali ya usalama

Makamu wa Rais Dkt.Mpango akutana na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza

Makamu wa Rais Dkt.Mpango akutana na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza

Spika Dkt.Tulia akutana na Rais Sulyok wa Hungary

Spika Dkt.Tulia akutana na Rais Sulyok wa Hungary

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:6
  • Today's page views 6
  • Total visitors 13,062
  • Total page views 14,807

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In