• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Sunday, January 18, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Siasa

ACT-Wazalendo kufanya uchunguzi huru wa matukio ya utekaji, utesaji, upoteaji na mauaji ya raia

by bajeti
September 24, 2025
in Siasa
0
ACT-Wazalendo kufanya kampeni nchi nzima Uchaguzi Serikali za Mitaa

Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo Dorothy Semu

Share on FacebookShare on Twitter

NA MWANDISHI WETU

CHAMA Cha ACT Wazalendo kimesema kitafanya uchunguzi huru na wa kitaalam wa matukio yote ya utekaji, utesaji, upoteaji na mauaji ya raia ikiwemo kuchukua hatua dhidi ya wote wanaohusika ndani ya siku 100 baada ya kushika dola.

Hata hivyo chama hicho kimedhamiria kuhakikisha kuwa Tanzania inakuwa sehemu salama kwa wananchi kufanya shughuli zao, kuishi na kupiga hatua za maendeleo bila hofu, wasiwasi na mashaka.

Hayo yamebainika katika Ilani ya Uchaguzi ya chama hicho ya 2025-2030   iliyozinduliwa Septemba 22,2025 jijini Dar es Salaam ikiwa itapata ridhaa ya kuchaguliwa na wananchi katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29,2025 na kuunda Serikali itakayoundwa na chama hicho.

Hata hivyo ACT-Wazalendo imezindua Ilani yake wakati ambapo mgombea wake wa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Luhaga Mpina akienguliwa kugombea nafasi hiyo na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) ambapo awali alikuwa amepitishwa na kukabidhiwa gari aina ya Land Cruiser kwa ajili ya kufanyia kampeni zake kabla ya kuwekewa pingamizi na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Johari Hamza.

Ilani hiyo imebainisha kuwa katika kuhakikisha Ulinzi na Usalama wa Raia na Serikali ya ACT Wazalendo itafanya uchunguzi huru na wa kitaalam wa matukio yote ya utekaji, utesaji, upoteaji na mauaji ya raia na kutoa ripoti ya kina kwa umma na kuchukua hatua dhidi ya wote wanaohusika ndani ya siku 100.

Mbali na hilo lakini pia itatoa msaada wa kisaikolojia, kijamii na kiuchumi kwa watu na jamii zilizoathiriwa na vitendo vya ukiukwaji haki.

“ACT-Wazalendo italiunda upya Jeshi la Polisi na kuliimarisha kitaaluma, kwa kulitoa kuwa chombo cha mabavu‘ (police force) na kulifanya kuwa chombo cha huduma (police service)

“Itakomesha vitendo vya utekaji, utesaji, uonevu, ubaguzi wa kiitikadi, unyanyasaji, uvunjifu wa haki za binadamu na mauaji ya raia na kuvunja magenge yote ya uhalifu na kuwachukulia hatua kali watu wote wanaohusika na vitendo hivyo.

“Itaipa uwezo wa kibajeti, kiweledi na kisheria Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora na Ofisi ya Uwakili wa Umma, ili kusimamia vyombo vya dola kulinda haki na usalama wa watu na mali zao kwa uhuru”imeeleza Ilani hiyo.

Ilani hiyo imefafanuwa kuwa itafanya mapitio ya Sheria ya Usalama wa Taifa na kuwaondolea mamlaka waliyopewa ya kukamata na kuwashikilia watu bila kuchukua hatua za sheria (arbitrary detention) na kufanya marekebisho ya sheria ya ugaidi na sheria nyingine kandamizi zinazotumika kiholela kwa ajili ya kupora haki za wananchi.

“ACT-Wazalendo itatunga sera ya mfumo wa Haki za Kijinai [Criminal Justice Policy] ili kuimarisha mifumo ya kitaasisi na kiuendeshaji wa taasisi za usimamizi wa jinai.

“Itaboresha mfumo wa upelelezi wa mashauri kwa kusimamia na kuweka ukomo wa muda wa upelelezi kwa makosa yote ili kupunguza mrundikano wa kesi.

“Itatunga sheria moja ya dhamana (Bail Act) kwa makosa yote ya jinai na kuweka utaratibu wa dhamana kwa makosa yote”imeongeza Ilani hiyo

Aidha chama hicho kupitia Ilani yake imeongeza kuwa itaimarisha utaratibu wa upatikanaji taarifa, uchunguzi na doria kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama ili kudhibiti matukio ya uhalifu na mauaji mijini na vijijini

Kwa upande wake Kiongozi wa chama hicho Doroth Semu amesema ACT Wazalendo inakuja na matumaini mapya na wanatambua kwamba Taifa linaweza kuongozwa kwa haki, uwazi, na misingi ya ushiriki wa wananchi kikamilifu.

“Tumedhamiria kujenga Taifa la Wote kwa Maslahi ya Wote, Taifa ambalo kila Mtanzania, popote alipo, anaweza kuishi kwa heshima, kupata huduma bora, kufanya kazi kwa uhuru na kunufaika na rasilimali za nchi yake.

“Ilani hii inabeba maono ya kuijenga Tanzania mpya – Taifa la Wote kwa Maslahi ya Wote.

“Taifa ambalo watoto wote wanapata elimu bora bila kulipishwa, wala kuchangishwa na kila mwananchi anapata huduma ya afya bila kuingia kwenye umasikini wakiwemo wakulima, wafugaji, wavuvi na wamachinga wanatambuliwa, kuheshimiwa na kuwezeshwa”amebainisha Semu

 

Next Post
Serikali ya ADA-TADEA kufuta upendeleo,rushwa na ufisadi

Serikali ya ADA-TADEA kufuta upendeleo,rushwa na ufisadi

Serikali ya SAU kuwadhibiti wanaharakati wanaofadhiliwa  na watu wasio wema

AAFP  kujenga ukuta mipaka yote ya Tanzania

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:27
  • Today's page views 27
  • Total visitors 13,184
  • Total page views 14,930

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In