• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Sunday, April 26, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Mazingira

Maji yaongezeka Bwawa la Nyumba ya Mungu,PBWB yahimiza wananchi kuchukua hatua

by bajeti
April 26, 2026
in Mazingira
0
Bodi ya Maji Bonde la Pangani(PBWB) na mikakati ya kulinda,kuhifadhi vyanzo vya maji,yaonya watumiaji wasiona na  vibali

Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Maji Bonde la Pangani (PBWB)Segule Segule

Share on FacebookShare on Twitter

NA MWANDISHI WETU,KILIMANJARO

MFUMO unaotumiwa na Bodi ya Maji  Bonde la Pangani (PBWB) wa kutoa taarifa kwa wananchi kuhusu hali ya maji katika Bwawa la Nyumba ya Mungu umesaidia kuondokana na maafa kwa  wanaofanya shughuli zao karibu na mito pamoja na maeneo yaliyo bondeni.

Bonde la Pangani ambalo mipaka yake inajumuisha mikoa minne ikiwemo Kilimanjaro,Arusha,Manyara na Tanga  lakini pia hushughulika na maji yaliyopo katika Bwawa la Nyumba ya Mungu ambalo kutumika na Shirika la Umeme nchini (TANESCO) kuzalisha umeme.

Hata hivyo PBWB imetengeneza mfumo wa utoaji taarifa za hali ya maji katika bwawa hilo kila siku ili kuwasaidia wananchi kuchukua tahadhari kabla ya maafa kutokea jambo linalowafanya wananchi kuwa makini pindi tu wanapopata taarifa.

Usimamizi Endelevu wa Rasilimali za Maji katika Bonde la Pangani hufanyika kwa kuzingatia mfumo shirikishi unaotoa fursa kwa jamii katika kupanga na kusimamia matumizi ya maji kama ulivyoainishwa katika mageuzi makubwa ya Sekta ya Maji yaliyofanyika kupitia Sera ya Maji ya Mwaka 2002

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Aprili 25,2026 kwa umma kuhusu hali ya maji kwenye Bwawa la Nyumba ya Mungu na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Maji  Bonde la Pangani (PBWB)Segule Segule amesema kina cha maji hadi kufikia Aprili 25,2026 cha bwawa  ni mita 689.25 juu ya usawa wa bahari  ambapo kina cha juu kabisa cha ujazo  wa bwawa ni mita 688.91 juu y usawa wa bahari

“Kina hicho ni juu ya kina kilichonakiliwa  Aprili 24,2026 kwa sentimita  5(Mita 0.05) ambapo kwa tarehe hiyo kilikuwa mita 689.20.

“Kina hicho ni sawa na sentimita 34(Mita 0.34) juu ya usawa wa juu wa bwawa hivyo tabaka hilo la maji  linapita  kwenye njia ya utoro (spillway) kwenda upande wa chini kwa kupitia Mto Pangani.

“Kufuatia hali hiyo ,mwenendo wa ongezeko la maji ndani ya bwawa kwa siku zilizopita  ni wastani wa sentimita  11 kwa siku”amesema Segule

Maji yakitiririka katika moja ya vyanzo vya Bonde la Pangani

Aidha Segule amebainisha kuwa  maji yanayotoka katika bwawa yataungana na maji yatolewayo na Shirika la Umeme nchini (TANESCO) kiasi cha mita za ujazo 33 kwa sekunde (sawa na lita 330,000/sekunde) ambayo yanatokana na shughuli za uzalishaji umeme na hivyo kiasi cha maji yatakayokapita Mto Pangani(wengine huita Mto Ruvu) kwenda upande wa chini wa mto huo  unaopita  maeneo ya Wilaya za Same(Vijiji vya Marwa na Ruvu),Mwanga(Kijiji cha Kirya),Simanjiro(Vijiji vya Ngage na Lemkuna),Korogwe(Vijiji vya Buiko,Korogwe Mjini,Makayo na Hale) pamoja na Wilaya ya Pangani  yatarajie kupokea maji mengi kuliko hali ya kawaida.

“Tanatoa wito kwa wadau wote hususani wananchi wanaoishi na kufanya shughuli zao chini ya Bwawa la Nyumba ya Mungu pembezoni mwa Mto Pangani pamoja na maeneo yote yanayozunguka bwawa,kuanza kuchukua tahadhari  mapema ikiwezekana kuondoka katika maeneo  hatarishi kwa ajili ya usalama wao  na mali zao.

“Taarifa itaendelee kutolewa ili kuwashirikisha wananchi  kuhusu hali ya Bwawa la Nyumba ya Mungu  kwa kadiri itakavyoonekana inafaa  mpaka pale ambapo hali itakaporejea kuwa ya kawaida”ameeleza Segule

Segule amewaomba wananchi wote wanaopata na kufikiwa na taarifa hizo za hali ya bwawa zinazotelewa mara kwa mara kuwafikishia wenzao ambao pengine kwa namna moja au nyingine hawapati taarifa kwa wakati ili kuepusha madhara yanaweza kutokea.

Bonde la Pangani linahudumia watu zaidi ya Milioni 4.7 hasa katika majiji ya Arusha na Tanga  pamoja na Moshi mkoani Kilimanjaro na sehemu ya Mkoa wa Manyara.

Mbali na kupita katika mikoa minne lakini pia linapita katika wilaya zaidi ya 20 ikiwemo Arusha, Jiji la Arusha,Arumeru(Meru),Simanjiro,Siha,Hai,Moshi Mjini na Moshi Vijijini,Rombo,Mwanga,Same,Korogwe,Korogwe Mjini,Pangani,Jiji la Tanga,Mkinga,Muheza,Handeni,Handeni Mjini,Kilindi ikiwemo na ,Lushoto

 

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:13
  • Today's page views 19
  • Total visitors 15,903
  • Total page views 18,035

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In