• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Friday, December 5, 2025
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Siasa

Wanafunzi elimu ya juu kupigwa marufuku kupanga vyumba mtaani

Yadaiwa kunaathiri masomo na maadili  yao

by bajeti
October 9, 2025
in Siasa
0
Serikali ya ADA-TADEA kuwalipa askari walioshiriki vita vya Kagera

Mgombea wa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa Cha African Democratic Alliance(ADA-TADEA) Georges Bussungu

Share on FacebookShare on Twitter

NA MWANDISHI WETU

SERIKALI ya Chama Cha African Democratic Alliance(ADA-TADEA) itapiga marufuku wanafunzi elimu ya juu (wanachuo) kupanga nyumba  mitaani ikiwa itapata ridhaa ya kuchaguliwa na wananchi kuongoza nchi katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29,2025.

Hata hivyo ADA-TADEA imebainisha kuwa mabadiliko ya Elimu yatafuata mkondo wa Serikali ya awamu ya kwanza ambapo elimu kuanzia chekechea hadi Chuo Kikuu itakuwa bure.

Hayo yamebainika ndani ya Ilani ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025-2030 ya chama hicho  iliyozinduliwa Septemba 14,2025 Mbagala mkoani Dar es Salaam muda mfupi baada ya kuzindua kampeni za urais,ubunge na udiwani ili kuwanadai wagombea wao nchi nzima.

Ilani hiyo imebainisha kuwa wanachuo wote watakuwa wanalipwa posho ya kujikimu kila mwezi, na utaratibu wa kupewa malazi na chakula bure utarejeshwa ili wasome kwa makini na bidii zaidi.

 “Aidha, vyuo vyote ni lazima viwe na hosteli zao, itakuwa marufuku wanachuo kupanga ovyo mitaani kwa kuwa imeonesha kuathiri Masomo na Maadili yao.

“Chama cha African Democratic Alliance (ADA-TADEA) kitaweka mkazo maalum katika maktaba na elimu mtandao (libraries and eLearning) kwenye shule zote.

“Kutunga sheria maalum kuhakikisha taasisi zote za Serikali zinatumia mitandao wa Serikali kuhakikisha maeneo yote ya elimu yanatumia mtandao bila vikwazo”imeongeza Ilani hiyo

Mbali na hilo, ADA-TADEA itaanzisha kanzidata ya wahitimu wote kufahamu mwaka waliomaliza na utaalamu waliosomea ambapo ajira zitafuata umalizaji wao na  aliyeanza kumaliza chuo ndiye atakayekuwa wa kwanza kupata ajira {First In First Out [FIFO]} na elimu  itakuwa inaandaliwa kulingana na mabadiliko ya teknolojia na mwelekeo wa Dunia.

Serikali ya ADA=TADEA itaangalia upya viwango vya kuajiri na kusajili watumishi wa umma akiwemo  Mwalimu wa Tanzania.

“Mtu akiajiriwa, Chama cha African Democratic Alliance (ADA-TADEA) kitahakikisha kinaboresha maslahi ya Waalimu wote.

“Walimu ambao wanapangiwa kwenye maeneo yenye changamoto nyingi watapewa posho maalum ikiwemo posho ya nyumba (accommodation allowance),

“Serikali itahakikisha nyumba za Walimu zinajengwa haraka kwenye maeneo ambayo ni vigumu kufikika na yenye mazingira magumu”imeongeza Ilani hiyo

Ilani hiyo imefafanuwa kuwa Ukaguzi wa Shule utaangaliwa upya na kuboreshwa ili kujua hali ya Waalimu na Wanafunzi ikoje na kama wanawajibika

“Tutahakikisha wazazi wanajihusisha na wanafunzi, ikiwemo kushiriki kwenye kamati za maendeleo ya shule na kamati zake ndogo, hii itasaidia kuleta utaalamu na weledi mbalimbali walionao wazazi.

“Hali hiyo itongea kiwango cha elimu kwa shule”imeleza Ilani hiyo

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Chama hicho Salehe Msumari ameelezea ilani yao kuwa ni bora kuliko za vyama vingine  na kwamba ADA-TADEA kimekuwa na kuendeela kupanuka kutokana na hamu ya wananchi kujikomboa kutoka kwenye uchumi hodhi,utumwa wa fikra  za ukoloni mambo leo na nguvu ya ubeberu

“Chama hiki kiliundwa  kwa lengo la kuleta mabadiliko kawa amani ya kisiasa  nchini Tanzania  yaliyoongozwa na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Tanzania African National Union (TANU) na Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  wakati wa awamu ya kwanza Hayati Oscar Salathiel Kambona(1925-1997)”amesema Msumari

 

Next Post

Wamiliki wa  nyumba kuzuiwa kujenga frame za maduka katika maeneo ya makazi

Mradi wa Maji wa Miji 28 mkoani Niombe utakavyoondoa changamoto ya maji safi na salama

Mradi wa Maji wa Miji 28 mkoani Niombe utakavyoondoa changamoto ya maji safi na salama

Kaburi la ajabu la Hayati Rais Laurent-Désiré Kabila wa DRC

Kaburi la ajabu la Hayati Rais Laurent-Désiré Kabila wa DRC

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:25
  • Today's page views 25
  • Total visitors 12,066
  • Total page views 13,719

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In